Kamati ya Lowassa Kukagua Balozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Lowassa Kukagua Balozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Papaya, Jun 27, 2012.

 1. P

  Papaya Senior Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kamati ya Bunge ya mambo ya nje,ulinzi na usalama imeanza ziara ya siku 14 katika balozi za tanzania kwenye nchi za marekani, ulaya na asia kukagua namna zinavyotekeleza mambo ya sera na uchumi. Ziara ya kamati iyo inayoongozwa na mbunge wa Monduli ilitangazwa jana katika uwanja wa ndege wakati wajumbe 20 wa kamati hiyo na makatibu 6 walipokuwa wanaondoka nchini. Hata hivyo, wakati kamati hiyo ikienda kutembelea balozi hizo, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Benard Membe mwenye dhamana na balozi hizo, alisema ziara hiyo haikuja wakati sahihi, kwa kuwa mkutano wa bunge la bajeti unaendelea. Lakini Lowasa alisema ziara iyo imekuja wakati sahihi kwa kuwa hiyo pia ni kazi ya Bunge.
  Katika ziara hiyo, kamati imegawanyika ktk makundi 6 yatakayotembelea balozi 14 ktk nchi 14.
  Wabunge hao ni yeye Edward Lowasa, Vita Kawawa, Khalifa Suleiman Khalifa, Rachel Mashishanga na Beatrice Shelukindo ambao watatembelea balozi za Canada, Washington na New York, na London.

  Wengine ni Mohamed Ibrahim Sanya, Mchungaji Israel Natse ambao watatembelea New Delhi na Kuala Lumpur.

  Wengine ni Musa Zungu, Hasan Ngwilizi, Bety Machagu na Musa Hasan Musa watakaotembelea Japan na China.

  Kundi jingine litakalokuwa Ujerumani na Sweden linawahusisha Ana Abdalah, John Shibuda na Agustino Masele.

  Wengine akiwamo Mohamed Seif Khatib, Hilda Ngoye na Anastazia Wambura watatembelea balozi za Brussels, Ubelgiji na Geneva.

  Kundi la mwisho linalotembelea Paris na Rome linawahusisha John Chiligati, Eugen Mwaiposa na Masoud Abdalah Salim.

  Ziara hiyo imeonyesha kumshangaza Waziri Membe akisema hajui wanakwenda kufanya nini huko.

  SOURCE:MWANANCHI JUMATANO JUNI 27

  My take
  Kama lengo ni kuangalia utendaji mbona inakuwa Ulaya, Marekani, Canada na Asia peke yake wakati balozi zetu zipo hata huku Africa?? Why now wakati bunge linaendelea wakati wabunge wanatakiwa kuwa bungeni kufatilia bajeti?? Wadau kwa mwendo huu tutakata matumizi yasiyo na tija kwa taifa? Hata uganda kuna balozi, kenya, rwanda! Why Us Europe Asia?
   
 2. v

  vngenge JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Bunge dhaifu letu dhaifu- Mnyika
   
 3. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hawa wakubwa wamebaini kuwa hata huko bungeni hakuna cha maana kinachoendelea zaidi ya umbeya wa kusema hapana kumbe moyoni unamaanisha ndiyo, ili kuepuka haya yote wameona ni bora wakazile hizi ambazo zipo hasa kwa kuzingatia kwa bado siku mbili tu mwaka wa fedha 2011/2012 uishe.

  Balozi za Afrika zimeachwa kwa sababu hakuna maeneo ya kufanya shopping kwa level yao. Sina uhakika kama ziara hii ina umuhimu wowote, hasa ikizingatiwa kuwa balozi nyingi zinalalamika kutokuatiwa fedha za kutekeleza majukumu yao ya kiutendaji achilia mbali hata mishahara tu inachelewa.

  Taarifa kutoka kila Ubalozi zinaandaliwa na kutumwa katika taasisi nyingi tu ya serikali kutegemeana na taarifa husika, na hata wakaguzi wa hesabu wanapokuja pia wanafanya ukaguzi pia wa utekelezaji wa majukumu v/s matumizi. Ziara ya siku moja kutoka Tanzania hadi ulaya/ amerika/Asia itamsaidiaje huyo mbunge kuona uhalisia wa utekelezaji wa majukumu ya balozi zetu?
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Lowassa anakwenda kutafuta uozo mwingine wa Membe kwenye hizo balozi baada ya ile mbinu yao ya kumpakazia huko Sahara/Morocco kushindwa kwa Rais wa Wapigania uhuru wa Sahara kufanya ziara rasmi Tanzania juzi!!
   
 5. W

  WaMzizima Senior Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa mujibu wa Magazeti Kamati ya Ulinzi na mambo ya nje inayoongozwa na Lowassa imeanza kutembelea balozi zetu nje. Mimi hii hainiingii akilini kuanza safari hii wakati huu kwa sababu zifuatazo;

  1. Kikao cha bajeti kinaendelea, jee hii ina maana hao wabunge hawana cha kuchangia kwenye vikao?

  2. Mbona safari zenyewe ni kwa nchi za marekani kaskazini, Ulaya na Asia, hawaendi nchi yeyote Afrika, hii imekaaje?

  3. Inakuwaje wanaenda huko ilhali Waziri husika anadai alikuwa hana taarifa.

  4. Nani anaetoa hizi ruhusa za kamati za bunge kusafiri wakati nyeti (bajeti), kwa nini wasisuburi hadi bajeti iishe?


  Kwa kweli kuna vitu havieleweki nchini kwetu, au hii ni katika kupigana vikumbo kati ya Membe na Lowassa kujipanga na uchaguzi wa 2015.

  Au ndio kujaribu kuhamisha haraka hela uswisi? Yetu macho na masikio
   
 6. T

  Tiote Senior Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is mindless decision, to say the least. Hawa jamaa wameondoka katika kipindi muhimu sana katika machakato wa maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha. kwa kawaida wenyeviti wa kamati hukutana kila wiki kama sehemu ya baraza la uongozi lakini wameamua kuacha hayo yote kwa ajili ya safari, tena mtu anajisifu with alot of gusto kwamba wanafanya safari, wakijua kwamba haina tija. Infact ni safari ya kifisadi.

  Imagine:
  1. Watu hawa hata taarifa kwenye balozi zetu hawajatoa na kueleza madhumuni ya safari zao;

  2. Kwa kawaida safari za kamati huwa wanakwenda kukutana na Kamati za bunge kwenye nchi husika, hawa hata hiyo hawakufanya na kwa hiyo haifahamiki wanakwenda kufanya nini huko na kwa kutumwa na nani;

  3. Choice ya hizo nchi na kuziacha balozi zilizoko katika nchi za Africa ni kiashiria cha wazi kwamba lengo lilikuwa ni kujipatia perdiem allowances na kwenda kuvinjari tu, na si vinginevyo;

  4. Watu hawa wanakwenda kukutana na kitu ambacho tayari kinafahamika i.e. ukata na hali ngumu ya kiutendaji inayotokana na bajeti finyu;

  5. Kama lengo la safari zao ni kukagua matumizi ya balozi zetu, basi hiyo ni kazi ya CAG ambaye taarifa yake ya ukaguzi ilitoka hivi karibuni;

  6. lakini tusilolijua ni kwamba robo ya wajumbe hawa watasafiri na first class wakati waliobaki watasafiria na business class. Hii itaigharimu Ofisi ya Bunge na Serikali zaidi ya shilingi milioni 200 na habari zilizopo ni kwamba ofisi ya Bunge inakabiliwa na upungufu wa fedha za vikao vya wiki hii na wameomba Ofisi ya Waziri Mkuu iwasaidie fedha. Hili limemshangaza hata Lukuvi na Katibu Mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu;

  6. Mwenyekiti wa kamati hii amesafiri na mke wake na walinzi wawili, as if yuko kwenye state visit, na wote hao watakuwa first class. Mheshimiwa Zungu ambaye ni Mwenyekiti wa Bunge amesafiri huku akijua kwamba kwa cheo chake kipya, hastahili kuendelea kuwemo kwenye msafara.

  Kwa ujumla safari hizi ni za kifisadi na zenye nia ya kufanya witch hunting dhidi ya Membe. Ufisadi huu unastahili kukemewa na haya ndiyo matokeo ya kuwa na Spika dhaifu, chaguo la mafisadi.
   
 7. w

  watenda Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maskini Lowassa! Anahangaika bure kudhani kwamba kumchimba Membe kutampa yeye fursa ya urais. Hata kama angepata maovu ya membe, ambayo hata hivyo hatayapata, hiyo haimpi sifa yeye ya kuwa mgombea urais tumtakaye! Muda huu angeutumia kutubu na kuungama labda ingemsaidia. Alifanya hivyo Morocco akaumbuka na sasa anakwenda kutumbukia kwenye tope zito. Ama kweli sikio la kufa ........
   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh! haikubaliki hii inawezekana Tanzania tu waziri husika hajui chochote?? nadhani go ahead inatolewa na spika hivyo inaonesha dharau kubwa kwa walipa kodi wanaotaka bunge la bajeti liwaokoe kwa kujadili mambo yenye maslahi kwa umma na taifa sasa kuwaondoa wajumbe wa mkutano kunapunguza ufanisi wa bunge zima. watawala wamechoka tuwaondoe kwa namna yoyote ile.
   
 9. n

  ndutu Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mimi ninayemfahamu Lowassa hili halitanishangaza hata kidogo. Alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hii aliwapigia mabalozi wote akiwataka wawe wanamtumia matatizo yao kwake. Hii ilikuwa ni mbinu ya kuhamisha allegiance kutoka kwa waziri kuja kwake na ku-take control ya wizara kinyemela. Hajui hata etiquettes za diplomasia na anadhani alivyokuwa nawa-control ma-RD, Ma-DC na wakurugenzi wa halmashauri ndivyo hivyo angefanya kwa balozi zetu! Sasa ana kazi ya kujieleza iwapo ni sahihi kusafiri kwenda kwenye ziara hizi akiwa na mkewe kwa gharama za serikali. Leo hii bwana huyu ni Mwenyekiti tu wa kamati anafuja hivi, je akiwa mkuu wa nchi si ataamuru milango ya vyumba vya kuhifadhia fedha benki kuu iachwe wazi washirika wake wajichotee?
   
 10. m

  mudavadi Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii mission ni chimba chimba. Nasikia hata wajumbe wenyewe wametoka hapa wakiwa hawaelewani maana hakukuwa na muafaka kuhusiana na madhumuni ya safari. Nia hapa ni kuendeleza ufisadi ule ule wa ku-exhaust mafungu kabla muda haujayoyoma na mwaka mpya wa fedha kuanza. Hivi moral authority ya viongozi hawa kupiga vita ufisadi iko wapi?
   
 11. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  hii serikali ina kazi sana ..ila mwisho wa siku kitaeleweka tuu
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni moja ya harakati za kuelekea 2015:mod:
   
 13. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  unganisheni dots basi, mahela yagunduliwa swiss, membe anasema atawataja wahusika, kamati ya lowassa wanalikacha bunge wanaenda kukagua balozi zetu nje, membe analalamika kama kukagua mbona balozi zilizo ulaya na amerika tu, vipi balozi zetu zilizoko afrika azikaguliwi, rasmi naamini maneno ya utaki unaacha.dah
   
 14. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Membe aache kulalama siku zote huwa ni mnafiki hasemi ukweli. Ni mnafiki mno huwa ana jinsia mbili za maamuzi.
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Badala ya kwenda Uswisi wanakwenda sehemu nyingine ambazo hazina ishu, inaelekewa wanataka ku-counter attack kabla Membe hajawataja....:mod:
   
 16. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Lowassa haishi kumuwinda Membe ili achafuke kama yeye...
  Wanakwenda kukagua utekelezaji wa sera wakati wa bunge...mbaya zaidi hawakanyagi ubalozi wowote africa...kweli Membe kamshika pabaya lowassa

  Sent from my BlackBerry 9930 using JamiiForums
   
 17. n

  nndondo JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Watanzania ujuha wetu ndio mtaji wetu, hizi kamati zinaenda kuzurura wapi wakati madaktari wamegoma? hivi tunatanzania ngapi ? na sisi tunaona vibweka nakuleta ushabidi hapa badala y akutoa statements na kuingia barabarani, tunangoja chadema wafanye maana sisi hatuhusiki, I am so embarassed na ndio maana mara nyingi upumbavu wa baadhi ya mijinga humu ndani inanifanya niepuke hata kuingia humu, shenzi kabisa sisi humu tunajifanya babu kubwa wakti wengi hata mlo mmoja unatushinda, panapokuja kufanya maamuzi magumu bado tunaleta ushabiki, Lega and Human rights wamepigania kesi ya epa tukabaki tunawazomea, sasa hao rex wezi wakubwa wa nchi hii ndio wanabakia kupewa ubalozi marekani na kupewa uenyekiti wa bodi za mazao ambazo hata hawana idea,huyu kikwete jamani tunamchelewesha bure, hebu tutokeni barabarani kuokoa watoto wetu, watoto wake wameshapata pamoja ja kuwa na ubongo hafifu, sisi tunacheka na ---- tutaishia msikitini. Leo hii wanamuua Ulimboka eti tunasema lete ushahidi , pusy cats, kweli ndio maana mtaishia kulamba mavi yao
   
 18. B

  BMT JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  membe mnafiki sana hatufai na wala hana sifa ya kuwa rais wa nchi hii,kitendo cha kusema viongozi wa chadema walikwenda kwake wakiwa na njaa,kilinikera sana,binafsi simpendi membe ni mnafiki sana
   
 19. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Wote wawili Lowassa na Nyoka wa mdimu Membe wanahangaika bure ,Urais hamna kati yao atakayeupata!!
   
Loading...