Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Wengi wetu wabunge wa upinzani tungeamua kuwa wana CCM , tungeshinda UBUNGE,ukigombea ubunge kwa kupitia ccm unasaidiwa na Polisi, mkuu wa wilaya , mkuu wa mkoa, na wakati mwingine usalama. Kwa ujumka system huwa inambeba mgombea wa ccm, kama swala ni ubunge tu! Ningeamua kufuata ccm, lakini kwa sababu l have a cause that lam fight for , nimeamua kukabiliana na magumu yote, kutoka chama tawala , polisi wanatukamata, kutupiga, kutubambika kesi,maji ya kuwasha, nk. kosa letu kuu moja, kutaka kujenga nchi yenye demokrasia na haki sawa kwa wote. ukiwa na upinzani dhaifu kamwe huwezi pata serikali makini, baada ya kumaliza kudhibiti upinzani , nina ukakika watafuata wanahabari , wanaharakati , na wengineo,. Wantzania tusikubali hali hii iendelee. Kujenga uchumi imara wa nchi ni pamoja na kupanua demokrasia
Chanzo : Mchungaji Peter Msigwa - Mbunge
Chanzo : Mchungaji Peter Msigwa - Mbunge