Kama wewe ni mmiliki wa kampuni pita hapa...Tangazo kwa Umma

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,972
1,083
TANGAZO KWA UMMA
KWA WAMILIKI WOTE WA MAKAMPUNI NCHINI
Kila Kampuni iliyosajiliwa nchini Tanzania ina wajibu wa kuwasilisha kwa Msajili Wa Makampuni MAREJESHO YA MWAKA (Annual Returns), kila mwaka,
yakiambatana na MAHESABU ya Kampuni yaliyokaguliwa na kupitishwa na Mkaguzi, chini ya vifungu 128(1) na 132(1) vya Sheria ya Makampuni (Sura
212).
Aidha Matawi ya Makampuni ya Kigeni yaliyoandikishwa nchini Tanzania pia yanapaswa kuwasilisha MAHESABU YA MWAKA (Annual Accounts) kila
mwaka, chini ya kifungu 438(1) cha Sheria hiyo.
Kutokuwasilisha kwa Taarifa na Nyaraka hizo ni kosa kisheria ambalo linaweza kusababisha Kampuni husika kufutwa, Wamiliki na Wakurugenzi wake
kufikishwa Mahakamani au vyote viwili kwa pamoja.
Tangazo hili ni kuyataka Makampuni yote ambayo hayajawasilisha Marejesho au Mahesabu yao kama inavyopaswa, kufanya hivyo ndani ya miezi mitatu
kuanzia tarehe 1 Februari 2017.
Zoezi la kuyafuta makampuni yatakayoshindwa kutekeleza Agizo hili na kuwafikisha wamiliki wake kwenye vyombo vya Sheria litaanza mara baada ya
kumalizika muda huo uliotolewa, tarehe 1 Mei 2017.
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya makampuni yanayodaiwa, Msajili ataendelea kutoa orodha ya wadaiwa wengine kadri zoezi la uhakiki linavyoendelea.
 

Attachments

  • tangazo_swahili.pdf
    14.3 MB · Views: 547
Back
Top Bottom