SirChief
JF-Expert Member
- Jun 23, 2014
- 3,304
- 3,367
80% ya media za marekani ni liberal wing medias na zote zilikuwa upande wake(democrats),Kwa sasa hiyo 80% ndio kila kukicha ina mu attack Trump,white privilege iko wapi hapo?.Obama alikuta nchi iko vitani ndio still aliendelea na hizo vita na 2011 alitoa order ya kuivamia Liblya kwa mwavuli wa NATO,unataka na hicho asilaumiwe?.Website ya Ikulu inatumika kutangaza mambo ya LGBTQ,unafikiri wamarekani wote wanakubaliana na mambo ya LGBTQ??,Kwa nini wasimlaumu?,Kipindi cha Obama ndio kipindi Iran ilijitanua,Russia ilijitanua,China ilipata nguvu kubwa ya kiuchumi kutokana na mkataba wa TPP ambao Obama aliingia na China,Unataka na hiyo wasiseme?.Obama alifanya mambo mazuri mengi sana tu,ila kama ilivyo binadamu yeyote alifanya makosa yake na ilibidi alaumiwe,sio kwa sababu ya rangi yake hapana ila kwa sababu ya makosa yale..Pale US kuna ujinga kwamba eti mtu wa rangi nyiingine akifanya makosa akilaumiwa wanasema ni Racism,sio sawa.Wngekuwa US ni wabaguzi kiasi hicho hakuna mweusi angekanyaga Ikulu wala bungeni pale USA,angekatwa na mapema na hiyo unayoiita white privileged system.Racism ipo ila iko exaggerated sana kuliko kawaida..Alisumbuliwa sana na "The Privileged White America" hasa wale wa upande wa pili pamoja na vyombo vyao vya habari: Binafsi naamini kuna mambo mengi mazuri angeyafanya yule mzee lakini hakufanikiwa kwasababu ya hujuma za kisiasa. Alipokea nchi ambayo tayari ilikuwa iko kwenye vita na anaingia madarakani mwaka 2008 akakaribishwa na anguko la kiuchumi: Mwisho wa siku yeye ndiye aliyelaumiwa kwa matatizo ya Marekani ambayo yalikuwepo kwa muda mrefu.