Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,273
- 21,455
Kwa mara ya kwanza tunashuhudia watu wengi wakiingia katika wigo wa vyombo vya sheria kwa makosa mengine hata hayana msingi. Achilia mbali kina Lowasa eti kwa kuwa alisimamishwa na wananchi ili asalimiwe. Mara ngapi tumeona hili likifanyika kwa raisi na hata mawaziri bila kusikia wamekamatwa na polisi kwa kusalimia wananchi waliosimamisha msafara wao?
Kisha tunaona wabunge kukamatwa na kufikisha polisi hadi mahakamani kuwa cha kawaida sana siku hizi. Kila siku tunasikia hili. Si tu kina Lema na Lijuakali, kuna wabunge wengi sana, hasa upinzani, imekuwa jambo dogo sana sasa kukamatwa na polisi kwa makosa mengine yasiyo na pua wala mdomo ambayo mara nyingi wanashinda hizo kesi. Bila aibu serikali imeamua kushusha hadhi na staha ya ubunge na hata polisi sasa wamefikia hatua wanawadharau na kuwaona wabunge si kitu tofauti na miaka ya nyuma. Utaamuaje wabunge waitwe waheshimiwa halafu unawakamata ovyo ovyo kama vibaka wa Kariakoo, kama watu wasiostahili heshima? Yaani katika serikali yetu imefikia ukitaka kulala rumande kirahisi basi uwe mbunge. Aibu sana kwa serikali. Aibu sana hata kwa Bunge lenyewe. Inafikia makosa ya faini mheshimiwa mbunge anafungwa gerezani kama vile kazi yake ya msingi ni uhalifu? Kusema wanavunja sheria ni kisingizio tu; ukweli ni kwamba sheria kwa sasa zinatumika kukomoa watu.
Halafu unakuja kwa wananchi wa kawaida, waandishi wa habari kutia ndani kina Max Melo na wengine tunasikia sijui wamemtukana raisi, hawajatoa majina sijui nk, mambo ambayo kwa kweli hayana pua wala mdomo.
Serikali kwa sasa inajiendesha kama askari trafiki; akisimamisha gari yako, hata kama ni mpya ya leo, na akaamua lazima akukute na kosa atalipata tu! Tumefikia mahali serikali yetu inakamata watu kwanza halafu inaanza kutafuta makosa ya kukushitakia - ndio maana utasikia ooh, Geita tulimkamata Lowasa kwa usalama wake. Uongo mtupu, polisi wanakamata watu wanaostahili kuheshimiwa bila kujua kwa nini wanawakamata!
Sasa basi, kwa mtu yeyote mwenye akili ataona serikali yetu imefikia hatua ambayo haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii. Kuna kila dalili kwamba serikali yetu ina walakini mkubwa, na sio watu au wanasiasa wake. Serikali ambayo inatafuta vikosa vidogovidogo ili kuwakamata na kuwafunga wananchi au wanasiasa wake, hiyo ina walakini mkubwa, na hizo ni dalili kwamba huko tunakoenda sio kuzuri. Na ukweli ni kwamba hizo ni dalili za serikali yetu inaelekea kwenye kitu kinachotwa kwa kiingereza "authoritarianism, tyranny, Stalinism, autocracy au hata dictatorship". Huenda hata tumeshafikia huko.
Lazima ifikie wakati ambapo tukiri bila aibu, kwamba hizi kamata kamata na fungafunga ni dalili kwamba wenye tatizo sio wananchi au wanasiasa, tatizo litakuwa kwenye serikali na staili yake ya uongozi. Kwa nini tuwe na uongozi ambao siku zote una ugomvi na wanasiasa au wananchi wake? Uongozi ndio wenye tatizo basi.