Kamanda kova na mawazo ya hovyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda kova na mawazo ya hovyo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kajunju, May 27, 2012.

 1. k

  kajunju JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Tangu kamanda kova atoe tamko kuwa maandamano ya mkutano wa chadema uliofanyika jana hayaruhusiwi. Nimeanza kujiuliza ana weredi gani na kazi yake? Licha ya watu kwenda kwa wing kama wanaoandamana,kama watu walivyoonekana wanatoka mkutanoni kwa maandamano.sijasikia kova akitoa tamko licha ya wananch kuandamana huku wakisukuma magari ya viongozi wa cdm hadi makao makuu ya chama. Ni wakati muafaka sasa kwa makamanda hasa hawa wazee kuangalia/kujifunza mood,mawazo ya watu kuliko kukurupuka na taarifa zisizo na kichwa wala mguu. Sehemu zote kunakotokea fujo polisi ndio wanaoanzisha fujo. Kigoma yaliwai kutokea mauaji ya rasta mmoja wa kijiji cha mnyegera aliyeuawa na polisi. Baada ya polisi kupata taarifa kuwa wananchi wanakwenda hosptali kuiona maiti. Polisi waliweka road block km 6 toka mjini kasulu. Kwakuwa wananchi walishapanga kufika hospital wanakijiji wote na ffu toka kgma walipanga kuwazuia,wananch waliamua wavunje kundi lao kubwa ili waende watatu watatu. Ffu walipitwa na mibunduki yao na mabom ya machozi.ndani ya masaa 2 Kijiji cha mnyegera kilikuwa kimetua hosptal. Polisi walioweka kizuizi waliona aibu. Mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa wote walifika kuskia kilio cha wananchi.shinikizo ili la wananchi limepelekea askari zaid ya 5 kuwa matatani had sasa. Mfano huu ni sawa yaliyomkuta kova jana. Akili za kuambiwa/kuamlishwa achanganye na zake.
   
Loading...