Kama lengo ni mwanamke aukwae Uspika, Je Anne Kilango kawakosea nini CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama lengo ni mwanamke aukwae Uspika, Je Anne Kilango kawakosea nini CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 10, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Anne Kilango alipewa nishani ya heshima ya Martin Luther King na serikali ya Marekani kwa michango yake ya kuboresha utawala bora hapa nchini...............na mara tu alipoipata hiyo nishani serikali ya CCM ilimpongeza kwa kuliweka taifa letu kwenye dira ya dunia.............na hivyo kuheshimika.......

  Sasa ulipokuja uteuzi wa uspika kupitia CCM nilitegemea jina lake lingelipitishwa hususani ukizingatia ya kuwa kipaumbele cha CC kilikuwa ni kumtema Spika anayemaliza muda wake Mheshimiwa Samwel Sitta ambaye JK na top cream ya CCM ilimweka kiporo kwa muda mrefu kutokana na kuruhusu mijadala mizito ya kupambana na ufisadi hapa nchini........Kumbuka Sitta alilalamikia matokeo ya ubunge jimboni kwake yalicheleweshwa mno ikiiashiria ya kuwa kulikuwa na mchezo mchadfu ukinukia dhidi yake..................Ndani ya CC wapo wanaomlaumu Sitta kuwa ndiye mwanzilishi wa CCJ..............na sasa CC wamepata ahueni ya malipizi.........................

  Hoja ya CC kuwa hii ni zamu ya wanawake kuukwaa Uspika ni danganya toto kama ilivyokuwa kwa UVCCM katika nafasi ya uenyekiti................JKna wenzie walipoona wana mtu wao kule Zanzibar aitwaye Masauni na wakielewa vijana hawatamchaguz kwa sababu hauziki wakaamua kuua demokrasia ndani ya UVCCN kwa kuwaondoa wabara kwa kile JK alikiita walikuwa wana vurugu..........vurugu zenyewe ni za Nape Nnauye ambaye kwanza umri ulikuwa unampiga stop asishiriki...............

  Sasa huyu Masauni alipita na kuwa Mwenyekiti wa UVCCM lakini kama tulivyokuja kujionea wenyewe CC iliadhirika mbele ya dunia yote kutokana na kumpitisha mtu ambaye alikuwa anavurugu zaidi ya wale wa bara ambao hawakuwa wameghushi umri wa kuzaliwa....................

  Baya zaidi kwa CC katika wale wagombea alikuwepo msichana mdogo kutoka bara lakini naye aliondolewa kwenye kinyang'anyiro ikithibitika wazi CC haina ukereketwa na masuala ya akinamama bali inapotokea mwananamama huyo ni kipenzi chao..........atakayelinda masilahi yao basi visingizio hutafutwa kumwinua kwa hoja babaishi za "Gender issues".......

  Ukiangalia majina ambayo CC wameyapendekeza kwa wabunge tayari yaonyesha ya kuwa lengo ni Anna Makinda awe Spika na Kate Kamba Naibu wake...............kwa hiyo wabunge wa CCM wakikubaliana na tabia hiyo ya mwaka arobaini na saba kuchaguliwa viongozi na CC basi tutafahamu kwa undani maadui zetu kwenye vita dhidi ya ufisadi ni akina nani...........................

  CC ya CCM imejiumbua yenyewe kwa kumkwepa mpiganaji wa vita vya ufisadi Mheshimiwa Anne Kilango na hili latuondolea wasiwasi kuwa lengo hapa siyo kuwainua akinamama bali kuwatumia akjnamama hao kama kivuli cha kufunika uozo wa jinsi serikali ya CCM inavyoendeshwa........................
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Wazee wetu (tanu+asp) vision yao ilikuwa uhuru, hawakuwa na dira zaidi ya hapo.
  ndiyo maana milipuko ya akili mbovu tunaishuhudia kwa kiwango cha kupitiliza siku hizi.
  bado vichwani mwao wanalo jibu la Mwalimu J.K.Nyerere alipoulizwa mtajitawalaje huku hamna wasomi, alipojibu,(Tunataka uhuru wetu!!).
  Naamini hata sasa wakiulizwa (ccm) mnataka kufanya nini na uhuru mkiupata/mlioupata, jibu ni simple tunataka ku(ji)tawala!!!!!!
  wanagangamala kwa kila njia kututawala, hakuna zaidi ya kutawala, akili zao-kutawala.
  kutawala, kutawala
  -kutawala-kutawalatutawala-tutawala-tutawala-tutawala
  rebel.
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hawana lolote la kumpa fursa mwanamke hapo wanaogopa kivuli chao wakiona vichwa vya wapinzani vilivyoingia bungeni wanakosa amani kabisa wako radhi kujidhalilisha kwa kila hali,wanamageuzi wabunge wa CCM wangekuwa na akili wangeamua kuchukua chama chao full stop badala ya kuachia kiife mikononi mwa KIKWETE,kwa saabu udikteta wa Anna Makinda au Kate Kamba wanayemtaka utafanya bungeni pasikalike na shughuli zote za serikali hazitaenda uchumi utashuka makali yatazidi nakubaliana aliyesema KIKWETE ni janga la kitaifa
   
 4. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #4
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hatima ya TZ iko mikononi mwetu wote. Hili dudu linloitwa ccm lilishakufa siku walipomzika baba wa taifa. Unapooongelea dudu hili nasikia kichefu... Ni lazima tuchukue hatua ngumu na maamuzi magumu tuikomboee nchi yetu kutoka kwa majambazi wsio na huruma hata chembe na WTZ. Mimi nimeanza kuyafundisha mawe juu ya udhalimu ulioko TZ na kma mtashindwa kuchukua hata mawe yatasema niliyoyafundisha. Tuamke we dont have time 2 waste! Let us die for TZ na sio vyama:nono:
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Hoja zote hapo juu nimeziafiki....................ninawashukuru kwa michango mizuri...........................
   
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwani Kilango naye alichukua fomu ya kuuomba? If you can't ask you can't be given
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kama ni gender wangemhamasisha hata Tibaijuka kugombea.
  them afraid haoooo
  weziiiiiiiii haooooooooooooooooooo
   
 8. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 875
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  ..sidhani km muda na mazingira tuliyomo bado yanaturuhusu kufanya maamuzi muhimu ya kitaifa kwa kufocus mambo ya jenda!kama ni hivyo kwa nn hawakusema presidential candidate this time awe mwanamke, ili baada ya kukosekana hoja yao waihamishie kwenye uspika?bt km hilo lilikuwa kichwani mwao ya nini kuruhusu wanaume wachukue fomu za uspika?
  Watz we hv to knw our true enemy now!
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hata yule mama wa Ukerewe (Beijing) naye angeweza kuwa spika mzuri kwa uzoefu wake wa ndani na nje ya nchi
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  JF imethibitisha ya kuwa aliomba.........lakini akakandamizwa kimyakimya tu...
   
Loading...