Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema waliotajwa kuripoti kituoni kama hawataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya hudhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.
Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Pia Sirro amesema Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima na Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji walilala polisi kwa kuwa bado upelelezi dhidi yao unaendelea.
"Operesheni ya dawa za kulevya bado inaendelea na kuanzia sasa hatutaruhusu mkusanyiko wa wananchi karibu na kituo cha polisi hiki watakaoonekana watashughulikiwa Kamishna Sirro kwa kuwa tayari nimeshatoa taarifa."
Chanzo: Mwananchi