Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 27,547
- 34,872
Ni kweli mkuu ! Angola na Zimbabwe waliisaidia sana hii DRC kipindi kile.Labda nikumbushe tu Kagame amewahi Iteka Congo nzima wakati wa 1st congo war ya kumng'oa mobutu kutokea ziwa kivu mpaka port matadi!!
Sio hivyo tu alipotaka kumng'oa Kabila aliiteka tena congo na alifika mpaka kinshasa kabisa na kama sio msaada wa Angola basi angekua ameiteka Congo nzima ndani ya wiki 2 pekee.
Kwenye vita za kileo ukubwa wa nchi hauna maana yeyote sababu vita inapiganwa kwa teknolojia nyingi mfano matumizi ya ndege na makombora ya masafa marefu kwahiyo unaweza zingirwa kwenye anga na kumalizwa ndani ya wiki tu kabla hata majeshi ya ardhini hayajafika Dodoma.
Kuna muda huwa nafikiri kama hizi nchi mbili (Angola na Zimbabwe) zisingejiingiza kwenye ile Vita upande wa Kabila huenda hii nchi (Drc) leo hii ingekuwa imepasuka vipande vipande huku Rwanda na Uganda wakidhibiti maeneo makubwa ya Madini huko Mashariki.
Drc iliyopasuka vipande vipande ingehatarisha usalama wa eneo lote la maziwa makuu, Ukanda wote wa SADC (hasa Angola, Tanzania na Zambia) na hata Africa Mashariki (Tanzania ikiwa muathirika mkubwa).