Bonny
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 13,370
- 29,961
- Kioo cha mbele mwa gari pekee ndio tumekataza kuweka hizo FULL TINTED, hii itasaidia sisi tukisimamisha gari kumuona aliyeko ndani kirahisi na pia kuepusha ajali za Madereva kutoona vizuri.
- Pamoja na kukataza Tinted kwenye kioo cha mbele kwenye magari, Tinted ndogo inayopita kama mstari juu kwenye kioo cha mbele ili kuzuia Jua,HAIJAKATAZWA.
- Mpaka sasa Polisi haijakataza wala kutoa tamko lolote la kuzuia Tinted kwenye vioo vya pembeni mwa gari hivyo ukisimamishwa hilo sio kosa.
- Ni marufuku kuweka Tinted ya mstari chini kwenye kioo cha mbele na kubakisha sehemu tu ya katikati, ni mtindo ambao Mabasi mengi ya abiria yamekua yakiufanya na kuitumia sehemu hiyo ya chini kunadi safari zao.
- Hatujakataza Tinted kwenye vioo vingine vya pembeni mwa gari labda kama maelekezo yatakuja baadae…….