Ni vichekesho na vituko ndiyo vimejaa hapo TANESCO, hili ndiyo shimo la kuzimu lisiloweza kujazwa na vijisenti vyote vya Watanzania. Watu wanaofahamika walibeba magunia ya mabillion ya shilingi na bado leo wanatanua mitaani tu huku tukiambiwa kuwa mahakama ya mafisadi eti imekosa kesi za kushughulikia? maanake ni kwamba Tanzania hakuna mafisadi.
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano ya watu wa Tanzania akiwa Bukoba alitengua uteuzi wa Mkurugenzi wa TANESCO bwana Mramba kwa kutaka kuongeza bei ya umeme kwa 8%.
Inawezekana kabisa ongezeko hili linachagizwa na ukweli kwamba hapo TANESCO kuna mikataba isiyo na faida kwanza kwa shirika lenyewe na kwa taifa kwa ujumla.
Na hili ndilo tatizo kubwa linalolikumba hili shirika kushindwa kujiendesha na kuwapatia watanzania umeme wa bei ya chini maana limezungukwa na ufisadi usioelezeka. Mramba anajua vizuri ni kwanini kuna mikataba ya aina hiyo. Muhongo hawezi kukwepa juu ya uwepo wa hiyo mikataba, na hawa ndiyo watu tunaowategemea watusaidie kupatikana kwa umeme nafuu?
Hebu fikiria ni kwanini watu walichota escrow bado wapo tena wanajulikana vizuri tu huku tukisema tunapambana na ufisadi?
Kweli tunahitaji kumuombea tu Rais ili moyo wake na niya ya kupambana na ufisadi ishike kasi zaidi. Bila mkono wa Mungu kumtia nguvu Rais, IPTL, Symbion, na mengine mengi ni ngumu mno kuufikia umeme wa bei nafuu kwa Watanzania. Bado faru John hajulikani aliko, bado mzungu anamiliki sehemu katikati ya mbuga zetu za wanyama, bado mwarabu wa loliondo,
Mungu mbariki na umtie nguvu Rais ili afanikiwe kuishinda hii dhuruma tuliyoifanya sisi na viongozi waliopita juu ya taifa letu sisi wenyewe.