Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Wanawake wa Dar wana Viwango vyao vya Hela.. Ukiwa unampa 50,000-90,000 utakuwa unaitw aJina lako tu, Goodmorning Kelvin..Hallow Kelvin How is your Day...Goodnite Kelvin. Ukiwa unampa kati ya 100,000 na 150,000 utakuwa unaitwa DEAR...Morning Dear..Umeamkaje Dear..Dear Umekula??Usiku mwema Dear usisahau kuniamsha Asubuhi Ukiwa unatoa kati ya 200,000-300,000 hapa utakuwa unaitwa BABY...Baby Hows ur day..Baby naumwa kweli leo...Baby naenda Mwenge see u later Ukihonga 300,000 na kuendelea hawa ndo wanaitwa HUBBY AKE...Utapendwa wewe hadi ushaangae...Kila kitu Hubby Ake...Hubby nimejikwaa...Hubby ndo nafunga mlango...Hubby kuna Mende chumbani njoo tulale wote...Hubby hivi unanipenda??NA swali lao KUBWA,Hubby hivi utanioa lini?? Chagua jina unalotaka...Mahaba ya siku hizi ni kama MENU ya MPESA, Unajihukumu mwenyewe Wengi mtakuwa mnaishia kuitwa DEAR na BABY tu...Tikisa Wallet kidogo na wewe kabla hujafa uitwe HUBBY AKE, Ukifikia level ya kuitwa HUBBY basi hata ukijamba utasikia....pole HUBBY umeumia 🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂😜😜😜😜
 
Jaman ifike mahali tuheshimiane, nimevumilia sana ila nimeshindwa. Kwa maoni yangu na sitaki kumponda mtu yeyote, baada ya kutafakari sana na kupima uzito kwa pande zote, ninachodhani na ninadhani na nyie pia mtakubaliana na mimi, maana ni jambo lipo wazi kabisa, ikibidi nitakumbusha na mifano kadhaa kwa mustakabali wetu kama kikundi, mi naomba tu niseme na nina sababu za kuamua kulisema hili hapa. Kwa sababu zilizo wazi na nahisi na nisinukuliwe vibaya nasema hivi,(ingawa kiukweli sijali itakavyotafsiriwa na wengine) na pia nataka wote muwe mashahidi, kwakweli hata sikumbuki nilikuwa nataka kusemaje.
 
*Msimu huu wa sikukuu. Ajali hutokea* *kwa sekunde moja lakini mateso yake* *hudumu maisha*. *Helmet na Condom zivaliwe kwenye* *vichwa husika kwa shughuli husika*.... *Hususani kama chombo sio chako.😅😁😂😃
 
Kilimanjaro Bana wanachekesha Etii angalia virefu vya Maneno MOSHI=Mungu Onyesha Sehemu Hela Ilipo; ROMBO=Ruhusu Ongezeko la Mapesa Bila Ombaomba; HIMO=Hata Ikipungua Mungu Ongeza; MARANGU=Mungu Angalia Raia Ngawira Utuhakikishie; MAMBA=Mungu Ahidi Mapesa Bila Ajira; MWIKA=Mungu Wekeza Ishara Kwenye Akaunti; URU=Usitunyime Riziki Uchumi; KIBOSHO=Kila Ikipungua Baba Ondoa Siasa Hela Ongeza; MACHAME=Mungu Atupe Chanzo Halisi na Ambacho Mapesa ni Endelevu na KISHIMUNDU=Kwetu Ikikosekana Shilingi Mungu Nakuapia Dunia Utaichukia! Rusha tag wachagga wote *waambie tunasaka mahela na hatupendi ujinga sisi*😎😎😎
 
hivi wasabato mwaka mpya kwenu unaanza saa sita za usiku au jua linapozama?
 
Back
Top Bottom