Kamati kuu ya chadema iwe makini - ushauri wa bure. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati kuu ya chadema iwe makini - ushauri wa bure.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teh Teh Teh, May 25, 2011.

 1. T

  Teh Teh Teh Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salamu wana JF!Kamati Kuu ya Chadema inakaa kesho, pamoja na ajenda zingine muhimu ni kukaa kama kikao cha kwanza cha uchujaji wa majina ya wagombea wa BAVICHA - Taifa.Ushauri wangu kwa KAMATI KUU YA CHADEMA:-Mosi, kuzuia wabunge kushiriki kwenye ajenda ya Uchaguzi wa Bavicha ambao tayari wameonesha interest kwenye uchaguzi wa BAVICHA kwa kusaidia fedha baadhi ya wagombea. wabunge hao ni Zitto, Lema, Wenje. Pili, kutoa onyo kwa mjumbe yeyote wa Kamati Kuu - kujihusisha na kampeni za wazi, kwani Kamati Kuu ndo ni Kikao cha Uchujaji, na pia huthibitisha uteuzi wa mwisho wa Katibu, Naibu Katibu, Mweka hazina na Mratibu wa uhamasishaji. Pia ni wasimamizi wakuu wa Uchaguzi huo kupitia &quot;wazee wa chama&quot;. (rejea mwongozo wa John John Mnyika).Tatu, Wajumbe wa secretariat ya Kamati Kuu wenye interest wawekwe mbali katika uchaguzi huu. Ni vizuri wazee wa Chama kama takwa la Katiba wasimamie uchaguzi huu. na Katibu Mkuu awe ni returning officer. wajumbe wa secretariat ya Kamati Kuu safi wawe ni wasaidizi wa Katibu Mkuu ambao ni John Mnyika, Benson Kigaila, John Mrema, Ally Chitanda. (ila Mnyika asiwepo kwani ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAVICHA). Nne, Kamati Kuu ya Chama ifanye udiriki wa kuengua baadhi ya wagombea ambao wameonekana kuvunja kanuni, taratibu, kampeni za wazi, isipowang'oa baadhi ya wagombea ambao wamefanya kampeni na kila mtu anajua, ni wazi kuwa CC ya Chadema itakuwa inakula matapishi ya CCM, na wao watatakiwa kujivua gamba! Tano, Ni vyema Katibu Mkuu - Dr. Slaa akawaita maafisa wa TAKUKURU (licha ya kutowaamini) wakawepo kuanzia siku ya Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi ambapo wajumbe wataanza kuwasili na kufanya uchaguzi huo uwanja wa Sabasaba. (rejea wajumbe wa BAVICHA kumtuhumu Zitto Kabwe kutoa rushwa wakati akimsaidia David Zacharia Kafulila wakati akigombea Uenyekiti wa BAVICHA - Taifa; hakuna hatua zozote za kichama wala kiserikali zilizochukuliwa). Tutawapa taarifa na ushirikiano wa vitendo vya rushwa vilivyoandaliwa. Sita, Kamati Kuu iandae vigezo on merit basis za kuwapata Katibu, Naibu Katibu, Mweka hazina na Mratibu wa uhamasishaji. ni wazi kuwa kila Mwenyekiti na Makamu na wajumbe wa kamati ya utendaji wa majina yao. kwa kuwa hawa ni watendaji wa secretariat ya BAVICHA Taifa, ni vyema wasitokane &quot;kisiasa na makundi ya kisiasa&quot; bali watokane na uwezo, ujuzi na uzoefu wao ndani ya Chama - waweze kufahamika ndani ya CHAMA. Saba, kutokana na kurejea uchaguzi uliovurugika, ni vyema Jeshi la Polisi wakawepo katika uchaguzi huo! Ipo Tension kubwa sana miongoni mwa wagombea wa Uenyekiti. Nane, Miundo mbinu zote kama karatasi za kura, sanduku ziwe wazi, kanuni, taratibu zifuatwe, Miongozo ya Baraza na Katiba zifutawe na kutamalaki kwenye uchaguzi huo. Tisa, Kamati Kuu iwazuie wajumbe vijana ambao ni Zitto, Lema, Wenje kutoshiriki katika uchaguzi huo wala kuonekana katika ukumbi au/na mazingira ya ukumbi unless otheriwise kutakuwa kuna vurugu kubwa sana - kwani Wenje ana muunga mkono Nyakarungu. Lema kwa Heche, Zitto kwa Mchange. Kumi, kijiografia na kimkakati - ukumbi wa sabasaba utawapa shida, una mianya mingi ya kufanyika kwa uhuni kama ambavyo ilivyokuwa katika uchaguzi wa kuwania Ubunge wa Viti Maalum. ni vyema ukumbi wa Mbezi - (ulipofanyika Baraza Kuu) ukafanyiwa uchaguzi wa BAVICHA. ANGALIZO: Tayari makosa mmeanza kuyafanya - uwepo wa John Mnyika kama mratibishi wa Kamati ya Vijana ya kuandaa uchaguzi kwa kiwango fulani, akishirikiana na Katibu Mkuu, na Wazee wa Chama - John Mnyika ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAVICHA - tayari kuna usemi na uvumi kuwa anamuunga mkono Saanane (ingawa siamini); ni vyema John mnyika akajitoa kwenye usimamizi wowote ule ambao anaweza akapangiwa na Katibu Mkuu (returning Officer); otherwise inaweza dhambi na uovu wowote unaweza ukamrudia (Back fire).Nimepitia majina ya wagombea wote. Kamati mnaweza mkafanya re-location with consultation na wagombea husika. Mfano: sioni kama kuna mgombea anaye-fit kwenye Ukatibu kwa maana ya uzoefu wao (note that this is going to estabilished, it needs strong, experienced, talented, education capacity), badala yake kuna mgombea wa Unaibu ambaye anafit sana kuwa Katibu na wa Ukatibu anafit kuwa Naibu. (This is ver serious to consider as a CC)Asanteni! Najua mmeelekeza mawazo yenu Tarime! Elekezeni mawazo yenu pia katika CC ya kesho hususani uchaguzi wa BAVICHA - Msifikiri BAVICHA itakuwa kama BAWACHA.Asalaaam.</p>
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Well said mkuu Kazi kwenu viongozi wa CDM.
   
 3. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuna taka chadema imara siyo ya kubebana
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,858
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Jaribu kui edit habari yako ili isomeke vizuri.

  Mosi, vitu ambavyo umeongelea haviwezi kutekelezeka(leo) kwa vile vinawekwa na kanuni labda ushauri kanuni zibadilishwe kwa chaguzi zijazo lakini siyo huu, mfano umependekeza returning officer Mnyika kubadilishwa leo wakati mchakato uko hatua za mwisho kifupi haiwezekani.

  Pili, umewa pin point wabunge vijana kina Zitto, Wenje na Lema wasijihusishe na uchaguzi sijui ni vigezo gani ulivyotumia hadi kufikia conclusion yako kuwa wanawasaidia uliowataja, unavielelezo kuwa uliwaona wakipeana mathalani pesa na ukathibitisha hizo pesa ni kwa ajili ya kampeni?

  Tatu, Kuihusisha takukuru chombo ambacho kina walakini katika utendaji wake ni kukaribisha matatizo zaidi kwenye chama na uchaguzi, endapo takukuru watasema kwa makusudi yao kuwa uchaguzi haukuwa huru ili mradi kukivuruga chama utakataa ushauri angali uliwakaribisha? Polisi kuwepo ni sawa maana kwenye kusanyiko lolote hata mikutano ya CDM huwa wanakuwepo lakini wasihusishwe kwa namna yeyote na uchaguzi.

  Nne, Umesema kamati iwazuie Zitto, Wenje, Lema kufika kwenye ukumbi wa Sabasaba ambao hata hivyo unapendekeza ubadilishwe nasema tena huna vigezo labda ni kwa utashi wako tu kusema kuwa uwepo wao utasababisha vurugu kubwa hiyo intelijensia umeitoa wapi au tuseme wewe umepanga hiyo vurugu.

  Mimi nafikiri tuiamini na kui support kamati iliyoteuliwa na chama kusimamia uchaguzi huu badala ya kuanza ku predict vitu hewa ambavyo havina msingi wowote na inawezekana havipo ni vya kufikirika.
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Teh teh,
  Naona umeshindwa kufanya utafiti,unasikiliza hearsa.Najua hofu inasumbua.Kuunga mkono mgombea si uhaini na si dhambi.Umehusisha majina ya watu bila tafiti.Kama kuna mtu anayeniunga mkono anaunga mkono ajenda na hili si kosa.Hilo suala la Mnyika kuniunga mkono sijui umelipata wapi.Naona hata wewe unachangia katika kuvuruga uchaguzi huu

  Last time ulikuja na ajenda za kutaka sisi baadhi ya wagombea kuondolewa.Leo umekuja na uzushi mwingine,tunakufahamu.Usidhani kwamba hufahamiki,na siku zote siasa zako zimekuwa za aina hii.Mbona hujapeleka barua rasmi?Acha upotoshaji
   
 6. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  By the way we must have some degree of trust to the cc member but i don't accept the presence of PCCB because they are sons and daughter of magamba party hence they will use that opportunity to penetrate magamba propaganda and destroy the whole election !!!
  GOD BLESS CHADEMA AND CONTINUE TO BLESS ME!!
   
Loading...