kama ndoa ni hivi mimi basi sioi

kama ndoa ni hivi mimi basi sioi

kidaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2013
Posts
2,999
Reaction score
2,582
poleni na mihangaiko ya siku na mimi katika pitapita zangu kwenye mihangaiko yangu nimekutana na hii habari nikaona ni vyema nipate ukweli juu ya hizi gharama za kuoa je ni kweli ndugu zangu.....
JAMANI KUOA SI JAMBO
DOGO,
UNATAKIWA UWE UMEJIANDAA:

Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume naunataka kuoa, jiandae kwa mambohaya: (hizi ni gharama utakazoingia nje ya michango ya harusi)

1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume keo
atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindiki za, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku
hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.

5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!

11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…" 400,000!

12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende….." 700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale ashangazi watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Yafanye hayo hapo juu kwenye namba

15 kwa wazazi wako. 150,000

17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele 10,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000
 
Mimi kwa Mkuu wa Wilaya, shilingi 22,000 au 50,000 tu! Asante serikali kwa kutuona sisi tusiokuwa na mpango na hizo habari
 
Inaweza kuwa kweli hizo gharama zote au la kutegemea na kabila unalooa na ushirikiano wa familia yenu katika kusaidiana, na jinsi gani unataka vitu clasic.

Ila gharama yoyote utakayoingia, ukishakaa kwenye ndoa na kama huyo mke ni chaguo lako, hutakumbuka hata centi tano, hasa Mungu akiwabariki na beautful girl or handsome boy kwenye ndoa yenu, hautokaa ujute,

Kumbuka, Mungu mwenyewe akasema 'si vema mtu (mwanamume) huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Kuoa / olewa raha, no comparison.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Na kwa bahati mbaya ndoa zenyewe baada ya gharama zote hizo, mwishoni hazidumu
 
Uchambuzi mzuri sana, lakini kama utaki makuu, mengi unaweze kuyapotezea!
Tatizo watanzania hatuna malengo ya baadae na dnio maana ndoa hazidumu.
 
Opt for ndoa ya kimila, vinginevyo chondechonde usitusababishie watoto wa mitaani
 
Hahahahaaaaa! dah haya majanga,hiyo ndoa imekuwa gharama mno now days sijui kama tutafika
 
Inaweza kuwa kweli hizo gharama zote au la kutegemea na kabila unalooa na ushirikiano wa familia yenu katika kusaidiana, na jinsi gani unataka vitu clasic.

Ila gharama yoyote utakayoingia, ukishakaa kwenye ndoa na kama huyo mke ni chaguo lako, hutakumbuka hata centi tano, hasa Mungu akiwabariki na beautful girl or handsome boy kwenye ndoa yenu, hautokaa ujute,

Kumbuka, Mungu mwenyewe akasema 'si vema mtu (mwanamume) huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Kuoa / olewa raha, no comparison.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
Hapo unawaza matokeo tu haujawaza hiyo hela anaitoa wapi,na umeshaambiwa kamati haihusiki mambo mengine,vip ikitokea hamjapata huyo handsome au beatul girl utashindwa kukumbuka machungu yote hayo? hapo lazima bisiness ziyumbe kwnza
 
Lolest, hizo gharama ni nyingi mno...
Naamini katika hayo uliyoainisha, yapo mengi sana ya kupotezea, hasa kama hutotaka makuu. Kma wewe ni kijana unayependa kuonekana unazo, kweli zitakutoka.

All in all, ukitaka kuoa lazima ujiandae, otherwise utaota mvi ndani ya miezi mitatu, lol.
 
Kina haja us kwenda benki na proposal ya mkopo ukiainisha gharama zote zilizotajwa hapo juu Ms ukaongezea na emergency kama 1m hivi usije umbuka
 
Inaweza kuwa kweli hizo gharama zote au la kutegemea na kabila unalooa na ushirikiano wa familia yenu katika kusaidiana, na jinsi gani unataka vitu clasic.

Ila gharama yoyote utakayoingia, ukishakaa kwenye ndoa na kama huyo mke ni chaguo lako, hutakumbuka hata centi tano, hasa Mungu akiwabariki na beautful girl or handsome boy kwenye ndoa yenu, hautokaa ujute,

Kumbuka, Mungu mwenyewe akasema 'si vema mtu (mwanamume) huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Kuoa / olewa raha, no comparison.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums

Watu wengi sana wanakuza haya mambo nenda wilayani kafunge ndoa.Pia kuna madhehebu yanafunga ndoa hata mkiwa wanne tu yaani wewe na wasimamizi wako.Mnaweza kufunga siku yeyote hata asubuhi ikimaliza unaenda kazini.Inategemea unavyoamua wewe mhusika na mpendwa wako kama anapenda kuuza sura yatakukuta!!kwa ujumla sioni umuhimu wa sherehe ya harusi zaidi kuharibu muda na pesa ambazo Mungu ametupa kufanya mambo ya muhimu.Card ya harusi kwa sasa ni laki,si bora nitoke na familia yangu tukafurahi pamoja kuliko harusi ambazo hata watoto hawaruhusiwi.
 
hadi kichwa kiliuma jamani kumbe tusione misafara barabarani na honi piiii piii ehhh piii piii eh kumbe watu wanaumia na gharama
 
Hata kama unazo au huna kitu simple ni bora kuliko kitu complicated
 
Hiyo gharama mbona ni ndogo sana, sema watz wengi ni wavivu hawa jishughulishi, biashara yake ikifikia tu-Tshs. say 8bn/- anaridhika na kubweteka.
 
Tatizo la tz ndoa imekua maonyesho fanya yaliyo ndani ya uwezo wako,,,, kama vp unafunga ya serikali!!!
Na baadhi ya kina dada hawaangalii bajeti ya mwenzie kinacho mata,ni aonekane kafunga ndoa ya gharama kubwa.
 
Back
Top Bottom