Kama kawa; CCM na rushwa Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kawa; CCM na rushwa Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by OSOKONI, Feb 22, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CCM Arumeru waanza kuvurugana [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  SIKU moja baada ya wanachama wa CCM, Jimbo la Arumeru Mashariki kumpendekeza Sioi Sumari kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo ujao, baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilayani humo, wamepinga uteuzi huo wakidai kuwa uchaguzi uligubikwa na mizengwe.

  Juzi, mkutano Mkuu wa Jimbo hilo ulimchagua Sioi, mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361 akifuatiwa na William Sarakikya aliyepata kura 259, Elishilia Kaaya (176), Elirehema Kaaya (205), Anthony Musari (22) na Moses Urio (11).

  Lakini jana, baadhi ya wajumbe hao wa UVCCM wakiongozwa na Mjumbe wa Baraza la Umoja Mkoani wa Arusha, K
  ennedy Mpumilwa walidai kwamba uchaguzi huo ni batili kwa kuwa ulitawaliwa na misingi ya rushwa.

  Mpumilwa alidai kwamba uchaguzi huo ulijaa rushwa kila kona. Hata hivyo, hakuweka bayana kama walihongwa ili wamchague nani kati ya wagombea hao sita.

  Alidai kwamba kigogo mmoja wa UVCCM ngazi ya mkoa aliyeongozana na kada mmoja wa jumuiya hiyo, walikuwa ndani ya gari karibu na eneo la uchaguzi wakigawa rushwa kwa wajumbe.

  “Huu uchaguzi haufai kabisa baadhi ya wajumbe walihongwa. Ilikuwa ikitolewa 150,000 kwa kila mjumbe atakayekubali. Sasa hii CCM gani kama uteuzi tu hadi ufuate rushwa,” alidai Mpumilwa.

  Alisema kwa jinsi mchakato wa uchaguzi huo ulivyofanyika, ni dhahiri chama hicho kimeingia katika mpasuko mkubwa ambao kama usipoangaliwa kwa makini, unaweza kukiathiri.

  Mpumilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, alisema baadhi ya wanachama wa umoja huo wilayani humo wamechukizwa na mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi huo huku wengine wakitishia kuhamia upinzani wakati wowote.

  “Nakwambia vijana wamechukizwa kabisa na kilichofanyika katika mchakato wa uchaguzi, sasa wengine wametishia kwenda upinzani wakati wowote,” alieleza Mpumilwa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waendelee tu kuzozana kwani kifo chao ndio neema kwa watz.
   
 3. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pia angalia hizo namba kwani kura za Elishia Kaaya176 wakati namba nne Elirehema Kaaya206! Takukuru walionya lakini nashangaa kwanini hawajachukua hatua mpaka watu wengine watuambie wakati wao wapo. Inasikitisha kwa kweli.
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,181
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Takukuru isitegemewe ktk jambo kama hilo, haina uwezo. Hawana man power ya kutosha jimbo zima pale wana ccm watakapo sambaa kama nzige wakigawa rushwa, pia nao ni washika wa ccm.. Reff. Igunga, nilikuwepo.
   
 5. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,934
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  safi kabisa ndo tulikuwa tunataka mjichanganye tutawaangusha tu, hii meru siyo ya familia fulani
   
 6. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mod unganisheni ihi thread na ile ya easyfit
   
Loading...