Kama sitta mbaya, wapo wapi wazuri ?

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
BMK linaendelea na vikao vyake. Licha ya kundi ukawa kususia kwa madai ya kubezwa na kuburuzwa na wajumbe kutoka CCM. Baada ya kutoka nje Ukawa, wito kutoka makundi mbalimbali umetolewa wakiwataka kurejea na kutoa hoja wanazozitoa wakiwa ndani ya bunge. Ili zijadiliwe na kama zitakubaliwa basi ziingwize katika rasimu.

Wanaowaunga mkono Ukawa wanajenga hoja kwamba mambo yanakwenda ndivyo sivyo na mwenyekiti wa BMK Samuel sitta analiburuza bunge hilo ili apitishe maoni na mapendekezo ya Chama chake kwa faida yake. Amekua akipewa lawama nyingi, zingine anastahili na nyingi hastahili, kama wale wasemao kuwa amepindua Rasimu ya katiba iliyowasilishwa bungeni na mwenyekiti warioba na eti kaiweka nyingine inayoratibiwa na Chama tawala.

Nimejaribu kutazama kama sitta anastahili lawama hizi na kugundua kuwa zinatoka kwa watu wale wale ambao kwa miaka mingi wamekua katika vita ya kisiasa. Isiyo na tija kwa taifa. Kama unataka kuamini kuwa wanaozungumza vibaya kuhusu sitta ni wapinzani wake kisiasa, Sasa wameanza kusema hafai kuwa Rais. Urais unakujaje katika uendeshaji wa vikao vya BMK. Urais unakuja kwasababu wapinzani wake wanamtengenezea zengwe ili aonekane hafai kwasababu zisizojitosheleza.

Ni vipi sitta anaweza kuvunja au kupindisha kanuni baadhi ya vipengele vilivyowasilishwa na Tume Ya jaji warioba? Ninavyijua mimi hili BMK Lina wajumbe wasiopungua 600 waliogawanyika katika kamati ndogo ndogo zilizopewa jukumu la kujadili, kupendekeza, kuondoa na kuongeza kitu wanachoona kinafaa ili kuijenga katiba mpya iliyo bora kwa ajili ya Wananchi Wote.
Kama tunasimamia kumuona sitta ndiye kila kitu bungeni maana yake tunawatusi pia wajumbe Wote wa BMK kwa kuwa wao ndiyo wanaojadili na kupendekeza mambo kwenye katiba mpya, na siyo sitta anawapelekea wao na kuwalazimisha kitu cha kujadili.

Kama Kweli uzushi huo ni Kweli iwe vipi mizengo pinda kiongozi wa shughuli serikalini bungeni na ambaye pia ametangaza nia ya kuwania Urais anamuacha sitta anapindua kanuni. Kama jambo hili linatendeka na watu tunaowategemea kama viongozi wa kitaifa wajao wanaangalia, basi tatizo kubwa liko kwao na si kwa sitta, kama bunge hili limekosa uhalali wa kisiasa, lakini linao uhalali wa kisheria, basi tatizo siyo la sitta kama mwenyekiti , Bali ni kosa la wajumbe Wote wanaondelea kusisitiza umuhimu wa kuendelea na vikao Bila baadhi ya wajumbe wenzao kuwemo.

Kwa vigezo vyote bado sitta anaendesha bunge hili vizuri kila mmoja anachangia kwa kadiri ya mawazo yake. Wote wakiwa na lengo moja tu kuhakikisha katiba bora inapatikana. Suala la sitta kufaa au kutofaa Urais ni Suala ambalo Wote wanaotajwa kuwania Urais wanapaswa kuulizwa na kuhojiwa. Kama sifa ni utendaji mbovu kwa wanaotajwa kuwania nafasi hiyo nadhani sitta ana sifa nzuri kuliko wengine kwa sababu tunajua walivyokua kwenye nafasi serikalini nini walifanya. Sitta ni mmoja wa wazee waliofanya kazi katika awamu zote nne. Alifanya kazi na baba wa Taifa na Mzee mwinyi na mzee mkapa na Sasa yupo Na J.K.

Kama wasiwasi ni kuwa sitta anatumia nafasi ya uenyekiti Wa BMK kujipigia upatu, ni uoga usio na msingi kwasababu tunaona wengine wanatumia fedha nyingi kutafuta uungwaji mkono katika makundi mbalimbali tena hata Yale waliyokua wanayapinga vita waliyokua kwenye nafasi.
 
Back
Top Bottom