Kamanda Sirro kajibu ombi la Diamond kuhusu biashara ya chips na bodaboda usiku

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Baada ya mwimbaji Diamond Platnumz leo
march 14 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 ya
Clouds TV kuomba serikali iwasaidie vijana wa
vibanda vya chipsi pamoja na bodaboda kuhusu
ishu ya muda wa kufanya kazi kuanzia saa sita
usiku ambapo alisema muda wa usiku chakula
hakipatikani na askari wamekuwa wakimwaga
vyakula vyao, kamanda kanda maalum Dar es
salaam simon Sirro kajibu kuhusu hilo……
diamond-1.png

>>>“K imsingi askari wetu wanapita kwa ajili ya
usalama na kama amevunja sheria kwa
kupitiliza muda hapo ni kuchukua chips zake na
yeye mwenyewe, lakini kwenye night clubs wana
leseni zao na wanamasharti yao na habari
nilizopata wanaweza kuendelea mpaka saa 11
kwa hiyo supu, chips zinapatikana kule ndani”

Source: Millard ayo
 
Viongozi wa Tanzania wengi wanakurupuka tu wengine huwa tunatoka safarini usiku wa manane so tutakuwa tunakula wapi??
 
Mm ninayesafiri nafika Dar SAA sita au saba na sina ndugu...kwahiyo nilale njaa?..sisi wengine tumezoea tunakula Chipsi tunapanda bodaboda tunaenda gesti kulala....sasa wanatubania riziki au ndio tuwe tunakuja Dar majira ya mchana. Wangewaacha vijana wafanye biashara, huku mikoani ndio wasimamie hizo sheria
 
Kijana aliyehaso mpaka kufikia kileleni.. Na bado hasahau alikotoka..

Anajitahidi kuwa sauti ya vijana wengine wanyonge walio chini..

Bravo chibu!!


Cc: Nifah
Mond anapgania vijana wenzake utadhani ndo yeye anataka atoke kimaisha.
Ni mfano wa kuigwa na vijana wote
 
"Mliipenda wenyewe..!"

Na bado; Sifurahii, liwe funzo kuelekea 2020.

Baada ya kuchakazwa kwa miaka 3, najua 2019 boda boda, wamachinga nk, mtafuatwa tena na kubembelezwa ... Asomaye na Afahamu..!
 
Back
Top Bottom