Nadhani sasa hivi vibaka wa Arusha wataneemeka sana kipindi hiki.Sipati picha hapo Unga ltd na giza totoro jinsi panavyochimbika! Ngoja niwasiliane na Mganga mkuu wa Mt.Meru waongeze idadi ya nyuzi za kushonea majeraha maana vibaka wa Arusha bila kumwaga damu bado hawajakuibia.
Sakina ndo targeted area,..na hasa kuanzia maeneo ya tecnical kuja huku juu,...nafikiri wanafanya makusudi ingawa sijui lengo ni nini hasa,hili tatizo halijaanza juzi ni muda kitambo kwa sisi tunaoishi huku maeneo ya technical.
Nimetoka kuongea na Customer care Tanesco (kwa simu namba 0732 979280) kuhusu mgao mpya wa umeme cha kusikitisha jamaa anaongea huku akicheka kuwa sehemu kubwa ya Arusha haitakuwa na umeme kabisa mchana kwa majuma kadhaa..(sishangai kwani sakina kuanznia j'pili hatuna umeme) nilipomuuuliza mpaka lini akasema Mungu ndo anajua....sasa najiuliza hilo jibu maana yake ni nini wakati rais ni juzi ameingiza kampuni ya Kimarekani kuzalisha umeme....au ile kampuni ni kanyaboya wahusika wanaendelea na ishu nyingine? Jamani tutaishije tunaochomelea....wafugaji wa kuku...wauza samaki wabichi.....internet cafe......saloon sawmill mashine za kusaga.....hii mbona ni kama kukomoana?
rais nchi imemshida........tuandamane tumtoeni
wanasema kisa ni Arusha kuchagua Chadema.Tunakomolewa.
Nadhani sasa hivi vibaka wa Arusha wataneemeka sana kipindi hiki.Sipati picha hapo Unga ltd na giza totoro jinsi panavyochimbika! Ngoja niwasiliane na Mganga mkuu wa Mt.Meru waongeze idadi ya nyuzi za kushonea majeraha maana vibaka wa Arusha bila kumwaga damu bado hawajakuibia.
Tutamkumbuka EL
vibaka wa Arusha wakishakuibia ukisikia wanasema "mpe risiti."... ujue ni panga la kichwa.... yaani na hili giza..... hivi Moshi kwa mzee Ndesa....mabo ndo hivi hivi...coz hii sasa ni siasa full....
wanasema kisa ni Arusha kuchagua Chadema.Tunakomolewa.
Mkuu hii ya kupewa risiti sijawahi isikia na kama ndivyo ilivyo basi hawa mijizi imezidisha ubunifu wa kishetwani sana. Usipotaka kupokea risiti inakuwaje sasa?
Mgao umekaa kisaniii kweli.... Majumbani - usiku kucha giza.... makazini - mchana hakuna umeme(kama huna generator kazi inalala) Mimi toka juzi sijui kama Tanesco wapo, maana nikitoka kazini kwenda nyumbani hakuna umeme, giza fullu , kombora nikiwahi kazini hakuna umeme !!! fullu matatizo!!!