Kama TANESCO kuna uchafu hivi mashirika mengine yakoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama TANESCO kuna uchafu hivi mashirika mengine yakoje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndumule, Aug 1, 2012.

 1. N

  Ndumule Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jamii forum nimekuwa nijiuliza maswali yafuatayo na mstakabali mzima wa maendeleo yetu ya nchi. Ukweli ni kwamba kama mashirika ya umma yana ufisadi mkubwa kiasi hiki uchumi wa nchi unaangamia sana.


  1. Kama TANESCO ambayo madudu yake ni rahisi kuonekana kwa vile madudu yake yanaleta mgao lakini mafisadi walikuwa na uwezo wa kufanya waliofanya ikiwa ni pamoja na kupanga lini mgao uwepo au usiwepo je nini kinatokea kwenye mashirika mengine ambayo mambo yakiharibika si rahisi kama vile TANESCO?
  2. Usalama wa taifa walikuwa wapi kujua na kumuarifu Rais kuhusiana na ufisadi huu.
  3. Je kama serikali hii haikuweza kujua nini kinaendelea TANESCO watawezaje kujua madudu kwenye mashirika mengine kama Bandari, NSSF, PPF n.k. Kitakachotokea TANESCO baada ya kuifumua na ambacho kimeshatokea tayali National Housing kinaonyesha mashirika yetu yanaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi kama watafunaji wataondolewa.
  4. Na kama kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ilikuwa na mgongano wa kimasilahi ambao umeleta madhara makubwa kiasi hiki je mchakato wa kuwaweka wabunge kwenye kamati mbalimbali huwa unaangalia mgangano wa kimaslai. Je wabunge wanatakiwa kueleza kamati ambazo hawatakiwi kukaa kwa vile kuna mgongano wa kimaslai? Mungu ibariki Tanzania
   
Loading...