Kama kweli Rais Magufuli ni wa wanyonge, basi angeanza na waliozika kilimo kwanza

JAH CITY

Member
May 24, 2016
40
125
KAMA KWELI RAIS MAGUFULI NI WAWANYONGE, BASI ANGEANZA NA WALIO ZIKA KILIMO KWANZA.

Sitatumia muda mwing kuelezea mawazo yangu.
Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali hapa nchi, 75% ya watanzania ni wakulima na weingi wana ajira zisizo rasmi.

Ukweli ni kwamba, sera ya kilimo kwanza ilikuwa sera pekee ya msingi ya kumkomboa mtanzania mnyonge na masikini. Vijana wengi walikuwa hawana ajira walikuwa tayari wamekusanyana kwenye makundi ili kufanya shughuri za kilimo kama sehemu ya kukuza pato lao.

Kilimo kwanza kimekufa, hakuna taarifa au reporti yenye majibu mazuri juu ya maswali yanayouliza mafanikio ya sera hii. Pesa nyingi zilitafunwa, pembejeo ziliibiwa na wanachi kupewa pembejeo feki.

Serikali hii ya awamu ya tano imejipambanua kusimamia masilahi ya wanyonge, lakini napata shida sana kuamini. Kwani ilipaswa kufufua kilimo kwanza, kuwachukulia hatua wale wote walio iua sera ya kilimo kwanza.

Pia hakuna ukuaji wa viwanda uliotokea hapa dunia bila ya kuwa na mapinduzi ya kilimo. LABDA TANZANIA TUWE WA KWANZA, JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI. Viwanda vinahitaji raw materials kutoka shambani, wakati huo huo tumeua mashamb makubwa na madogo tunayapuuza.

ILI NIAMAINI KUWA SERIKALI NI YA WANYONGE, BASI IHAKIKISHE INAENDELEZA SERA YA KILIMO KWA UFANISI NA KUWACHUKULIA HATUA WOTE WALIO HUSIKA KUIA.

ASANTE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom