Kama unafikiri umepatwa na mitihani mikubwa hebu mfikirie mwanafunzi huyu

hao wamama kama wako kwenye msiba wa ndugu yangu nawatoa nduki pumbavu zao wengine wako kwenye majonzi wao wamekalia kupiga picha ili wakaposti mitandaoni...mijinga sana
Aisee hii tabia ni mbaya sana. Kama jumuia tujitahidi kuikomesha. Msibani siyo sehemu ya kupiga picha kama uko kwenye harusi.
 
Hii ni mipango ya Mungu sio

Cc Kiranga

Unamwongeleaje sir God Mzee 😅
Huyu fictional character anayeitwa Mungu tunamsingizia mengi sana.Yeye pamoja na mwenzake Shetani ni characters wanaosingiziwa mambo kuliko wengine wowote katika historia.

Inabidi tuchukue wajibu zaidi kubadili mambo sisi wenyewe bila kuwasingizia hawa characters.
 
Masista wa shule anayosoma Mt. Mama Theresa wa Calculta wamemficha ili amalize mitihani yake, hivyo na sie tujitahidi kumficha tusitume tume kwenye mitandao
 
Huyo binti anatakiwa aandaliwe wataalamu wasaikorojia ndio wampe taarifa

Bila yakufanya hivyo Kuna uwezekano mkubwa wakumpoteza nayeye kulingana nataarifa atakayofikishiwa

Napia itakua vizuri apewe taarifa akiwa hospitali au karibu Na hospitali ili lolote Likitokea iwe Wepesi kupata msaada wamatabibu

Maana ishashuhudiwa watu wanaopata mitihani hiyo nao kufa kwapresha pindi wanapopewa taarifa km hizo

Mungu amsaidie Na ampe subra maana nimtihani mzito kwabinaadamu yeyote Yule.
 
Ukiona una magumu basi simulia unaona una afadhali. Pole sana mwanafunzi
 
Kama unafikiri umepatwa na mitihani mikubwa mfikirie huyu mwanafunzi wangu... Ni msichana wa kidato cha nne ambaye wiki ijayo anaanza mitihani ya kumaliza kidato cha nne ila sio mitihani hiyo ninayotaka kuwaeleza... Jumamosi ilikuwa graduation yao.Hivyo alitarajia wazazi wake wanakuja.Na alipigiwa simu kwamba safari imeanza tunakuja.

Lahaula.Graduation imeanza mpaka imeisha haoni wazazi waliosema wanakuja.Anaomba simu kuwapigia hawapatikani.Giza linaingia bado hawapatikani wala hawafiki.ANALIA.

Baadhi ya waalimu,wanafunzi wenzake na wageni waliokuja kwenye graduation wanambembeleza.Wanamuambia "nyamaza usilie kuna dharura kwenye maisha ni kawaida."Sherehe inaisha watu wanatawanyika.

Kesho yake anataka tena wazazi wapigiwe simu waulizwe kulikoni?Simu zote hazipatikani.

Jioni tena inafika.Simu inapigwa kutoka Dar.Waliopiga wanaulizia kama wazazi wa mwanafunzi (huyu tunayemzungumzia)walifika jana maana na wao wanawapigia hawapatikani na hawajarudi!!?? Ndipo ufuatiliaji kutoka pande zote unafanyika.Ukweli unafahamika.Ni ukweli mchungu.Lakini ndio ukweli.Wazazi wa mwanafunzi wetu huyu wakiwa na familia nzima ndani ya gari maeneo ya Tanga daraja lilipoharibiwa na mafuriko walizama kwenye maji na gari yao.Wamefariki wote watano.Baba mama dada wawili na mdogo wake wa miezi kadhaa.

Mpaka sasa mwili wa mtoto mdogo bado haujapatikana.Miili ya wengine imepatikana ikiwa imeharibika vibaya.

Usiku huu wanazikwa Dar es salaam.Wameharibika sana hawatangoja kesho.

Mwanafunzi wetu hatumuambii.Afanye mitihani ya form four kwanza.akimaliza anarudi nyumani kukutana na mitihani migumu zaidiView attachment 1250042
nimepitia mengi ndo hadithi ya kila muumini
 
Hii habari mbona vyombo vingi vya habari hatukuona?tuliona ile Noah ya iliyoua watu saba tu hii nayo news ilikua hit lkn ndio naiona leo jamii forums
R.I.P family
 
Ndio hio mkuu hao watu saba ni familia ya huyu mwanafunzi
Hii habari mbona vyombo vingi vya habari hatukuona?tuliona ile Noah ya iliyoua watu saba tu hii nayo news ilikua hit lkn ndio naiona leo jamii forums
R.I.P family
 
amina
Hakuna faraja unayoweza ipata hapa duniani tena.
Jaribu kujiweka katika nafasi ya huyu mtoto.. inatisha sana,inaogofya sana,huzuni yake haina mfano.

Mungu mwenyezi pekee anaweza mpa uhai huyu aliyebaki.

Namuombea kwa Mungu apate faraja na tulizo la moyo na akili kwa haya yaliyomkuta. Mungu mtazame mtoto huyu kwa upendo wako unaotukirimia.
 
Mungu pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuchukua/kutoa roho ya Binadamu yeyote yule duniani.

MATHAYO 10:28.

"Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum."
Sijasema Mungu hana uwezo wa kuua.Wakati wa Nuhu aliua,wakati wa Sodoma aliua.
Mungu anapoua hutoa tahadhali,onyo mapema na kutoa nafasi ya mtu kujirekebisha.
Lakini gari linapinduka unasema eti ni kazi ya Mungu ni kumsingizia Mungu.
Yohana 8:44 Ninyi mmetoka kwa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kufanya tamaa za baba yenu. Alikuwa muuaji alipoanza, naye hakusimama imara katika kweli, kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anaposema uwongo, yeye husema kulingana na mwelekeo wake mwenyewe, kwa sababu yeye ni mwongo na ndiye baba ya uwongo.
 
Sijasema Mungu hana uwezo wa kuua.Wakati wa Nuhu aliua,wakati wa Sodoma aliua.
Mungu anapoua hutoa tahadhali,onyo mapema na kutoa nafasi ya mtu kujirekebisha.
Lakini gari linapinduka unasema eti ni kazi ya Mungu ni kumsingizia Mungu.
Yohana 8:44 Ninyi mmetoka kwa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kufanya tamaa za baba yenu. Alikuwa muuaji alipoanza, naye hakusimama imara katika kweli, kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anaposema uwongo, yeye husema kulingana na mwelekeo wake mwenyewe, kwa sababu yeye ni mwongo na ndiye baba ya uwongo.
Sasa Mtu na familia yake akiwa safarini kwenda kusherehekea kumaliza form four kwa Mtoto wake ili ampongeze ndiko kutamani kufa?

Endelea kuteseka sana kwa kutojitambua.
 
Back
Top Bottom