Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
Nawasalimia wadau wa JF.
Kuna baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini kwetu, mwenyekiti ni kama mfalme. Tangu aingie madarakani hana mpango wa kupisha wengine waweze kuongoza chama.
Na kuna vyama tangu vijulikane katibu mkuu wake ni yule yule tu. Miongo zaidi ya miwili bado yupo kwenye kiti hicho, huku akidai kugombea kuongoza nchi.
Kama kiongozi huyo ameshindwa kuleta demokrasia ndani ya chama chake je, ni halali kumwamini kiongozi huyo na chama chake?
Viongozi hao wameonekana wakijaribu na kuweza kuwafumba midomo wengine wenye nia ya kugombea kiasa cha kuwaita wasaliti na kuwaundia zengwe zito na wanabaki kuwa makabwela.
Zengwe zito linaloleta ukabwela linafanya wenye kung'amua mambo na kuwaona hao watu kama hawajajiandaa au wanataka kuwa wafalme ndani ya chama.
Ni vyema kutoa boliti kwenye jicho kabla ya kukatoa ka kibanzi kwenye jicho la wengine.