Kama kweli My umeruhusu wimbo wa Nay,ruhusu na "am sorry JK" ya Nikki mbishi

Ahmad Mtunda

Member
Mar 15, 2014
37
20
Habari wanajamvi

Ukiusikiliza wimbo wa Nikki Mbishi unaoitwa "am sorry JK" ambao BASATA waliufungia na kumpa onyo Kali Nikki Mbishi na ukiusikiliza wimbo wa "wapo" wa Msanii Ney wa Mitego ambao pia BASATA wameufungia(ila utapigwa kwa idhini ya Mkulu) utajifunza kitu.

Pamoja na maudhui ya nyimbo hizo kufanana kwa zaidi ya 60%,tofauti yake ni kidogo tu kwamba huyu mwingine (Ney ) ameimba vitu na hasa current issues ambapo on other side anazungumzia suala la utawala uliopo na anazungumzia pia uongozi uliopita wa Jakaya kwamba kuna watu wanamkumbuka kwa uongozi wake.

Kwa upande wa Nikki Mbishi, yeye aliimba na kusifu uongozi wa JK kwa kulinganisha hali ya maisha ilivyo hivi sasa na ile ya kipindi cha Jakaya na anaonesha kujutia chini ya uongozi huu wa sasa ukilinganisha na ule wa JK.

Nikki Mbishi pia anaeleza namna ambavyo alikuwa anamwona JK kama kiongozi Mpole asiye na maamuzi lakini kumbe alikuwa sahihi kwenye baadhi ya mambo ambayo Nikki aliona kama JK hafanyi vile inavyotakiwa na hivyo msanii anaamua kumuomba msamaha JK kwa kumhukumu sivyo.

Wote ni wasanii na tofauti ni kwamba huyu mmoja(Ney) kaimba ujumbe wa moja kwa moja hasa mambo yalivyo na yanavyokwenda na huyu mwingine (Nikki) aliimba mambo yalivyo na yanavyokwenda ila kwa kuangalia madhaifu ya awamu hii ya tano na ile ya nne.

Nikuombe mheshimiwa uruhusu na wimbo wa Nikki Mbishi unaoitwa "am sorry JK" Kama kweli umeruhusu aina hizi za nyimbo zenye ukweli wa moja kwa moja ambayo kweli ndio muziki wa hiphop ambao moja ya nguzo zake ni "ukweli".
 
Tatizo hujaelewa mzee baba wikii hii anapambana kufa na kupona kuizima issue ya bashite na ya kumtumbua nape

Mkuu anajaribu kwa njia zote kuwa kwenye headlines ili mambo mengine ya msingi yasahaulike

Kwa mfano yake ya kuzuia makontea bandarini na hii ya leo ya nay imekuwa ndio headline na habari ya bashite tayari imeshaanza kupotea mdogo.mdogo

Inshort magu anajua kucheza na akili za watu
 
Kuruhusiwa kwa wimbo wa wapo ni kiashiria kwamba rais ameota ngozi ngumu na sasa hivi hababaishwi na maneno. Kwamba rais amekomaa na amejidhatiti kazini zaidi kuliko kusikiliza umbea na kuathiriwa nao.
Kama ni hivyo namshauri pia aruhusu mikutano ya kisiasa ili watu wapate pa kutapikia nyongo zao ili awe ni rais anayeongoza kidemokrasia.
 
Msinipangie, mimi ndo naamua vitu gani viwepo kwenye nyimbo.
 
Tatizo hujaelewa mzee baba wikii hii anapambana kufa na kupona kuizima issue ya bashite na ya kumtumbua nape

Mkuu anajaribu kwa njia zote kuwa kwenye headlines ili mambo mengine ya msingi yasahaulike

Kwa mfano yake ya kuzuia makontea bandarini na hii ya leo ya nay imekuwa ndio headline na habari ya bashite tayari imeshaanza kupotea mdogo.mdogo

Inshort magu anajua kucheza na akili za watu
hlyo n kwel kabisa mkuu au pia yaweza ikawa ni mtego kwa Nay ili ayaropoke majina vizuri ili ushahidi ukamilike
 
Back
Top Bottom