Kama si Peter Serukamba,ningemchagua nani?

Kama si Peter Serukamba,ningemchagua nani?

mwankuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Posts
334
Reaction score
120
KAMA SI PETER SERUKAMBA,NINGEMCHAGUA NANI?

Ni Aprili nyingine.Na Dodoma ndiyo habari ya mjini kwa sasa.Ni habari za Bunge!Wabunge wetu wapendwa wapo Dodoma "kututengenezea maisha"kupitia bajeti.Majadiliano yanaendelea na sasa yamechukua mkondo mpya.Ni zomeazomea,tukana,vuruga,hadi kieleweke.Bora tukose wote!

Wakati wengi tukiamini kwamba wale maadui watatu tuliotangaziwa tangu tunapata uhuru,wanazidi kujiimarisha,waheshimiwa wabunge walishahama kujadili hayo,na sasa wako na ajenda mpya mezani.Sasa ni vita vya wazi kati ya CCM (SERIKALI) na Chadema kwa wema au ubaya.

Kilichotokea bungeni wiki iliyopita na kubarikiwa na uongozi wa bunge kimewashangaza wengi.Matusi ya nguoni,kama alivyofanya mheshimiwa sana Peter Serukamba,sasa ni sehemu ya bunge hili tukufu.Pamoja na kwamba nilishtuka kuona mtu mzima,achilia mbali ubunge wake,anatukana,na uongozi wa bunge ukiwa kimya,lakini haya yangeweza kutabirika.

Mimi kwa uelewa wangu mdogo,nilitegemea Mhe.Peter Serukamba kujitokeza mbele ya umma na kuomba radhi kwa alichofanya.Pengine ningemwelewa zaidi,kuliko ilivyo sasa.Hii ni busara ya kawaida sana.Pamoja na kwamba kuna watu aliwalenga,lakini kutumia chombo cha umma,ni sawa na kwamba amewatukana watanzania.Wabunge wengi wanatukana,lakini hili la Peter Serukamba limevuka kiwango cha ujinga wetu.

Watanzania wengi wamekasirishwa na kitendo hicho(sio tu cha Serukamba) na madhara yake ni kushuka kwa thamani ya bunge na ubunge.Wakati bado tunatafakari sababu za kushuka kwa idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi,masuala kama haya yanaweza kushusha zaidi idadi ya wapiga kura kwenye chaguzi zijazo.Wananchi wanaona bunge si sehemu ya kutatua matatizo yao.Wengine wanaapa kutowapigia kura baadhi ya wabunge katika uchaguzi ujao.Hapa najiuliza,usipompigia kura mbunge wa sasa,utampigia nani?

Bahati mbaya watanzania ni wasahaurifu sana,na wenye huruma,na maisha ya wengine kuliko hata maisha yao.Matukio mengi yanatokea,tunashtuka,tunashangaa na baadaye tunaendelea na maisha kama kawaida.Hakuna anayejihangaisha na suluhu.Mahala pengine,mambo kama haya yasingeweza kupita bila hatua kuchukuliwa.

Utampigia kura nani?Wengi mnaweza kujilaumu sana kwa kuwapigia kura wabunge wenu,kwa sababu wameshindwa kuwawakiliha wananchi na sasa wanatetea vyama vyao.Lakini mimi nakuomba acha kujilaumu.Hukufanya makosa kumchagua mbunge wako.Makosa ni ya jamii nzima.Katika wote waliojitokeza,hakuna ambaye angefaa kuwa mbunge!Niamini!

Mtu anayefaa kuwa mbunge yuko busy sana na mambo yake.Yuko ofisini,Yuko shambani!Mbunge bora ni nadra sana kumkuta kwenye vyama vya siasa,yuko ofisini au shambani akipiga kazi!Amejiwekea malengo na anahangaika usiku na mchana kuyafikia malengo yake na jamii kwa ujumla.

Mbunge huyu hana muda wa kukaa kijiweni na kupanga dili feki.Mbunge huyu ana kazi halali inayompatia kipato,na amekuwa msaada mkubwa kwa wanaomzunguka.Anaona kazi anayofanya inalipa zaidi kuliko hata ya ubunge.Anaona kujiunga na vyama vyua sasa,na pengine kugombea ubunge ni kupoteza muda.Anaona ubunge utamshushia heshima na kuwa mtu wa hovyo kwenye jamii.Hapendi kugombea ubunge kwa sababu anaona kazi hiyo ni mzigo,ni utumwa licha ya kwamba hawa jamaa wameweka kama ajira.

Hata akigombea ubunge,kwake kusema uongo ni mwiko na ni dhambi,na hawezi kuwaahidi ahadi hewa wananchi.Anaona kama jamii inapenda sana watu waongo kuliko wakweli.Jamii inapenda rushwa/takrima.Hivyo akijitokeza hawezi kutoa rushwa ili achaguliwe.Mbunge huyu anaona hawezi kuendeshwa na zidumu fikra za mwenyekiti wa chama.Anaona akichaguliwa na wananchi,atasimamia mambo ya wananchi na sio chama.Yuko tofauti na akina Mwigulu Nchemba (bingwa wa uchumi) ambaye yuko tayari kufa kwa ajili ya chama kuliko Taifa.Watu hawa wamekaa kando,hawataki kabisa kujihusisha na siasa,japo wanasaidia jamii kwa njia nyingine.

Watu kama hawa utawashawishi vipi kugombea ubunge?Baada ya "watu wema" kukaa kando na siasa,ndipo tunawapata akina Peter Serukamba,Livingstone Lusinde,Juma Nkamia.Godbless Lema,Joseph Mbilinyi n.k.Wananchi wamekosa upana wa kuwachagua wawakilishi,hivyo yeyote anayekuja mbele yao anafaa,au wanaamua kufumba macho na kusema 'lolote na liwe".Lakini neno hili,linatugharimu sana.Tunafanya majaribu kwenye maisha yetu!

Japo tunashangaa akina Serukamba kutukana,hali kama hii ipo sana kwenye familia zetu,shuleni,ofisini,kanisani/mskitini na mitaani.Kama jamii inaonekana,kuna pepo mbaya katupumbaza.Baba kumtukana matusi ya hovyo mwanaye,mke,jirani,n.k ni kawaida.Hivyo mlitaka Serukamba afanye nini hasa?

Ametukana,na wala hajaona kama ni kosa,na yuko Dodoma.Kwa kama hili limepita,tukio lijalo linaweza kuwa kubwa zaidi.Tusije kushangaa mtu akipigwa risasi bungeni.Utamtoa Peter Serukamba kwenye ubunge,utamweka Namanzila,na mambo yatakuwa yaleyale.Mimi ndio maana sijutii kumchagua mbunge wangu kwa sababu ndiye aliyekuwepo.

Pengine kazi inayotukabili zaidi mbele ya safari,sio kuwatoa viongozi wasiofaa kwenye madaraka,bali kuwapata wakubadili nafasi hizo ambao watasimamia masilahi mapana ya umma.Hawa ambao naamini wapo,wanaweza kutusaidia kuleta mageuzi kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.Hawa hawapatikani kijiweni au kumbi za starehe.Hawa wapo ofisini na shambani wanafanya kazi.

Baba Tusajigwe.


 
Umenena vyema ila sijaua kosa la Godbless Lema..kwangu Lema ni mbunge aliyekkamilika...anayejua haki zake na yupo tayari kufa kwa ajili ya wapiga kura wake..si muoga bali mtetezi wa raia wake..uwongo kwake mwiko ndo maana mpaka leo ushahidi dhidi ya waziri mkuu umewekwa kapuni...
 
I assure you kwamba wapiga kura wengi wa Kigoma,waliomchagua huyu bwana hawajui maana ya ' F.......off.
Tungekuwa na wapiga kura wa Ulaya au Marekani huyu mtu chama chake kingemwondolea whip,na kuombwa kujiuzulu.
 
I assure you kwamba wapiga kura wengi wa Kigoma,waliomchagua huyu bwana hawajui maana ya ' F.......off.
Tungekuwa na wapiga kura wa Ulaya au Marekani huyu mtu chama chake kingemwondolea whip,na kuombwa kujiuzulu.

Mkuu ndio maana hana hofu!kwa wengine waungwana angejitokeza na kuomba radhi.Kwa kuwa hii ndio tz,Serukamba anaweza kupita tena na kuwa mbunge kwenye uchaguzi ujao
 
Back
Top Bottom