Kamati`imeroga`Taifa Stars

Kamati`imeroga`Taifa Stars

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,108
Reaction score
34,934
Kamati ya Operesheni Ushindi ya timu ya taifa ya soka ilitoa "hamasa" ya sh. milioni 30 kwa Taifa Stars katikati ya wiki, kwa ajili ya mechi ya Juni 8 ya michuano ya awali ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo jijini Dar Es Salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo Mohammed Dewji amekaririwa akisema ni kichocheo cha ushindi kwa ajili ya mchezo huo, na tunafahamu Nipashe hata bila kuambiwa wachezaji wanafahamu fika kuwa ili kubakiza hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za Brazili 2014, ni lazima Taifa Stars ishinde.

Mbali na kutoa fedha hizo, taslimu zikiwa kwenye boksi, Dewji ambaye amewahi kuongoza kamati hiyo siku za nyuma na kuwa mfadhili ama mdhamini wa timu za Simba, Singida United na African Lyon kwa nyakati tofauti pia aliahidi zawadi KUBWA zaidi kama Stars itashinda Morocco.

Lakini kutoa fedha na kuahidi zawadi kubwa zaidi ni kitendo ambacho kinaashiria kuwa wachezaji wa Taifa Stars ni watu wasiojua wajibu wao na kwamba bila harufu ya 'rupia' hawawezi kuwa na uzalendo kwa nchi yao, Nipashe tunaona,.

Na hapo ndipo nia yoyote njema ya kamati inapokuwa athari kwa timu ya taifa.
Tuliwahi kueleza athari za jumla za kuunda kamati ya ushindi kama hii ya Dewji wakati serikali ilipotamka nia yake hiyo mapema mwaka huu; tukizungumzia uwezekano mkubwa wa kuvuruga mwenendo mzuri wa Taifa Stars katika Kundi C lake.

Kwa vyovyote, Taifa Stars ilishavuka malengo ya kufanya vizuri katika michuano hii kabla hata serikali haijakurupuka kuunda kamati, na tulisema tungeweza kuielewa Wizara ya Michezo angalau kidogo kama TU ingetoa wazo lake hilo katikati ya mwaka jana wakati kinyang'anyiro kikianza.

Kuwa na pointi sita kati ya tisa katikati ya safari; katika kundi lenye timu za Ivory Coast, Morocco na Gambia ni mafanikio ambayo ni Watanzania wachache wangeweza kuyaota wakati ratiba ya michuano hiyo ikipangwa miaka miwili iliyopita.

Lakini kuwa nyuma ya viongozi wa kundi Ivory Coast, ambayo ni ya 12 duniani katika viwango vya FIFA, shirikisho la soka la kimataifa, kwa tofauti ya pointi moja hadi kufika nusu safari ni mafaikio ambayo, hakika, hakuna Mtanzania ambaye alitaraji.

Hakuna Mtanzania ambaye alitaraji pia unapoangalia historia ya ushiriki wa Taifa Stars katika michuano ya awali hii iliyopita na ukweli kuwa Morocco ambayo ipo nyuma yetu kwa tofauti ya pointi nne ni ya 18 kwa ubora Afrika.

Kuna mazingira fulani kambini na ari kwenye kikosi ambavyo vimeleta mafanikio haya, tunafahamu Nipashe na ndiyo maana endapo ushindi katika mchezo wa Juni 8 utaenda sambamba na Ivory Coast kushindwa kuvuna pointi zote kwa Gambia, timu yetu ambayo ni ya 116 duniani kwa mujibu wa viwango hivyo vya FIFA vya mwezi huu itakaa kileleni mwa Kundi C, kimaajabu.

Hata hivyo, tunaona Nipashe, mwenendo mzuri huu wa Taifa Stars unaelekea kutibuliwa na kamati ya Dewji kwenye michuano hii ambayo hatujawahi kuvuka kigingi cha kwanza cha michuano ya awali tangu nchi ianze kuwa mwanachama wa FIFA mwaka 1964.

Kama ambavyo tumeshasema awali, kuna mazingira ya ndani na nje ya uwanja ambayo yaliiwezesha Taifa Stars kushinda mara mbili na kufungwa kwa taabu na Ivory Coast ugenini, na tunafahamu Nipashe kuwa kwa vyovyote kamati si moja ya mazingira mazuri hayo.

Tunafahamu kamati si moja ya vichocheo vya ushindi huo kwa sababu imeanzishwa ikionekana kuelekea kudandia mafanikio ambayo yameletwa na benchi makini la ufundi na moyo wa uzalendo ambao kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, upo kwenye kizazi cha sasa cha wachezaji wa Taifa Stars.

Ndiyo maana, tunaona Nipashe, zawadi na ahadi zozote za fedha nyingi zaidi ni kuwavuruga akili wachezaji hawa kana kwamba si Watanzania wenye kufahamu ukubwa wa jukumu lililo mbele yao bila fedha, wasiojua maana ya kutimiza kwa makini maelekezo ya mwalimu Kim Poulsen na pia wasio na moyo wa kutetea rangi za bluu, kijani, nyeusi na njano zilizo katika bendera ya nchi bila fedha kuwekwa mbele yao.

Sasa, tunaona Nipashe, Taifa Stars haitacheza tena dhidi ya Morocco katika mazingira yaleyale ya utulivu na uzalendo kama ilivyokuwa kabla ya kamati, kupewa na kuahidiwa fedha zaidi.
Si vibaya kutunza, hasa kama mwanamichezo atafanya vizuri na baada ya jukumu lililomkabili kutimia -- Septemba.


CHANZO: NIPASHE
 
Mimi mbna naona sio vibaya kumpa mwanao hamasa ya zawadi siku ya kwenda kufanya mtihani?-inatia hamasa na tunaona hata nchi nyingi tu duniani wanafanya hivo mkuu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
tunaye samata na ulimwengu, ya nini kuhofia? kazi ngumu ni kufunga mikia miwili ya simba wenye njaa iungane, lakini kumfunga mmoroco, mgabia ma m ivori, ni raisi sana kam ailivyo bata katika maji!
 
Wachezaj watakua wanacheza wanawaza pesa tu sio heshima ya taifa.!!
 
Back
Top Bottom