Kama Seif atamkaribisha Lipumba awe Mwenyekiti, basi Jecha alikuwa sahihi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,819
49,016
Leo Lipumba ameomba kutengua barua yake ya kujiuzulu, ina maana kaomba kuendelea na uenyekiti wake.

Seif akumbuke kwenye uchaguzi wa Zanzibar uliopita aliungwa mkono na washirika wote wa UKAWA,

Hadi leo bado kuna vuguvugu la kudai mshindi wa Oktoba 25 ambaye ni Seif atangazwe.

Lipumba ambaye anadai kutaka awe Mwenyekiti tena wa chama hicho, hajatoa kauli yeyote ya kumpinga Jecha aliyepora ushindi wa Seif, kwa maana nyingine yuko upande wa Jecha.

Basi iwapo Maalim Seif atamkaribisha Lipumba, yeye Maalim na Jecha wanawachezea Wazanzibari, na kwa maana hiyo Jecha alikuwa sahihi kumwadhibu Seif kwa kuwadanganya wananchi kuwa ni mpinzani huku akishirikiana na wanaofifisha mapambano.

Naomba kuwasilisha.
 
Binafsi sikubaliani na cuf kumkaribisha lipumba kirahisi namna hii mtu ambaye aliamua kukikimbia chama kwenye wakati mgumu sana wa uchaguzi
 
Pia inawezekana lipumba akawa ni pandikizi la ccm ili kuhujumu vugu vugu la ukawa ktk kuibana ccm linalo endelea kwa sasa ili ahakikishe anavunja umoja wa wapinzani bungeni
 
Kama hamjui ngoja niwafahamishe, mapambano ya CUF Zanzibar yanajitoshereza wala hakihitajiki chama chochote kuisaidia CUF kuicha chafya CCM
so hoja yako ni mfu na kwa kuongezea Prof Lipumba anatimiza formalities tu, Plan nzima ilishachorwa ilijadiliwa na sasa ipo kwenye utekelezaji.

fact nyingine ni kwamba lipumba anakuja kuwa mwenyekiti na hapo hapo ndoa ya UKAWA inaisha, ukitaka kulithibitisha hilo rejea namna ambavyo Babu Duni alivyorejea CUF na kauli alizozitoa dhidi ya CHADEMA wakati anakihama chama hicho.

CUF hawalizishwi namna Mbowe anavyohodhi madaraka na kufanya maamuzi bila kuwashirikisha maamuzi ya Chadema kutoka tengeru au Ufipa ndio yamekuwa maamuzi ya ukawa. ushirika namna hiyo CUF hawaupendi CUF wanaona CHADEMA imevaa koti la UKAWA na hivyo kudhohofisha jitihada za CUF katika kujipambanua.

Yaani kama vile wasivyo kubali munganao wa TANGANYIKA NA ZANZIBAR kwa serikali ya tanganyika kuvaa koti la muungano hivyo hivyo wasivyokubali kwa CHADEMA kuvaa koti la UKAWA.
 
Kama hamjui ngoja niwafahamishe, mapambano ya CUF Zanzibar yanajitoshereza wala hakihitajiki chama chochote kuisaidia CUF kuicha chafya CCM
so hoja yako ni mfu na kwa kuongezea Prof Lipumba anatimiza formalities tu, Plan nzima ilishachorwa ilijadiliwa na sasa ipo kwenye utekelezaji.
fact nyingine ni kwamba lipumba anakuja kuwa mwenyekiti na hapo hapo ndoa ya UKAWA inaisha, ukitaka kulithibitisha hilo rejea namna ambavyo Babu Duni alivyorejea CUF na kauli alizozitoa dhidi ya CHADEMA wakati anakihama chama hicho.

CUF hawalizishwi namna Mbowe anavyohodhi madaraka na kufanya maamuzi bila kuwashirikisha
maamuzi ya Chadema kutoka tengeru au Ufipa ndio yamekuwa maamuzi ya ukawa. ushirika namna hiyo CUF hawaupendi
CUF wanaona CHADEMA imevaa koti la UKAWA na hivyo kudhohofisha jitihada za CUF katika kujipambanua

CUF wajiandae kupungua/kupoteza idadi kubwa ya wabunge na madiwani mwaka 2020
 
Binafsi sikubaliani na cuf kumkaribisha lipumba kirahisi namna hii mtu ambaye aliamua kukikimbia chama kwenye wakati mgumu sana wa uchaguzi
Lipumba alikuwa sahihi kumkataa Lowassa......anarudi chama chake alichokizoea.....usishangae siku moja ukisikia Lowassa nae anarudi CCM.....Medeye kaonesha hilo kuwa linawezekana
 
Pia inawezekana lipumba akawa ni pandikizi la ccm ili kuhujumu vugu vugu la ukawa ktk kuibana ccm linalo endelea kwa sasa ili ahakikishe anavunja umoja wa wapinzani bungeni
Mapandikizi ya CCM bado hayajaisha.....Medeye kaanza.....bado Masha, Msindai, Lembeli, Sumaye kisha unamalizia na Lowassa.
 
Kama hamjui ngoja niwafahamishe, mapambano ya CUF Zanzibar yanajitoshereza wala hakihitajiki chama chochote kuisaidia CUF kuicha chafya CCM
so hoja yako ni mfu na kwa kuongezea Prof Lipumba anatimiza formalities tu, Plan nzima ilishachorwa ilijadiliwa na sasa ipo kwenye utekelezaji.
fact nyingine ni kwamba lipumba anakuja kuwa mwenyekiti na hapo hapo ndoa ya UKAWA inaisha, ukitaka kulithibitisha hilo rejea namna ambavyo Babu Duni alivyorejea CUF na kauli alizozitoa dhidi ya CHADEMA wakati anakihama chama hicho.

CUF hawalizishwi namna Mbowe anavyohodhi madaraka na kufanya maamuzi bila kuwashirikisha
maamuzi ya Chadema kutoka tengeru au Ufipa ndio yamekuwa maamuzi ya ukawa. ushirika namna hiyo CUF hawaupendi
CUF wanaona CHADEMA imevaa koti la UKAWA na hivyo kudhohofisha jitihada za CUF katika kujipambanua
Yaani kama vile wasivyo kubali munganao wa TANGANYIKA NA ZANZIBAR kwa serikali ya tanganyika kuvaa koti la muungano hivyo hivyo wasivyokubali kwa CHADEMA kuvaa koti la UKAWA.

....umeandika kishabiki,kizandiki, umejaa husda,una chuki,kiherehere yaani kama wewe ni mtoto wa kiume..............?!
 
Mapandikizi ya CCM bado hayajaisha.....Medeye kaanza.....bado Masha, Msindai, Lembeli, Sumaye kisha unamalizia na Lowassa.
Kikubwa ni mchango wao ulisaidia vipi kuipaisha cdm kutoka wabunge 30 na kitu hadi 70 na kitu
 
Msimamo wa Prof lipumba juu ya ufisadi unajulikana sasa akirudi UKAWA itakuwepo na Lowasa akiwemo? Tusubiri tuone
 
CUF wajiandae kupungua/kupoteza idadi kubwa ya wabunge na madiwani mwaka 2020

Kwa hiyo unataka kusema UKAWA Imeisaidia zaidi CUF kuliko CHADEMA? Kama ndio so unataka kusema kwamba wingi wabunge wa CHADEMA haujatokana na Msukumo uliopatikana kutokana Muunganiko wa UKAWA bali ni kwa CHADEMA yenyewe?
Kama sio kwa nini usihitimishe kwa kusema wabunge wa upinzani watapungua?
 
Back
Top Bottom