Kama sivyo, wajiandae...

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Wananchi a.k.a. Raia tumechoka,

Hivi ikitokea wazazi wamefariki na wakaacha mali halafu watoto wakabaki matabaka mawili wakubwa na wadogo, wakubwa wanataka wawanyonye ama kuwadhurumu wadogo , je nn kitafuatia katika familia hiyo?

Kama nchi hii haitapata chama mahili kitakacho takeover kwa kuichallenge ccm hapo 2025, nchi hii haitakalika tena kwa amani, hakuna atakayekula akitazamwa kama wanavyojidanganya.

Tumeona mababa wa taifa wengi wamefariki dunia, waliobaki wanajaribu kuandaa vizazi vyao ili vibaki kuendelea kitunyonya , tunasema hapana, hakuna anaekubali kuruhisu huo muundo wa utumwa na utwana unaoandaliwa na wote tunaona.

Vijana wamejaa na degree zao mitaani, ujenzi ni shida, biashara ni shida, kilimo ni shida , taifa limewashinda , kazi wizi na ufisadi, hapa kazi ni moja tu, mabadiriko ya kweli, muda ni ukuta na sasa msemo huo umetimia Tanzania.

VIONGOZI WA DINI
Hao wengi ni wanafiki , hawakemei maovu , wakasome manabii kama YEREMIA walivyosimamia haki hata walipotishwa uhai wao.
Oooh, tunatii mamlaka

Mamlaka isipotenda haki inapoteza uhalali kwa sababu MUNGU anaitwa hakimu wa haki, tayari MUNGU hazitambui hizo mamlaka ila bado zinatambuliwa na viongozi wa dini wapumbavu wanaojali tu kupata sadaka na maisha ya raha za dunia hii.

Hata Sauli mfalme wa Israeli na wafalme wengine walipomuudhi MUNGU waliuawa vitani kwa ridhaa ya MUNGU mwenyewe akiwaambia watauawa kupitia vinywa vya manabii wake. Leo viongozi wa dini wanafiki wa taifa hili wanajipemdekeza kwa viongozi waovu.

Kuna tukio moja tu litatokea kwa mfano tu , ni mfano , kama lile la kufa Akwilina Akwilini kwa risasi inayosemekana ilikuwa imuondoe mbowe, likijirudia tukio kama hilo , kwenye hamsha hamsha zinazokuja 2025, na wananchi tukiona uchaguzi hautatoa haki, tutapita nalo tukio hilo na nchi haitakalika hata mtoe vifaru barabarani, safari hii mtaelewa.

TUNASEMA WAZEE WAMEKUFA, USIUNDWE UFALME WA WATOTO WAO NCHI HII, IPATIKANE KATIBA MPYA NA CHAMA KIPYA CHA KIZALENDO CHENYE MISINGI YA UTAIFA WETU.

ALUTA JAKABOOU....
 
Back
Top Bottom