Kamanda Sirro: Kutishia silaha si uhalifu, ni ushamba

Kamanda Sirro: Kutishia silaha si uhalifu, ni ushamba

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro (kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari leo), watu wanaowatishia watu bastola ni WASHAMBA.

Amenukuliwa akisema "watu wanaofanya hivyo ni washamba na hawajui taratibu za matumizi ya silaha, kwa sababu silaha hutumika pale ambapo nguvu za kawaida zimeshindikana".

Ukiisoma katikati ya mistari kauli hiyo ya Kamanda Sirro na kuyachambua matumizi ya maneno hayo, kuna ujumbe mkubwa sana unaweza kuupata.

Kwa hiyo tunaambiwa, tena na Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, kuwa kutishia bastola si tena kosa la jinai bali ni USHAMBA.

Na kwa sababu huo ni ushamba wala si uhalifu na wanaofanya ni washamba wala si wahalifu, maana yake tusitarajie hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya uhalifu na wahalifu.

Kauli hii inatupatia ujumbe mzito kuhusu kigugumizi walichonacho polisi katika kushughulikia matukio ya hivi karibuni ambayo yamehusisha utoaji wa silaha hadharani na kutishia watu.

Maana yake, kwa kauli ya Sirro, ni kwamba yule aliyemtolea na kumtishia bastola Nape Nnauye wakati akizuiwa kuzungumza na waandishi wa habari ni MSHAMBA aliyefanya kitendo cha KISHAMBA, sasa tangu lini Jeshi la Polisi likashughulikia masuala ya USHAMBA wa mtu au watu!

Kwa kauli hiyo ya Kamishna Sirro, mmoja wa wavamizi wa press conference ya viongozi wa CUF hivi majuzi ambaye anatuhumiwa kutoa na kuwatishia bastola viongozi wale na waandishi wa habari na kusababisha taharuki kubwa na kuumiza watu, ni mtu MSHAMBA aliyefanya tendo la KISHAMBA.

Kutoa na kutishia watu kwa bastola ni USHAMBA. Alas!

Kauli hiyo ukiichambua sana unaweza kujikuta unafanya rejea ya zile kauli zinazotumika sana huko 'site' kuwasema baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu wa vyombo vya dola ambao wakikaa mahali (baa) na wakata kutambulika kuwa wapo na wao ni akina nani, hujigamba kwa kutoa vitambulisho au kuonesha bastola. Watu 'baki' au raia wa kawaida huishia kusema USHAMBA huo.

Huishia kuwaita washamba kwa sababu hawana uwezo wa kufanya jambo jingine dhidi ya 'maofisa' hao.

Wallah, Hoi polloi tuna kazi kubwa awamu hii. Tutasikia na kuona mengi. Tunasubiri kuona polisi wa Kamishna Sirro wakishughulika na watu WASHAMBA wanofanya mambo ya KISHAMBA ya kutishia watu bastola (tena wasiokuwa wahalifu) mchana kweupe.

Na kama matukio ya namna hiyo yameanza kutafutiwa na kupewa jina la USHAMBA, fikiria mwenyewe tuko katika hali gani na nini kitatokea au kitaendelea kutokea.
Aisee kumbe kweli kichaa hajipeleki hospitali mwenyewe mpaka apelekkwe na wasamaria wema.sasa basi ukinitishia na bastola nitakuona mshamba alafu utajukuta wodini dakitari akikchukua maelezo ya awali.sitaki ujinga eti....
 
Kwahiyo Siro ndio anayetamka sheria, maana unatuambia kwakuwa amesema ni ushamba basi sio jinai? Kwa mapovu yako ni kwamba kuanzia jana basi ile sheria inayosimamia silaha za moto imefutwa na kamanda Siro? Akili za nyumbu wanazijua wenyewe na USHAMBA WAO.
mleta mada anataka kuonesha double standard ilivyoshamiri awamu hii ya tano; watu wa usalama, polisi na kundi la Lipumba wakitishia bastola ni ushamba. Lakini RAIA wasio kwenye system wakitishia bastola ni kosa la jinai.Na Kamanda Siro anataka Ku justify position yake ya kushindwa kuchukua hatua za kisheria.
 
Chadema bana,Sijaona sehemu amabayo Sirro amesema kutishia silaha si uhalifu.Acheni kufinyanga maneno jamani
Kama Siro amesema kutishia silaha ni ushamba,haimani kwamba amesema kutishia silaha si uhalifu
Mwanahabari Huru ukanjanja wako fanyia kwa Mbowe
 
Kwahiyo Siro ndio anayetamka sheria, maana unatuambia kwakuwa amesema ni ushamba basi sio jinai? Kwa mapovu yako ni kwamba kuanzia jana basi ile sheria inayosimamia silaha za moto imefutwa na kamanda Siro? Akili za nyumbu wanazijua wenyewe na USHAMBA WAO.
Umemuelewa lakini?au unavyeti feki zaidi ya Bashite?
 
Ushamba tu aaah naona wengine kibao wanatembea na sime rungu Ushamba tu Tz ya washamba
 
HATA Mi nakubari ni ushamba kumtishia mtu silaha ,,dawa ilitakiwa ampe mtu shaba ya kichwa ndio tungemuona mjanja,,,, viva kamanda sirro
Kama ni kweli wanaonyesha silaha zao kwa ushamba walionao, itafika mahali watazifyatua kuua watu ili waendelee kusifiwa
 
Watu wanaotishia wengine silaha ni kwa sababu hawajui matumizi yake sahihi, swali! nani anatoa kibali cha kuwapa washamba hao silaha huku wakiwa hawajui matumizi yake sahihi? Kama sirro amesema hayo basi akapimwe akili.
 
Naomba Sirro ajitafakal upya kwa statements zake huo ni uvunjifu wa sheria mkubwa hakuna tofaut na majambazi maana wanatumia siraha kinyume na taratibu then unasemq ni ushamba? Swali, hzo siraha wanazimiliki kiharali? Nani kawapa idhin ya kuztumia kinyume na utaratibu?
 
Chadema bana,Sijaona sehemu amabayo Sirro amesema kutishia silaha si uhalifu.Acheni kufinyanga maneno jamani
Kama Siro amesema kutishia silaha ni ushamba,haimani kwamba amesema kutishia silaha si uhalifu
Mwanahabari Huru ukanjanja wako fanyia kwa Mbowe
Ukishirikisha Ubongo kabla ya kutanua mdomo ungenielewa siyo kosa lako unashikirisha makalio sana
 
Back
Top Bottom