Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 36,155
- 30,823
Licha ya kwamba inafahamika wazi kwamba, tayari kipo chombo mahususi cha kisheria kilichoundwa na mtukufu rais ili kuondoa utata na sintofahamu juu ya jambo hilo, na kuipa tume hiyo jukumu la kutafiti, kuchunguza na hatimae kubainisha ukweli au uzushi kuhusu kilichodaiwa kutokea baada ya uchaguzi mkuu huru, wa haki na wa wazi uliofanyika kwa amani na utulivu mapema Oct.29.2025.
Pamoja na hayo, lakini bado kuna wadau mbalimbali wa JF, tena wa heshima kabisa na wengine kutoka mitandao mbalimbali ya kijamii, bila haya, woga wala aibu wanaendelea kutunga stori na habari mbalimbali zisizo na uthibitisho juu ya hicho ambacho wengi kwasasa wanaona ni kama porojo, uongo na uzushi wa kutafuta uamarufu wa kisiasa, tension au useless public sympathy. Inaaminika hivyo kwasasa kwasababu kila mtunga hiyo porojo anakuja na script yake na takwimu zake amabazo ni za kutunga na zisizo na uthibitisho wowote tena zikiwa tofauti kabisa na mtunga porojo mwingine kuhusu jambo lilelile.
Wananchi wengi wanahoji, hivi kulikoni hawajawahi kuona matanga hata moja ya wanachodai kutokea october au kuona majeruhi moja tu wa athari za wanachozusha kutokea? Picha za kutengeneza sisizo na maelezo au habari yenye utata vimezidi kutia mashaka zaidi dhidi ya porojo na uzushi huo unaochakatwa na kusambazwa na hasa mamaluki wa vibaraka wa mabwenye ya magharibi.
Kongole nyingi sana ziviendee vyombo vya habari vyote nchini ikiwa ni pamoja na magazeti, kwa weledi wao katika jukumu la kuandika, kuchakata na kutoa habari mbalimbali nchini hasa za october na kukataa kua sehemu ya kuhadaa wananchi kwa habari za uongo na uzushi hasa kuhusu oct.29.2025.
Ni muhimu sana kama wananchi wazalendo, kua wastahimilivu na wenye subra wakati ukweli ukibainishwa na tume huru ya uchunguzi, huku sote tukijiepusha na uzushi unaosambazwa na wasiolitakia mema Taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania