Kama unafikiri umepatwa na mitihani mikubwa hebu mfikirie mwanafunzi huyu

Inna lillah wainaillah rajuun.....hakika sisi wote ni wa Allah
Allah hatupi Mitihani ila tunayoiweza
Mungu ampe nguvu zenye kukabiliana na Mtihani huu mkubwa
 
Inauma jamani Mungu amtie nguvu huyo mwanafunzi akabiliane na ukweli atakaokutana nao
 
Kila mtu ana machungu yake, machungu ya huyo binti hayawezi kupunguza machungu yangu mimi. Pole kwa wafiwa
 
Uzembe wa Baba ndio umewakost. Dereva alitakiwa kuwa makini mana alikua haoni daraja.
Afu si lazima kubebana familia nzima kisa graduation
Si lazima kwako wewe, but kwao ilikua ni UPENDO tu wanaenda shuleni kwa mwanao,
Na hakuna uzembe sababu mimi na wewe hatujui tokea gari inakaribia maeneo hayo kulitokea nini na nini kilikua mawazoni mwao na maongezi yao humo ndani ya gari.
 
Auz uko sawa kutoa tahadhari ila mungu ana mipango yake.Huwezi jua mungu aliwahitaji kwa njia hiyo si ajabu wasingesafiri siku hiyo angewachukua kwa njia ingine mfano moto,radi n.k
Ila mungu awape nguvu waliobaki
Tusilazimishe mambo hasa mama asili anapohusika. Kama mvua inamwaiga kupita kiasi na kuna mafuriko, endesha taratibu na ikibidi sitisha safari ikiwa haiwezekani kuendelea au kurudi ulikotoka.
Wapumzike kwa Amani!
 
Ifikie hatua tuambiane Ukweli.

Kwanza pole kwa binti kwa msiba mzito.

Pili hao wazazi walikuwa wapumbavu kupitiliza, hivi inakuwaje unaona mvua zinanyesha vya kutosha halafu bado unajifanya unataka uwahi tukio fulani ili hali unajua kabisa maji huwa hayana majadiliano yanapokuwa mengi!
Rejea tukio la yule Askari usalama na familia yake miaka kadhaa iliyopita ni Morogoro au Dodoma, sikumbuki vizuri eneo lilipotukia tukio hilo. Kuna vitu vingine tunakuwa tunavitaka wenyewe kutokea.

Pia kwenye namna ya vyombo vya kusafiria tumekuwa sijui ni ujinga au upumbavu!? Mtu unakuta anasafiri na hivi vigari vidogo sijui ki Premio, Crown, IST, Vitz, Rav4! Hizi ni gari za Trip town, unakwenda kazini au sokoni na kurudi nyumbani. Unataka kusafiri kuna gari za kusafiri.
 
Hizo gari za kusafiria ndo zipi mkuu, ukisafiria nazo ndo hautapata ajali. Cha msingi ni kuwa makini unapokuwa barabarani.
 
[/QUOTE
Umeshakutana na Nissan Patrol au Safari ngapi zimepinduka!? Au Benz au BMW!? Umakini unatakiwa popote pale lakini mara nyingine tuwe na kuwaza kwa Uyakinifu kabla ya kuanza kufanya jambo
 
Kama unafikiri umepatwa na mitihani mikubwa mfikirie huyu mwanafunzi wangu... Ni msichana wa kidato cha nne ambaye wiki ijayo anaanza mitihani ya kumaliza kidato cha nne ila sio mitihani hiyo ninayotaka kuwaeleza... Jumamosi ilikuwa graduation yao.Hivyo alitarajia wazazi wake wanakuja.Na alipigiwa simu kwamba safari imeanza tunakuja.

Lahaula.Graduation imeanza mpaka imeisha haoni wazazi waliosema wanakuja.Anaomba simu kuwapigia hawapatikani.Giza linaingia bado hawapatikani wala hawafiki.ANALIA.

Baadhi ya waalimu,wanafunzi wenzake na wageni waliokuja kwenye graduation wanambembeleza.Wanamuambia "nyamaza usilie kuna dharura kwenye maisha ni kawaida."Sherehe inaisha watu wanatawanyika.

Kesho yake anataka tena wazazi wapigiwe simu waulizwe kulikoni?Simu zote hazipatikani.

Jioni tena inafika.Simu inapigwa kutoka Dar.Waliopiga wanaulizia kama wazazi wa mwanafunzi (huyu tunayemzungumzia)walifika jana maana na wao wanawapigia hawapatikani na hawajarudi!!?? Ndipo ufuatiliaji kutoka pande zote unafanyika.Ukweli unafahamika.Ni ukweli mchungu.Lakini ndio ukweli.Wazazi wa mwanafunzi wetu huyu wakiwa na familia nzima ndani ya gari maeneo ya Tanga daraja lilipoharibiwa na mafuriko walizama kwenye maji na gari yao.Wamefariki wote watano.Baba mama dada wawili na mdogo wake wa miezi kadhaa.

Mpaka sasa mwili wa mtoto mdogo bado haujapatikana.Miili ya wengine imepatikana ikiwa imeharibika vibaya.

Usiku huu wanazikwa Dar es salaam.Wameharibika sana hawatangoja kesho.

Mwanafunzi wetu hatumuambii.Afanye mitihani ya form four kwanza.akimaliza anarudi nyumani kukutana na mitihani migumu zaidiView attachment 1250042
Katika maisha kuna nyakati mbili......Nyakati za furaha na nyakat za huzun zote hiz hatuna bud kuzpitia
 
Jamani pole nyingi sana kwa bint na pia MUNGU awarehem mar when wote! Ila narudia tena ni hatari sana kusafiri familia nzima kwenye chombo kimoja cha usafir iwe private car, basi Suz Ndege!! Kama kuna ulazima familia ijigawe kwa makundi na isafiri kwa usafiri tofauti.
 
Viatu havivaliki hata na uzee huu siviwezi.

Giza tororo. Mungu tu anaweza haya. Atamvusha
 
Kama unafikiri umepatwa na mitihani mikubwa mfikirie huyu mwanafunzi wangu... Ni msichana wa kidato cha nne ambaye wiki ijayo anaanza mitihani ya kumaliza kidato cha nne ila sio mitihani hiyo ninayotaka kuwaeleza... Jumamosi ilikuwa graduation yao.Hivyo alitarajia wazazi wake wanakuja.Na alipigiwa simu kwamba safari imeanza tunakuja.

Lahaula.Graduation imeanza mpaka imeisha haoni wazazi waliosema wanakuja.Anaomba simu kuwapigia hawapatikani.Giza linaingia bado hawapatikani wala hawafiki.ANALIA.

Baadhi ya waalimu,wanafunzi wenzake na wageni waliokuja kwenye graduation wanambembeleza.Wanamuambia "nyamaza usilie kuna dharura kwenye maisha ni kawaida."Sherehe inaisha watu wanatawanyika.

Kesho yake anataka tena wazazi wapigiwe simu waulizwe kulikoni?Simu zote hazipatikani.

Jioni tena inafika.Simu inapigwa kutoka Dar.Waliopiga wanaulizia kama wazazi wa mwanafunzi (huyu tunayemzungumzia)walifika jana maana na wao wanawapigia hawapatikani na hawajarudi!!?? Ndipo ufuatiliaji kutoka pande zote unafanyika.Ukweli unafahamika.Ni ukweli mchungu.Lakini ndio ukweli.Wazazi wa mwanafunzi wetu huyu wakiwa na familia nzima ndani ya gari maeneo ya Tanga daraja lilipoharibiwa na mafuriko walizama kwenye maji na gari yao.Wamefariki wote watano.Baba mama dada wawili na mdogo wake wa miezi kadhaa.

Mpaka sasa mwili wa mtoto mdogo bado haujapatikana.Miili ya wengine imepatikana ikiwa imeharibika vibaya.

Usiku huu wanazikwa Dar es salaam.Wameharibika sana hawatangoja kesho.

Mwanafunzi wetu hatumuambii.Afanye mitihani ya form four kwanza.akimaliza anarudi nyumani kukutana na mitihani migumu zaidiView attachment 1250042

Sasa mkuu na Hii mitandao kama Mimi wa mbali nasoma je Hawa wanafunzi wa kizazi cha Leo. Kama kafichwa habari ilipaswa nanyi mvumilie. Ingawa kama mwanadamu Nina Hakika nafsi yake itaguswa na Hali fulani ya Ajabu. Damu nzito.
 
Back
Top Bottom