Kama kila kitu tutategemea kuhabarishwa................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kila kitu tutategemea kuhabarishwa................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Mar 27, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Tumekwishaa!
  Lazima tujue "kuchanganya na za kwetu..." waandishi habari na waandika makala wengi Tanzania... wengi wanaandika vitu kwa utashi wao na si kuzingatia hali halisi. Wapo baadhi wanaoona wamejaaliwa kuteka hisia za watu na wanaitumia nafasi hiyo kuwayumbisha watanzania ambao mpaka leo hii hawajajitambua. na ndio maana kila mdundo unaopita Watanzania wanakwenda nao kwa sababu ya media!Imani ya watanzania kwa vyombo vya habari imevuka mpaka ya akili za watanzania wengi...
  Leo mtanzania hataki kufikiria kinyume na chombo cha habari kilivyotangaza!
  Hebu fikiria vyombo vya habari vitatu vinatoa taarifa moja inaotofautiana!! kwa mfano moja itasema ajali yajeruhi watatu na kuua mmoja! nyingne ikisema Ajali yaua wawili na kujeruhi wanne! na hata habari zenyewe ukizisoma unaona wazi zinatofautiana!! na hii inawapelekea kla mmoja kuamini vile alivyosoma! hakuna anaehakiki ukweli!

  Hizo ndizo media zinazoaminika Tanzana! ukitoka hapo njoo wa "WASANII WETU" hapo namaanisha WANASIASA.. wengi wetu tumejenga imani kwao lakini nao pia ni kama waandishi wetu wa habari HAWATOFAUTIANI!

  Na hao ndio tunaowategemea WATUVUSHE!hawezekani kwa sababu wao wenyewe hawajui sisi tunataka kwenda wapi, hivy basi wanajaribu kulazimisha Watanzania waende kule wanakotaka wao (WANASIASA) na mwisho wa siku ndio maana malumbano ya wao kwa wao hayaishi kwenye vyama vyao! wapobaadhi yao wanaotaka Tanzania tuitakayo, na wapo wale wanaodhani CHAMA ndicho chenye haki ya kuchangua taifa liende wapi! Na wapo ambao wanataka ukuu na kugombea mkate waondani ya vyama..... wakifika hapa HAWAKUBALIANI!!

  Ndio maana SIASA za Tanzania na HARAKATI za Mageuzi ni kama HOMA ZA VIPINDI!

  UKIWAONA AMBAO HAWAPATANI, WATAZAME SANA HAO NDO WANAOPATANA!
  NA UKIONA WAMEKAA KIMYA, JUA KUNA MAKUBALIANO YAMEPITA...
  TUNAYO HIYARI, KUFANYA SIASA KWA MAANA YA SIASA AMA KUENDELEA NA SIASA MAIGIZO... UAMUZI NI WETU.
   
Loading...