Full 8
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 313
- 271
Ni aibu kwa wamiliki wa petrol station mjini dodoma kutokuwa na EFD mashine na ukihitaji wanakuonesha petrol station ya PUMA kuwa ndipo pekee unaweza ipata.
Baada ya serikali kuona mapato mengi sana yanapotelea mifukoni mwa watu kutokana na matumizi ya stakabadhi, ilikuja na mbinu mbadala ya kutumia mashine za EFD. Ni jambo zuri japo limepingwa vikali na wafanyabiashara hasa waliokua wanaficha mapato yao halisi ili watoe kiasi kidogo cha kodi.
Rais magufuli katika moja ya hotuba zake ametuhimiza watanzania kudai risiti za malipo mara baada ya kufanya manunuzi yoyote. kuna changamoto mbalimbali ambazo mimi nimeziona na napenda kuziainisha na kupendekeza nini kifanyike walau kufikia lengo hili la kukusanya kodi halali kutokana na biashara zinazofanyika nchini.
changamoto.
1. Kukosekana kwa mashine za EFD kwa wafanyabiashara.
2. Desturi ya watanzania kutodai risiti
3. Mashine za EFD kutotoa risiti kutokana na matatizo ya mtandao
Mapendekezo.
1.Serikali ihakikishe kuwa kila mfanyabiashara anakua ana mashine ya EFD ambayo inafanya kazi sawia. hii ni kutokana na kuwepo kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati wasiotumia mashine hizi kwa makusudi.
2.Kuhakikisha mtandao unapatikana vyema kwa kuzibana kampuni husika ili kisingizio hiki kisiwepo.
3.Utengenezwe mtaala ambao utawafundisha watoto umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti ili wakue wakijua kuwa kwa kufanya hivyo unatimiza wajibu kama mtanzania.
4. Waandae promotions/appreciation na tuzo kwa mtu/watu wakaofanya vizuri katika kudai na kutoa risiti ili iwe chachu kwa watu kutekeleza wajibu huu kwani anakua anategemea kuwa mshindi hivyo kudai/kutoa risiti kwa juhudi zote.