Kama Serikali inabadili mitaala ya elimu

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375
2,000
NAIPONGEZA SANA SERIKALI KAMA IMEAMUA KUONDOA VITABU VYA ZAMANI.

Lakini angalizo langu ni swala hili liwekwe wazi kwanza uwepo mjadala wa mitaala kwanza watanzania waangalie nini mtoto wa shule ya msingi anahitaji kujifunza, nini m
toto wa sekondari anahitaji kujifunza na ni nini malengo ya kila hatua ya elimu.

Ni aibu kuona mtoto anamaliza darasa la saba eti anajua ukichanganya besi na tindikali unapata nini lakini hajui mbinu za kilimo, hajui sababu zinazoleta magonjwa na nini suluhisho, hajui kanuni za usalama katika makazi , barabarani, makazini, hana elimu yoyote ya ujasiliamali kwa kujua kuwa kila anachokifanya lazima akifanye kibiashara badala yake taifa lina asilimia kubwa ya wananchi wake elimu yao ni kuanzia form 4 na kushuka chini hawana mbinu yoyote ya kimaisha walioambulia katika elimu waliyoipata bali kukaririshwa mambo yasiyowasaidia na wakikumbana na changamoto ya kimaisha wanakimbilia kwenye upotoshaji unaofanywa na imani kwa sababu elimu yao haikuwakomboa au hawana mbinu.

Tuweke malengo ya mtoto akimaliza darasa fulani awe amepata nini na tuanzie hapo kutengeneza mitaala. Tukumbuke kuwa elimu ya maisha lazima ndio uwe msingi wa elimu ya watu wote na wale wanaobobea ndio wanakuwa wataalamu wa kuwaongezea ujuzi wananchi juu ya jambo Fulani.

Mfano tusitegemee wakulima wote waende katika vyuo vya kilimo bali tunategemea kila mtanzania apate mda wa kutosha katika elimu ya msingi kujua ili kanuni bora za kilimo, kujua kwa nini maeneo tofauti wanalima mazao tofauti, kujua mbinu za ujasiliamali katika kilimo kwa kuangalia gharama za kuzalisha, masoko, jinsi ya kuchagua ni zao gani alime kwa wakati gani kwa kuangalia soko na misimu, kujua ni mambo gani yanayoweza kumsababishia hasara katika kilimo, kujua katika kilimo jamii au serikali inaweza kuwa na mchango gani na mkulima mwenyewe anaweza kuwa na mchango gani na je jamii inaweza kunufaikaje na mkulima mwenyewe anaweza kunufaikaje.

Tukiwapa watoto wetu elimu kama hizi nadhani tutapiga hatua kimaendeleo katika mda mfupi sana.

Vitabu vya zamani vimepitwa na wkati tena sana. ukombozi mtu anaupata pale tu anapokuwa na mbinu za kukabiliana na changamoto za maisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom