Kama tumekubali uhafidhina wa Zanzibar, tusilalamike

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Tanzania kama nchi tunapaswa kujitathimini wakati wote na sio kwa matukio tu. kule Zanzibar kinachoendelea walau kwa hii miaka 25 ya vyama vingi ni aibu.Tumeshindwa kujuwa vipaumbele vyetu Tuko njia panda. Nazungumzia Zanzibar zaidi na mwelekeo wa siasa zetu kama nchi.

Kwamba zaidi ya miaka 50 ya mapinduzi hakujaonekana umuhimu wa kuwaunganisha watu na badala yake tunawagawa zaidi. Watawala wamehiyari mbinu hii na kukubali uhafidhina kuwa ndio majaliwa ya zanzibar?

Watawala wa Tanzania wamekubali kuwalinda wahafidhina muda wote(Kundi la watawala la CCM -Zanzibar) bila kujali maslahi ya Taifa na mara zote wanawalinda na kuwasaidia. Haya yanayoikumba Tanzania sasa ya kuzuiwa misaada ni mwendelezo tu.

Ni wahafidhina hawa hawa waliosababisha Tanzania kuingia doa baya la kuzalisha wakimbizi mwaka 2001 baada ya watawala kutoheshimu demokrasia.

Ni wahafidhina hawa wanaoendesha sera za kuwagawa watu wa Zanzibar ili kupata maslahi ya kisiasa. walitengeneza mazingira ionekane CUF chama kikuu cha upinzani Zanzibar kuwa ni cha Pemba tu. Muda wote wa kuanzia miaka ya 2000 hadi leo walipanga matokeo ionekane hivyo lakini uchaguzi wa 2010 na 2015 uliwaumbuwa.

Ni wahafidhina hao hao wanaoendesha siasa za kibaguzi za wazi bila kuingiliwa na vyombo vya dola. Mbao za kupiga kauli mbiu hizo zipo na wala haziguswi.( kisonge, Kachochora na redio za chama Bahari FM) haulizwi mtu,

Ni wahafidhina hao hao tena kwa mara nyengine wameiingiza Tanzania katika mgogoro wa kidiplomasia na wahisani na kuwanyima fursa watanzania kusonga mbele. Baya zaidi tunaaminishwa kwamba haya ya sasa tushirikiane ili kujitegemea na kuachwa waliosababisha hasara hii wakipeta(wahafidhina)

Ni wahafidhina hawa kwa njia hizi za kuendekezwa na watawala(Bara)wanautikisa Muungano wetu zaidi. Maamuzi ya wazanzibari mifano( Kupinga katiba pendekezwa na uchaguzi wa oktoba,2015) maamuzi yaliingiliwa kwa nguvu za bara na kulindwa wahafidhina. Hali hii inawafanya wazanzibari kwa umoja wao(walio wengi) kuuchukia muungano.

Mifano iko mingi ya namna uhafidhina wa Zanzibar unavyolindwa na kulitia hasara taifa zima la Tanzania.

Tayari jamii ya Tanzania imegawika makundi mawili kuhusu hali hii ya sintofahamu ya wahisani kuzuiya misaada yao. Wengine wakiunga mkono ili kuheshimiwa demokrasia na wengine wakipinga kwa jina la uzalendo wa kinafiki na kubariki uhafidhina wa Zanzibar.

Watawala watambuwe kuwa Watanzania walio wengi na wazanzibari walio wengi hawaungi mkono unafiki huu na kwa hivyo wasilazimishwe kumeza uchafu wa wahafidhina wanaoungwa mkono na watawala (Bara).

Kitendo cha kuachwa wahafidhina kuitesa Tanzania ndio msingi mkuu wa sasa wa kurejesha nyuma maendeleo ya Watanzania kwa kuzalisha mitafaruku ya kisiasa kila wakati wa uchaguzi kule Zanzibar na mara hii athari zitakuwa kubwa kwa Tanzania nzima.

Ikiwa tumekubali uhafidhina wa Zanzibar basi tusije kulalamika huko mbele, tugugumie maumivu lakini tusifanye unafiki wa kujitegemea na uzalendo feki.

Ikiwa tumekubali uhafidhina wa Zanzibar, Tusilalamike.
 
Sera zenu nyie haziko static, hamjui mnachosimamia nyie bora tuu mpate kiki, watu wanakosa imani na nyie bcoz you all about destruction, politics za madaraka lishapitwa,suala la Zanzibar is the past, deal na present and future politics za maendeleo
 
Na kwa kweli bila busara za viongozi wa CUF na mwaka huu kungekuwa na wakimbizi zanzibar, Mungu wabariki viongozi wa CUF waendelee kuwa na busara
 
Back
Top Bottom