Kamanda Kova: Ningekuwa IGP ningehakikisha askari polisi na raia wanakuwa kitu kimoja kama timu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,944
141,920
Kamanda mstaafu wa polisi kanda maalumu ya Dsm mzee Suleiman Kova ameelezea mafanikio aliyoyapata alipokuwa katika utumishi.

Kamanda Kova amesema yeye alikuwa akipelekwa maeneo yaliyoshindikana kwa uhalifu na alipofika alifanikiwa kuleta amani na Upendo.

Ametolea mfano mkoa wa Kigoma ambao ulikithiri kwa ujambazi wa kutumia silaha lakini alipofika alifanikiwa kukamata silaha zote, pili Mbeya kulikokithiri imani za kishirikina za uchunaji ngozi na upigaji nondo vichwani lakini alipowasili alilimaliza tatizo hilo.

Akijibu swali la mtangazaji Hasan Ngoma aliyetaka kujua endapo Rais Magufuli angemteua kuwa IGP angefanya mambo gani mahususi ya kuacha alama, Kova amesema angehakikisha askari polisi na raia wanakuwa kitu kimoja as a team wakiishi kwa kusaidiana na kupendana.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!
 
Akijibu swali la mtangazaji Hasan Ngoma aliyetaka kujua endapo Rais Magufuli angemteua kuwa IGP angefanya mambo gani mahususi ya kuacha alama, Kova amesema angehakikisha askari polisi na raia wanakuwa kitu kimoja as a team wakiishi kwa kusaidiana na kupendana.

Kwa maneno mengine anakiri kwamba IGP wa sasa anaboronga. Tumemsikia na tulishaliona hilo.
 
Kova huenda ana kisukari...

hii ninge...ninge...ningekuwa ni maneno ya MTU ambaye huenda utimamu wa akili unaelekea kupata matatizo...au dalili za kujutia kitu... anyway ni mawazo ya mtu mzee aliyepoteza mvuto ktk jamii

Ameshindwa kuwaunganisha ngazi ya mkoa.. Taifa ndio ninge ninge ninge...ninge....ninge....

Akacheki Afya ya ubongo kwanza...
 
Usimlishe maneno hayo ni mawazo yako!
Watu kama nyie mnaishi kama roboti. Hamtaki kufikiri zaidi ya mnachosikia.

Wakati fulani huko nyuma Yesu alisema usipokula nyama na damu yangu hutauona ufalme wa mbinguni. Wengi waliposikia maneno haya wakamkimbia. Watu wale ni kama wewe.Watu wasio na uwezo wa kuelewa zaidi ya walichosikia.
 
Bado yanabaki kuwa ni mawazo yako na si ya mstaafu Kova!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom