Kama ningelikuwa Lowassa,Rostam au Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama ningelikuwa Lowassa,Rostam au Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Apr 25, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kama mimi ningelikuwa mmoja wa wale mapacha 3 wa UFISADI al-maarufu RACHEL ningelichukua uamuzi ambao CCM wasingesahau:
  Uamuzi huu ungelikuwa kama ifuatavyo: Kwanza tungelifanya kikao na kuweka mikakati ya namna ya kupangua hoja za CC na Mwenyekiti wetu Kiwete:

  Lowassa ndiye angelianza kuongea kuwa yeye amekuwa karibu sana na Kiwete tangu wakiwa Chuo Kikuu,namna walivyojiunga na TANU enzi hizo wakijulikana kama Boyz 2 Men.

  Jinsi walivyopanda ngazi kwenye nafasi mabalimbali za uongozi mpaka kwenye Uwaziri na kufikia Urais na u-PM. Lowassa angelielezea jinsi walivyochukua fomu za kugombea Urais wakisindikizana kwa mbwembwe. Namna walivyokubaliana kuwa Urais huu watapeana ZAMU kwa kuanzia Kiwete na baada ya awamu zake 2 Lowasa naye atatinga IKULU kwa mtindo uleule wa kupokezana vijiti.Jinsi walivyopanga na kuweka mkakati wa kuchota YALE MABILIONI YA EPA ili wayaiingize kwenye kampeni za Uchaguzi wa 2005 kwa Urais na Ubunge ili waweze kushinda kwa kishindo.

  Wa pili angelikuwa ni RA(Rostam Aziz) naye angelieleza jinsi yeye akiwa Mweka Hazina wa Chama cha Magamba alivyoweka mikakati mizuri ya kuzichota zile Bilioni za EPA kwa kupitia zile Kampuni bandia au hewa za Kagoda,Deep Green,Meremeta n.k. Jinsi alivyokuwa akiitwa Ikulu mara kwa mara na Mkapa ili kuweka mipango mizuri ya kufanikisha mbinu hizo za Chama. Jinsi alivyojitolea kwa pesa zake mwenyewe mfukoni ili kumwezesha Kiwete aingie madarakani na namna Kiwete atakavyomsaidia kupata tender kama za Richmond ili waendelee kukusanya tena Mabilioni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 na hatimaye Funga Kazi ya 2015 kwa ajili ya Kampeni za kufa mtu maarufu kama: LOWASSA FOR PRESIDENCY,2015!

  Na wa mwisho kujieleza angelikuwa Mzee wa Vijisenti- AC(Andrew Chenge). Chenge yeye angelianza kueleza namna alivyojitahidi kupindisha sheria na mikataba mbalimbali ili kuiwezesha CCM itawale kiulaini. Kwa miaka yote 10 akiwa na Mzee Nkapa walivyocheza na Marehemu Balali Gavana wa Benki Kuu kufanikisha uchotaji wa Mabilino ya EPA ili tu CCM ifanikiwe na hasa wakimtengenea njia Kiwete!

  Baada ya maelezo ya kila mmoja basi tungelianza mikakati ya kuzuia mpango wa kutufukuza ndani ya Chama maana kinachofanyika ni uonevu kabisa. Haiwezekani kuwa sisi 3 peke yetu ndiyo tuonekana kuwa ni MAFISADI wakti mipango yote tulikuwa tukifanya pamoja na Mwenyekiti wetu Kiwete tukishirikiana na Rais mstaafu Mkapa. Haiwezekani sisi tuwe ndiyo kondoo wa sadaka. Kama ni UFISADI basi ni CCM yote na SERIKALI yake kwa maana ya Mwenyekiti wetu Kiwete,M/mwenyekiti Malecela,Makamba,Chiligati na CC iliyojiuzulu na kupewa ZAWADI YA MASHANGINGI.

  Sasa kama ni noma na iwe noma.Lazima CCM yote ijiuzulu kwa kuanzia M/KITI wake Kiwete,CC mpya na NEC yake yote. Maana viongozi wote wa CCM wakiwemo Mawaziri,Wabunge, wakiwemo makada kama Wakuu wa (W)/(M)wote waliingia kwa fedha ya EPA.

  Hapo tungeandika taarifa ya Kikao chetu na kumpelekea Kiwete pale Ikulu tukimtahadharisha kuwa hizo siku 90 alizotoa kwa sisi kujiondoa CCM basi ajue kuwa NDIYO KIFO CHA CCM. Tutamweleza Kiwete kuwa tunajua SIRI nyingi namna hata yeye alivyoshiriki katika kukwapua yale Mabilioni ya EPA. Tutamkumbusha kuwa hata yeye yuko kweny ile list of shame ya MFISADI 11. Haiwezekani sisi rafiki zake wa karibu kabisa atusaliti na kututosa kirahisi rahisi namna hii. Hiyo haiwezekani ni afadhali Chombo kizama baharini tufe wote na atakayeweza kuogelea ndiye atakaye-survive!

  Hii ni kwa nia njema na ya dhati kabisa kuwa sisi kama viongozi waandamizi wa Chama wenye uzoefu na tukiwa na mtaji wa wafuasi karibu robo 3 ya wana-CCM tukiondoka CCM itakufilia mbali. Tuko tayari kwenda kuanzisha Chama kingine chenye nguvu kuliko hata CCM.

  Wasalaaam,

  RACHEL.
   
 2. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kikwete kashawahi na anatafuta support ya wapiga kura!uwezo wa kuwapoteza anao!
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  sijui kama itafanya kazi,RA kishaanza kuhamishia vitega uchumi vyake nje
   
 4. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni ngumu sana kwa wao kuthubutu hayo kwa sababu zifuatavyo:_
  Kwa mujibu wa katiba iliyopo bado LOWASA,CHENGE,HATA ROSTAM hawana uwezo au mamlaka ya kumfanya chochote Rais ila wataisaidia nguvu ya umma kumuondoa mtu mzima kwenye kiti cha enzi na kumfanya arudi zake hukooo misogwa Bagamoyo.

  (a)Madhara yatakayo wapata watakapo amua sasa kuvuana nguo ni makubwa kuliko Kikwete
  ( b)Upo uwezekano mkubwa mwisho wao kua mbaya kuliko walivyoanza kuanzia mali zao hadi maisha yao.
  (c) Hata ikitokea wameunda Chama chao uwezekano wa kupata umaarufu hata wa kile chama cha muta mwega hawatafikia.
  Huo utakua ndio mwisho wao kwenye ulimwengu wa siasa.
   
 5. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  wakali wa kuchakachua tupeni mambo wengine bado tunathubiria ushauri kwa JK
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Criss,

  Aksante kwa mchango wako.
  Ila tu napenda nitofautiane nawewe. Kwamba eti Kikatiba hawana uwezo wa wa kumfanya kitu chochote Rais si kweli. Kumbuka haya mambo yanaenda kichama yaani ki-CCM.

  Kwa hiyo hawa jamaa watajipanga na kumkabili Kiwete kama Mwenyekiti wao wa Chama cha Majambazi au Magamba. Hawaendi kum-attack kama Rais wa nchi! Kwa hiyo kama wanachama wa CCM hiyo nafasi wanayo. Tumeambiwa watapewa barua na bila shaka watakuwa na nafasi ya kujitetea. Siamini katika udikteta kwa CCM wa kumhukumu mwanachama pasi ya kujitetea! Kumbuka hawa jamaa hawana KESI YOYOTE YA UFISADI MAHAKAMANI! Vipi uwatimue kwenye Chama? Mbona hawajawatimua kina Mramba, Yona na wengineo ambao ytayari wana kesi za UFISADI Mahakamani?

  These guys are still in the system. Bado ni Wabunge. Lowassa kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Usalama na Mambo ya Nje. Kwa hiyo hii swala huwezi kulichukulia lightly kiasi hicho.

  Kikwete hapa ameamua kulamba matapishi yake. Mpaka sasa watu wanahoji ilikuwaje mwaka jana kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010 personally alipita kwenye majimbo ya hawa jamaa akiomba KURA/KULA na bado akawashika mikono hawa jamaa na KUWANADI KUWA NI WATU SAFI hawana doa lolote. Na ndiyo maana leo wako Bungeni.

  Chenge al-maarufu Mzee wa vijisenti hana kesi. TAKUKURU walimsafisha kuwa hana hatia na baadaye Waingereza nao wakamwaga manyanga.

  Msemakweli atakuwa 90 days. Hapo ndiyo mbichi na mbivu za CCM zitakapojulikana.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hukumu ya jamaa imeshapitishwa na sasa ni hiarin yao kuitekeleza kwaustaarabu au kusubiri kufurushwa. Hawana uwezo wa kuhama na kuanzisha chama na ndiyo maana wanahaha kuhakikisha wanabaki kwa sababu umaarufu wao haumfikii hata Fahmi Dovutwa na chama chake. Tunazo habari kwamba sasa wanahaha kuwachochea wajumbe wa NEC wabadili maamuzi baada ya siku 90 lakini kwamwe hawatafanikiwa. Wanachochea kuvunjwa kwa muungano na kuwachonganisha viongozi wa dini as if ufisadi una dini au wakiiba wanagawana na waumini wenzao. Mbona wasiwe na ujasiri kama wa Mpendazoe?
   
Loading...