Yapo aisee, kuna mdada alikuwa analalamika na dilemma ya possible fathers 3. Alilalwa na wanaume watatu akiwa tilatila kwenye party. Tena na hii get together ya tanga, inabidi maxence aweke doria.
Ni stori ya kweli. Mkeo ni mjamzito wa miezi nane amekuaga anaenda kwa nduguzake, wewe ukabaki home umepumzika baadae ukiwa unasikiliza redio unamsikia mkeo live kwenye redio anabishana na wanaume wawili kua mimba aliyonayo si ya kwao kama alivyokua amewaambie hapo awali bali ni yako na wakabishana sana kila mwanaume akitoa ushaid wake na mmoja wao alikua akisoma nae chuo, na ukweli ni kua wote alitembeanao bila kuvaa kinga na mkeo anakiri wote alifanyanao mapenzi maana kila mmoja alidai mimba ni yake Je? Ungekua ni wewe ndio mme wake na huyo mwanamke ungechukua uamuzi gani? Ukizingatia wewe ulimuoa baada ya kukuambia ana mimba yako. Chanzo cha stori ni Clouds fm kwenye kipindi cha njia panda, kwa waliofuatilia tupo pamoja.
Kumbe ni stori iliyotokea kweli...!!
Kumbe dunia imefika mwisho aisee...!!
Hapa hakuna kingine zaidi ya kuchukua maamuzi sahihi ya kukata kamba kwani mwanamke kishaonyesha kuwa si mkweli katika mapenzi. Huyu ni kicheche na aliolewa kwa kuangalia wapi atapata faida zaidi lakini hana mapenzi ya dhati kama walivyo mademu wengi wa siku hizi hapa Bongo. Dawa yake ni kumwacha tu na kama huyo kichanga akibainika ni wako then unamchukua kwani ukimwachia yeye anaweza kumuua ukizingatia kila jamaa kamkataa huyo demu. Hivyo kwa hasira za kususwa anaweza fanya jamba baya kwa mtoto ili awe tena single aanze ukicheche wake aje pata jibaba lingine la kulidanganya. Tupilia mbali kicheche.
Bangi nyingine bwana! Baba yenu napita tu ingawa sipendezwi na stori ya uongo na uzushi. Go tell it to the birds.
Niliyafuatilia yale mahojiano toka mwanzo paka mwisho, mbaya zaidi yul binti akaulizwa na mmoja kati ya wale jamaa wailikuwa studuio KWANINI UNATUCHANGANYA WANAUME WATATU KWA WAKATI MMOJA? Yule dada akajibu, KWASABABU NI MAZOBA. Nilichoka kwa hilo jibu Msemakweli ni DNA, ila binti ajatulia kabisaaaa
Aisee yaani yule dada mcharuko noma! Ila nilishangazwa na yule aliyekuwa aking'ang'ania mimba na hali alishafahamishshwa kuwa mtoto akizaliwa wakapime DNA.
Usimcheke anaweza kua mkeo maana kwenye kipindi waliomba kutumia majina ambayo sio yao halisi.
Ha ha ha ha hapo kazi inazidi kuwa ngumu du!Pia inawezekana sio ya hao watatu wanaojuana kuna mwingine ndo mwenye mzigo.