Kama Nchi Tunataka AFCON '27 Isiwe Aibu? Ondoa CCM '25 Vinginevyo ni Majuto

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,801
71,226
Mchezo wa mpira wa miguu ni jambo kubwa sana na wenye kujua limewapandisha kiuchumi, kiwatambulisha duniani na hata kuleta amani kwenye vita.

Tumeona wote jinsi taifa la Ivory Coast lilivyoandaa kwa mafanikio na kupendeza sana AFCON 2023 wakati wao ni taifa dogo kulinganisha na Tanzania.

Sisi tumechaguliwa kuandaa kwa pamoja na nchi zingine za East Africa, lakini kila ukiangalia utayari wetu na jinsi tunavyokuwa na mambo ya kienyeji kutokana na uwezo mdogo wa maarifa wa serikali hii ya CCM ni wazi tunaenda kukumbana na AIBU KUBWA pengine tokea mashindano hayo yaanzishwe.

Kwa kushindwa huku kwenye umeme,maji, miundombinu ya usafiri na mawasiliano na coordination kwa ujumla TUSIPOIONDOA CCM madarakani 2025 na kuweka wenye ubunifu basi kijacho ni AIBU ambayo tunaosafiri nje ya nchi hii tutakana utaifa wetu tukiulizwa.

Unajiuliza mbona hawa Ivory Coast tumewazidi kwa mengi lakini tunashindwa na wao wenye raslimali chache na kuna kipindi vita viliwaathiri?

Tuwatoe CCM na kama mnawapenda kwa kulishwa limbwata basi 2030 tuone kama hamu nao bado mnayo warudisheni.

Screenshot_20240129-182127_Chrome.jpg

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2887242

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
huu mchanganyo ni wa mapochopocho au chombeza la michezo, siasa, uchumi, vyama vya siasa na uchaguzi mkuu 2025? :D
 
Huyu mama asiye na plan zozote atatuondolea aibu kweli?

Yeye anadhani kutoa milioni 10 kwa kila goli la Simba na Yanga ndiyo kuandaa wachezaji. Aibu naona mm kwa kuwa na kiongozi kama huyu.

Angalia hata waliosindikiza timu huko Ivory coast, ni akina Babalevo na Mwijaku. Wakati wenzetu timu inasindikizwa na waliokuwa wachezaji maarufu toka nchini mwao.

Taifa la kijuha sana hili.
 
Konyagi kitu hatari sana kuinywa wakati wa jua kali, kwa hiyo ikiingia chadema mtakuwa na timu ya ushindi ya kuchukuwa kombe 😁😁
Ujinga mbaya Sana.
"Wingi wa wananchi siyo kigezo kwamba lazima uwe na timu ya ushindi"
Ushindi ni kujipanga na kuwa na malengo mahsusi, vision ya mbali ya kimichezo!
 
Kwani nyumbu wanafikiria basi? Labda kama wanafikiri timu ya taifa itaundwa na viti maalum wanavyoteua wao.
 
Konyagi kitu hatari sana kuinywa wakati wa jua kali, kwa hiyo ikiingia chadema mtakuwa na timu ya ushindi ya kuchukuwa kombe
Ujinga mbaya Sana.
"Wingi wa wananchi siyo kigezo kwamba lazima uwe na timu ya ushindi"
Ushindi ni kujipanga na kuwa na malengo mahsusi, vision ya mbali ya kimichezo!
Ona akili za kiCCM hizi, hatuzungumzii kushinda taji hapa! Sisi tunazungumzia maandalizi, uendeshaji hadi kufanikisha mkusanyiko huo kama nchi zingine zilivyofanikisha ikiwemo hii Ivory Coast.
Akili zenu ndio za hivyo, ona aibu inaanzia hata kwenye thread JF!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ona akili za kiCCM hizi, hatuzungumzii kushinda taji hapa! Sisi tunazungumzia maandalizi, uendeshaji hadi kufanikisha mkusanyiko huo kama nchi zingine zilivyofanikisha ikiwemo hii Ivory Coast.
Akili zenu ndio za hivyo, ona aibu inaanzia hata kwenye thread JF!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Acha laghai zako wewe, unapindisha lugha, mtazamo wako ni hadaa sasa umeupindua
 
Back
Top Bottom