Kamanda James Kombe apata mrithi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda James Kombe apata mrithi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Halisi, Mar 9, 2010.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  http://www.dar411.com/2009/images/uploads/img240x250

  IGP MWEMA ATEUA KAMANDA MPYA
  KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI
  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

  DAR ES SALAAM JUMANNE MACHI 09, 2010. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amefanya ya mabadiliko ya Uongozi kwenye Jeshi hilo yakihusisha Kikosi cha Usalama Barabarani na maafisa wa vitengo mbalimbali kikiwemo Kitengo cha Habari cha Jeshi la Polisi.

  Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema leo kuwa katika mabadiliko hayo Mkuu wa Jeshi la Polisi amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohammed Mpinga, kuwa kamanda Mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini badala ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi James Kombe, ambaye anastaafu kwa mujibu wa Sheria.

  Kamanda Mssika amesema kuwa nafasi ya Kamanda Mpinga, inachukuliwa na Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Pwani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Johansen Kahatano. Kabla ya Uteuzi huo, Kamanda Mpinga alikua ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini.

  Katika mabadiliko hayo Mkuu wa Jeshi la Polisi amemteua Mrakibu Msaidizi wa Polisi Advera Senso, kuwa Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi badala ya Mrakibu Suzan Kaganda, ambaye amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa msaidizi wa kitengo cha masuala ya Operesheni.

  Wengine waliohamishwa ni Afisa Mnadhimu mkoa wa Tanga ACP Simon Mgawe, kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Kigoma SSP Salehe Mbaga, kwenda kuwa Mkuu mpya wa Usalama barabarani mkoa wa Pwani.

  Kamanda Mssika amesema kuwa, Mkuu wa Upelelezi wa Kikosi cha Reli Mrakibu wa Polisi Adolphina Kapufi, sasa anakuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa wa Tanga ambapo nafasi yake inachukuliwa na SP Sebastian Mbutta, kutoka Upelelezi Singida.

  Amesema SP Robert Masanja, ambaye ni Mkufunzi Chuo cha Polisi CCP Moshi sasa anakuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na ASP marco Joshua ambaye sasa anahamishiwa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma.

  Kamanda Mssika amewataja maafisa wengine waliohamishwa kuwa ni ASP Anthony Masonzu, kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Jijini Dar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ambapo Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Kigoma Mrakibu Msaidizi wa Polisi William Mkonda yeye ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kigoma.

  Kamanda Mssika amesema kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga zaidi katika kuboresho ufanisi katika kutoa huduma za Polisi kwa Jamii.
   

  Attached Files:

 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160

  hapa Kamanda mwema amecheza, asante ,
  kama alikua kwenye akili yangu , kuwa matatizo ya usafiri na usafirishaji DSM CHANZO NI HUYU, hakuwa nauwezo , alikua mtafuta sifa, mara nyingi nilikua namuona pale mataa ya salenda , akiongoza magari, kwangu hakuwa kiongozi makini na mahiri.​
   
 3. N

  Nanu JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tunategemea pia tuone mabadiliko ya ma-RPC wa Arusha, Manyara, na Dar es Salaam katika kuongeza ufanisi. (Manyara-polisi wananyanyasa wananchi huko Hanang, Arusha-ujambazi umeshika kasi inaonekana kama vile polisi wamezidiwa, Dar es Salaam-ujambazi umeibuka upya licha ya Kova kuwepo kwenye TV mara kwa mara kuonyesha anafanya kazi hali bado kuna watu wanapoteza maisha kutwa kwa ujambazi)
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Ni vema,labda mabadiliko yatakuwepo!
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  sasa zawadi nyingine kwangu ni kumuondoa huyu jamaa , mkuu wa polisi kanda maalumu ya DSM.
   
 6. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Umsimsfie IGP, umemabiwa jamaa anastaafu kwa mujibu wa sheria tu na wala sio anabadilishwa. Halafu kuongoza magari si ndo alikuwa mchapa kazi au?
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kweli kabisa sioni sababu kwann kamanda Sele anaendelea kubaki dar hapa...tunataka mtu mchapakazi hapa anaweza kuwepeleka puta Majambazi haswa sio kusumbuana na vijambazi vidogo na kesi zakupandikiza za JMuro
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu mtu afanyapo vyema hupongezwa.......HATA HILI TWASHINDWA KUPONGEZA...?Tutabaki laumu tu mpaka lini?Mbona wakati wa yule aliyepita ulikuwa ukisikia "matusi" kwenye radio zao..huku wao wenyewe wakimwaga sifa kwa TIBA...? utawasikia wakitoa lawama na manung'uniko yao kwenye redio wakimtoa kamanda TIBA....!Na juu ya hili Mkulu wa geshi hili apongezwe
   
Loading...