Najua uletaji wa tochi mpya ni kujaribu kupunguza ajali za barabarani kwa maderewa kutii amri za barabarani. Lakini kujihusisha tuu kwa polisi kukaa mabarabarani nchi nzima kila mahali kumdhibiti dereva anayekiuka amri naona haina tija. Barabara zetu zimefuatwa na wananchi kupenda kukaa karibu na barabara, kufanya biashara barabarani, hata kama barabara itapitishwa nje ya mji , wananchi wataifuata kama pale manyoni. na hivyo kila pahara penye makazi ya watu kuna udhibiti wa 50km/hr. SWALI, msafiri anatoka Dar kwenda Mwanza na kila baada ya km chache kuna 50km/hr atafika baada ya saa ngapi? Licha ya 50km/hr kuna matuta na polisi pia. Mfanya biashara ili apate faida ni muhimu kwenda haraka na kurudi haraka. Ningependa kuona madereva wote wafunzwe maadili zaidi ya kutii kwa mkandamizo wa polisi. Matuta yote yatolewe. Leseni zitolewe kwa madereva waliofuzu na timamu tu. Dereva huru na mzuri ni kama mfanyakazi yoyote hahitaji na kama atahitaji ni uangalizi kidogo - minimum supervision. Ikitokea ajali bahati mbaya ndipo polisi aende kupima.