Kama wewe ni mfanyakazi na mwanachama wa nssf hii inakuhusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama wewe ni mfanyakazi na mwanachama wa nssf hii inakuhusu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JRK, Jul 23, 2012.

 1. J

  JRK Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [FONT=&quot]Kumb. Na. AE/164/334/Vol.II/2[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Makamu wa Rais, Corporate Affairs[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Barrick Gold[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]S.L.P 1081[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Dar-es-Salaam[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]20 JULAI, 2012[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya[/FONT]
  [FONT=&quot]Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili,[/FONT]
  [FONT=&quot]2012[/FONT][FONT=&quot]. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza[/FONT]
  [FONT=&quot]kutumika rasmi[/FONT][FONT=&quot]. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini[/FONT]
  [FONT=&quot]mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits)[/FONT]
  [FONT=&quot]yamefutwa[/FONT][FONT=&quot] na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa[/FONT]
  [FONT=&quot]pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko[/FONT]
  [FONT=&quot]atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55)[/FONT]
  [FONT=&quot]au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya[/FONT]
  [FONT=&quot]nyumba[/FONT][FONT=&quot] kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye[/FONT]
  [FONT=&quot]Sheria ya SSRA kipengele cha 38.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza[/FONT]
  [FONT=&quot]lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa[/FONT]
  [FONT=&quot]mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu[/FONT]
  [FONT=&quot]maisha ya uzeeni[/FONT][FONT=&quot] wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi[/FONT]
  [FONT=&quot]pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya[/FONT]
  [FONT=&quot]hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia[/FONT]
  [FONT=&quot]wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu[/FONT]
  [FONT=&quot]tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu[/FONT]
  [FONT=&quot]kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena[/FONT]
  [FONT=&quot]muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na[/FONT]
  [FONT=&quot]Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama[/FONT]
  [FONT=&quot]sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha[/FONT]
  [FONT=&quot]kazi[/FONT][FONT=&quot] kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea[/FONT]
  [FONT=&quot]haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa[/FONT]
  [FONT=&quot]kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama,[/FONT]
  [FONT=&quot]kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri[/FONT]
  [FONT=&quot]ili kupata maoni yao.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa,[/FONT]
  [FONT=&quot]mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa[/FONT]
  [FONT=&quot]kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la[/FONT]
  [FONT=&quot]ulemavu[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na[/FONT]
  [FONT=&quot]fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo[/FONT]
  [FONT=&quot]kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda[/FONT]
  [FONT=&quot]kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama[/FONT]
  [FONT=&quot]yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo[/FONT][FONT=&quot].[/FONT]
  [FONT=&quot]Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la[/FONT]
  [FONT=&quot]kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Wenu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Irene Isaka[/FONT]
  [FONT=&quot]MKURUGENZI MKUU[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
Loading...