Kama wanalijua hili kwa nini wanadai.......?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,948
710
Sina hakika kama nina uvivu au nina makengeza wa kushindwa kutambua kile kilichodaiwa na kiongozi mmoja wa CUF. Katika madai hayo, kiongozi huyo (Naibu Katibu Mkuu wa CUF) Bw. Ismail Jussa Ladhu amesema hivi

“Ni kweli tulipokuwa wapinzani, tulikuwa tukipiga kelele kuhusiana na matumizi mabaya ya mali za umma ikiwemo magari ya serikali kutumika kwa shughuli za kichama, leo CUF ni sehemu ya Serikali, hatuwezi kwenda kinyume na misingi ya utawala bora, hilo tumeliona, lakini tayari tumeshawataarifu mawaziri na Naibu mawaziri wote kutotumia magari ya serikali katika shughuli za kichama,” alisema.

Kama kweli CUF wanalitambua hilo kuwa wao ni sehemu ya serikali, kwa nini wanadai kambi ndogo ya upinzani bungeni?? Huu so undumilakuwili?
You can't have both.
 
CUF wanauvivu wa kufikiria wakati mwingine. Wanajua wazi kuwa wao ni sehemu ya serikali then wanajiita wapinzani.... POPO hao!!
 
Kama kweli CUF wanalitambua hilo kuwa wao ni sehemu ya serikali, kwa nini wanadai kambi ndogo ya upinzani bungeni?? Huu so undumilakuwili?
You can't have both.[/QUOTE]

CUF wazushi tu hawana maana kabisa. Huoni Mwanza wamewasaliti CHADEMA? Ukiwaweka CUF kwenye upinzania ni makosa ni CCM part two hao.
 
Sina hakika kama nina uvivu au nina makengeza wa kushindwa kutambua kile kilichodaiwa na kiongozi mmoja wa CUF. Katika madai hayo, kiongozi huyo (Naibu Katibu Mkuu wa CUF) Bw. Ismail Jussa Ladhu amesema hivi

"Ni kweli tulipokuwa wapinzani, tulikuwa tukipiga kelele kuhusiana na matumizi mabaya ya mali za umma ikiwemo magari ya serikali kutumika kwa shughuli za kichama, leo CUF ni sehemu ya Serikali, hatuwezi kwenda kinyume na misingi ya utawala bora, hilo tumeliona, lakini tayari tumeshawataarifu mawaziri na Naibu mawaziri wote kutotumia magari ya serikali katika shughuli za kichama," alisema.

Kama kweli CUF wanalitambua hilo kuwa wao ni sehemu ya serikali, kwa nini wanadai kambi ndogo ya upinzani bungeni?? Huu so undumilakuwili?
You can't have both.

Hivyo mpango huu wa CUF itawahusu Mawaziri wangapi walioapishwa na Rais wa Muungano na ni Wabunge katika hilo bunge ambalo CUF wanadaikambi ndogo ya upinzani???
Watu wengine Bwana kila wanachokionyesha hadharani basi kina ushahidi wake!!
 
CUF wanauvivu wa kufikiria wakati mwingine. Wanajua wazi kuwa wao ni sehemu ya serikali then wanajiita wapinzani.... POPO hao!!

Usishangae kwani hata wewe unashangaliwa. Akili ni nywele na kila zikiwa kijivu ...
 
Tuaposhindwa kutambuwa tofauti ya Zanzibar na Tanzania basi aidha tunafanya kwa utashi au ukosefu wa nadharia.

Hivyo nyote mliotangulia pamoja na mtowa mada hamjuwi kuwa CUF wako kwenye Serikali ya Zanzibar ambako kuna Baraza la Wawakilishi na Bunge ni chombo cha kutunga Sheria Tanganyika??
 
Back
Top Bottom