KAMA TTCL INATAKA KUSHIKA SOKO SERIOUSLY

KAMA TTCL INATAKA KUSHIKA SOKO SERIOUSLY

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,096
Reaction score
22,820
Habarini.

Nafuatilia kwa umakini agizo la mkuu wa kaya, mhehishimiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania juu ya maagizo aliyotamka kuwataka wafanya kazi na watendaji wa serikali kumiliki line ya simu ya kampuni hii ya umma. Hii si ombi ni amri.

Kwanza ni vema tukafahamu kuwa kumiliki line ya simu ya mtandao ambao ni mali ya taifa letu ni uzalendo wa hali ya juu. Kwa maana tunaruhusu pesa za wananchi kulikuza shirika lao kumiliki kwa maana shirika la taifa.

Sasa nijikite kwenye kushauri juu ya mkakati bora wa kuhakikisha hili la umiliki line kwa asilimia kubwa linazaa matunda.

Sote tunafahamu kuwa uchumi wa sasa kwa mataifa mengi kwa asilimia tisini (90%) ni uchumi wa soko hiria kwa maana nguvu za ugavi na mahitaji (Demand & Supply)ndizo zinaendesha soko kinyume na maagizo ya mhehishimiwa raisi ambae ametumia utashi wa kizalendo kutoa maagizo yale muhimu.

Napenda kushauri hili shirika ambalo limekuwapo kwa muda mrefu kujikita zaidi katika mauzo ya internet kwa kutoa vifurushi vya gharama nafuu na ujazo mzuri. Matumizi ya simu kwasasa ni 90% internet related kama vile ambavyo watumiaji wa smartphone wanavyozidi kuongezeka kila uchao.

Hali halisi katika soko kwasasa ni nani mwenye huduma bora...... Na si nani ana line nyingi ndio mafanikio yalipo.

Mimi nimeweka kapuni line za kampuni kede wa kede kama halotel, tigo, na wengineo sababu ya kuwa disappointed na huduma ambazo hazinishawishi kutumia pesa yangu kuzinunua hizo mbovu na sizizokidhi mahitaji.

Vifurushi vya TTCL internet bado viko gharama ya juu sana ukilinganisha na makampuni mengine binafsi na ukizingatia kuwa hili ni shirika la serikali.

Hakuna uchawi wala hujuma za aina yoyote bali nasema ni uzembe uliokithiri wa watendaji waliopo kutokupambana kitaalamu na kutokuwa wabunifu.

Badala ya muheshimiwa raisi kusema kila kiongozi na mtendaji wa serikali kuwa na line ya ttcl kwann watendaji wa TTCL wasiweke vifurushi kwa gharama nafuu sana ambayo itawawezesha kuamsha ugwadu wa kuitaka line ya ttcl?!

Kwani tigo au halotel walisaidiwa na raisi wa awamu ipi kupigiwa debe na hadi wakapata subscribers wengi hadi kupata boom katika mauzo na kupata faida kali hatari?!

Hawa watendaji wa TTCL wanauzoefu au ubunifu kiwango gani katika level za soko la kisasa?!

Hebu watendaji wa TTCL kuweni serious na utendaji. Na nitawafanyia figisu hadi muone uchungu kukalia hizo siti na kukuna matumbo badala ya vichwa.

Shirika la serikali eti mb 300 nanunua kwa Tsh. 500.

Me nilitengemea at least mkao wa bei ungekuwa kama ifauatavyo!

Vifurushi vya siku (saa 24)
500 mb = Tsh 250
1gb = Tsh 500
2gb= Tsh 700 au 800
4gb = 1,000
6gb = 1,500
8gb = 2,000
20gb =4,000

Vifurushi vya wiki (siku 7)

4gb= 500
8gb=1,000
10gb=2,000
15gb=2,500
20gb =4,000
30gb=5,000

Vifurushi vya mwezi (siku 30)
10gb= 4,000
20gb= 8,000
40gb= 10,000
60gb=15,000
80gb=20,000
100gb=30,000

Waweke hivi vifurushi halafu watajionea balaa lake idadi ya wateja watakaopokea kwa siku....... Hakuna uchawi ni kusacrifice tu bei za chini kwaajiri ya wateja uone kama mambo hayatojibu.
 
we jamaa hizo bei zako unajua kua TTCL ni 4G lakini? mbona unaweka bei za mitandao ya 3G ambao nao sidhan kama wana hizo bei.

Kisa wateja ndio wawape vitu bure asee HAPANA hata mimi staki mteremko wa hivyo ndio dalili za kuja kuolewa bure bila mahari.
 
Vifurushi vya TTCL internet bado viko gharama ya juu sana ukilinganisha na makampuni mengine binafsi na ukizingatia kuwa hili ni shirika la serikali.
Mkuu umeongea vyema sana ila hapo natofautiana na wewe. Hebu tuwekee na bei za tigo, vodacom, airtel, halotel n.k tulinganishe tuone ni kampuni gani yenye vifurushu ghali
 
we jamaa hizo bei zako unajua kua TTCL ni 4G lakini? mbona unaweka bei za mitandao ya 3G ambao nao sidhan kama wana hizo bei.

Kisa wateja ndio wawape vitu bure asee HAPANA hata mimi staki mteremko wa hivyo ndio dalili za kuja kuolewa bure bila mahari.
Unaelewa tofauti ya shirika la umma/serikali na shirika binafsi.....?!

Unadhani tutafikia vipi yale malengo ya jamii kuwa na access ya internet kwa 99% na 80% population iwe ni watumiaji wakudumu?!

Nyie ndio sampuli ya watu waliopo katika meza za maamuzi za ofisi za serikali, ushamba, ubinafsi na roho ya korosho plus umangi meza ndizo sifa zenu za utendaji na ndio sababu kubwa inayopelekea taasisi za serikali zinafeli sababu mnashindwa kutake risks na kufanya maamuzi magumu.

Kampuni kama fastjet walikuja kuvunja ule mwiko wa muda mrefu ambapo kampuni za ndege zilikuwa inachaji nauli juu sana.... Ila wao wakaja kitofauti.

Tigo walikuja kuvunja mwiko wa matumizi ya simu ya gharama ambayo hayakuwa na vifurushi na vocha zilikuwa juu sana kuanzia 5000 huko..... Wao wakaja tofauti leo unaona tuna hadi vocha ya shilling mia.

Sasa kwann shirika la serikali lishindwe kufanya hivyo kushusha bei na lina ruzuku na ulinzi wa serikali?!
 
Mkuu umeongea vyema sana ila hapo natofautiana na wewe. Hebu tuwekee na bei za tigo, vodacom, airtel, halotel n.k tulinganishe tuone ni kampuni gani yenye vifurushu ghali
Sawa ngoja.....
 
Sawa ngoja.....
Hiyo ni Airtel siku na wiki
20190528_192530.jpeg
20190528_192631.jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_20190528-192416.jpeg
    Screenshot_20190528-192416.jpeg
    19.7 KB · Views: 36
Mimi namuunga mkono rais Magufuli kwa kulazimisha 'vibopa' si kununua tu line za Ttcl bali kuziumia kwa shurti.

Hapo mapungufu na figisu za Ttcl zitaonekana mapema sana.

Shirika lenye sifa kubwa litasuasuaje katika utoaji wa huduma na kuwa nyuma ya makampuni binafsi kwa ufanisi na ubora?

Ushauri wote wa wadau unaotolewa humu hausikilizwi na hawana muda huo!

Hadi huwa najiuliza, kuna ajenda gani ya siri nyuma ya kusuasua makusudi kwa kampuni?

Hivi hilo gawio wanalolitoa kwa serikali, ni matokeo ya faida kweli ama ni michango ya mafisadi kwa serikali ili kuidhoofisha Ttcl?

Hadi tunavyoongea hapa, shirika halina minara yake specific maeneo mengi.
Inatoa mawasiliano kwa kujishikiza ama kupanga kwenye minara ya makampuni mengine binafsi!

Tukija kwenye ajira, ndiyo utashangaa! Ofisi nzima utakuta vimbabu vilivyoongezewa muda wa kustaafu vikihudumu na mvi zao sehemu ambazo zinastahili kufanywa na damu changa.com! Hawataki kuajiri vijana kuweza kukidhi mawazo mapya na ushindani

Ttcl wajitathimini pakubwa na huenda hata hizo sifa wanazopewa na mheshimiwa rais kwa kutoa gawio serikalini wanguwangu ni ghilba za kuficha mapungufu waliyonayo ili kulinda vitumbua kwa ajili kushibisha matumbo yao.
 
Ila mimi katika kitu kinaniboa ni hii tabia ya serikali kutokuongeza ajira mpya kwa kuacha wazee wenye umri wa kustaafu kuwapo makazini
 
Kwanza waanze coverage ya network, kwasababu maeneo mengi mno, internet ni ipo na speed ndogo.. yaani afadhali hata mwendo wa kobe
Si unaona hamna kitu kabisa..... Wanadhani sijui wote tunatumia tecno
 
Unaelewa tofauti ya shirika la umma/serikali na shirika binafsi.....?!

Unadhani tutafikia vipi yale malengo ya jamii kuwa na access ya internet kwa 99% na 80% population iwe ni watumiaji wakudumu?!

Nyie ndio sampuli ya watu waliopo katika meza za maamuzi za ofisi za serikali, ushamba, ubinafsi na roho ya korosho plus umangi meza ndizo sifa zenu za utendaji na ndio sababu kubwa inayopelekea taasisi za serikali zinafeli sababu mnashindwa kutake risks na kufanya maamuzi magumu.

Kampuni kama fastjet walikuja kuvunja ule mwiko wa muda mrefu ambapo kampuni za ndege zilikuwa inachaji nauli juu sana.... Ila wao wakaja kitofauti.

Tigo walikuja kuvunja mwiko wa matumizi ya simu ya gharama ambayo hayakuwa na vifurushi na vocha zilikuwa juu sana kuanzia 5000 huko..... Wao wakaja tofauti leo unaona tuna hadi vocha ya shilling mia.

Sasa kwann shirika la serikali lishindwe kufanya hivyo kushusha bei na lina ruzuku na ulinzi wa serikali?!
Its not just about risk taking but there should be very caluculated move, taking greatest risk at the highest profit not greatest risk at the lowest profit...

Kushusha gharama ya vifurushi sio njia sahihi wala kipaumbele kwa TTCL angalau si kwa sasa, maana bado hawajawafikia hata hao wateja kwa sehemu kubwa nchini, wakifanya hiyo promotion ya kushusha bei ina tija gani zaidi sana sana watapata hasara shirika halitakuwa linajiendesha lenyewe bila kutegemea ruzuku, wanahitajika kusambaza na kuboresha huduma kwanza ili kuongeza markert share, kama ulisikiliza kwenye hotuba yao kwenye gawio,wanahitaji trilioni kuboresha huduma ikiwa pamoja na kuweka minara.

Halafu si kushusha bei tu bali kuboresha huduma its not just about quantity but quality matters the most.
 
Nadhani kuna watu walisema the same scary staff kwa tigo halotel, kampuni ambazo zimeleta mapinduzi ya kimatumizi na kuuza kwa kasi ndani ya muda mfupi na kuongeza marketshare yao. Sikiliza nikwambie ndugu, katika biashara sometimes kuna ile hali ya "stalemate" ambapo kila mtu anahofia kutake the first move kwa kuhofia kupata loss na kupoteza revenue sokoni..... And when that happens ndipo kampuni huwa zinakuwa almost the same kwenye bei za bidhaa na huduma ili kubreak even.

Lakini, nikwambie tu jambo moja ni kwamba, kampuni ambazo huja na idea ya tofauti ya kihuduma na kwa bei nafuu ndio hufanikiwa kubreak hiyo stalemate scenario na mambo hugeuka kwa hiyo kampuni kuwa leader.....

Kwa mfano kwa hawa ma ISP wa fiber kuna kampuni inaitwa ZUKU Fiber kwa sasa inaoparate upanga, masaki, msasani na maeno ya fire hapo ipo very cheap and fastest of them all na hakuna kampuni inaifikia kwa sasa..... na ni very very affordable na money value back......kitu ambacho ni tofauti katika industry ya fiber internet.

Hawa ttcl wana room ya kuexpand na kukua kama wataamua kufanya risk ya kuuza vifurushi cheap below normal market prices zilizopo. Na wakifanya hivyo watakuwa wamemaliza.

Kwa upande wangu nadhani TTCL wanajaribu tu kuwa na staha na huruma maana uwezo wa kushusha bei to the minimum and lowest point impossible wanao ila tu wanaplay fair na hawa waliopo sokoni maana wakishusha ndani ya muda mfupi soko loote la watumia internet lita divert kuja kwao. Kwan nani alianza washawishi watu kununua products za halotel, it was simply the attractive, affordable and cheap packages ndizo zilifanya watu kujoin...... Same story kwa tigo ambayo ilikimbiza sana soko baada ya kuchange package ya huduma zao kwa kuleta vifurushi ya extreme ambavyo at first it looked like a very risky move ila it paid well na kampuni ilikuwa inapumulia mashine ikaanza kurudi kwenye afya yake hadi leo ni top giant ya kampuni za mitandao ya simu na internet.

Hebu niambie what could be more risky than kuruhusu watu kuongea free kutoka saa nne usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi kisha baadae kuintroduce huduma ya package ya extreme ambayo unatakiwa kulipa only 1000 Tshs, na kuongea na kutuma text (internet ilikuwa bado kipindi kile maana no smartphones kama za kileo za Google play zilikuwako) tokea saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.....Unadhani ungelikuwa ni wewe ungethubutu kushawishi panel kuruhusu hayo maamuzi na hela za wawekezaji zikiwa on stake......?!

Sasa kwann risky move iwe ni tatizo kwa shirika la serikali ambalo mbali na advantage ya kupewa ruzuku na mtaji na serikali lakini pia lina brand name so popular ambayo inatambulika tokea miaka ya 1980's.......

So kwa upande wangu i don't see the risks at all....
 
Unashangaa 500 = 300mb.??

Dah..itakuwa huijui Tigo na Voda wewe..
 
Kwanza waanze coverage ya network, kwasababu maeneo mengi mno, internet ni ipo na speed ndogo.. yaani afadhali hata mwendo wa kobe
Hizo "ni" katikati ya sentensi unaziweka makusudi au kwa kutokujua!!?
Shuleni huwa mnaenda kujifunza au kununua mabumunda?
 
Back
Top Bottom