Anne Kilango alipewa nishani ya heshima ya Martin Luther King na serikali ya Marekani kwa michango yake ya kuboresha utawala bora hapa nchini...............na mara tu alipoipata hiyo nishani serikali ya CCM ilimpongeza kwa kuliweka taifa letu kwenye dira ya dunia.............na hivyo kuheshimika.......
Sasa ulipokuja uteuzi wa uspika kupitia CCM nilitegemea jina lake lingelipitishwa hususani ukizingatia ya kuwa kipaumbele cha CC kilikuwa ni kumtema Spika anayemaliza muda wake Mheshimiwa Samwel Sitta ambaye JK na top cream ya CCM ilimweka kiporo kwa muda mrefu kutokana na kuruhusu mijadala mizito ya kupambana na ufisadi hapa nchini........Kumbuka Sitta alilalamikia matokeo ya ubunge jimboni kwake yalicheleweshwa mno ikiiashiria ya kuwa kulikuwa na mchezo mchadfu ukinukia dhidi yake..................Ndani ya CC wapo wanaomlaumu Sitta kuwa ndiye mwanzilishi wa CCJ..............na sasa CC wamepata ahueni ya malipizi.........................
Hoja ya CC kuwa hii ni zamu ya wanawake kuukwaa Uspika ni danganya toto kama ilivyokuwa kwa UVCCM katika nafasi ya uenyekiti................JKna wenzie walipoona wana mtu wao kule Zanzibar aitwaye Masauni na wakielewa vijana hawatamchaguz kwa sababu hauziki wakaamua kuua demokrasia ndani ya UVCCN kwa kuwaondoa wabara kwa kile JK alikiita walikuwa wana vurugu..........vurugu zenyewe ni za Nape Nnauye ambaye kwanza umri ulikuwa unampiga stop asishiriki...............
Sasa huyu Masauni alipita na kuwa Mwenyekiti wa UVCCM lakini kama tulivyokuja kujionea wenyewe CC iliadhirika mbele ya dunia yote kutokana na kumpitisha mtu ambaye alikuwa anavurugu zaidi ya wale wa bara ambao hawakuwa wameghushi umri wa kuzaliwa....................
Baya zaidi kwa CC katika wale wagombea alikuwepo msichana mdogo kutoka bara lakini naye aliondolewa kwenye kinyang'anyiro ikithibitika wazi CC haina ukereketwa na masuala ya akinamama bali inapotokea mwananamama huyo ni kipenzi chao..........atakayelinda masilahi yao basi visingizio hutafutwa kumwinua kwa hoja babaishi za "Gender issues".......
Ukiangalia majina ambayo CC wameyapendekeza kwa wabunge tayari yaonyesha ya kuwa lengo ni Anna Makinda awe Spika na Kate Kamba Naibu wake...............kwa hiyo wabunge wa CCM wakikubaliana na tabia hiyo ya mwaka arobaini na saba kuchaguliwa viongozi na CC basi tutafahamu kwa undani maadui zetu kwenye vita dhidi ya ufisadi ni akina nani...........................
CC ya CCM imejiumbua yenyewe kwa kumkwepa mpiganaji wa vita vya ufisadi Mheshimiwa Anne Kilango na hili latuondolea wasiwasi kuwa lengo hapa siyo kuwainua akinamama bali kuwatumia akjnamama hao kama kivuli cha kufunika uozo wa jinsi serikali ya CCM inavyoendeshwa........................