Kama ingekuwa wewe ungefanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama ingekuwa wewe ungefanyaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Papa Mopao, Aug 25, 2010.

 1. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,354
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Wewe ni Baba/Mama/Kaka/Dada au Mlezi, una mtoto/watoto/wadogo zako mdogo/wadogo labda wa kuanzia miaka 4 na kuendelea hadi ukubwani huko tuseme miaka labda 25 hivi au kuendelea.

  Sasa mtoto/watoto/wadogo zako w/anapofanya kosa au w/amefanya kosa fulani, je katika kumrekebisha/kuwarekebisha w/asirudie kufanya kosa hilo katika siku za mbeleni.

  Utachukua hatua zipi?
  1. Kumuelimisha wanao/mwanao au mtoto/watoto/wadogo zako
  2. Kumchapa/kuwachapa viboko, ili w/asirudie kufanya kosa hilo.

  Na kama ulitumia eitha mojawapo wa hizo njia au zote mbili na mtoto/watoto/wadogo zako bado w/anaendelea kufanya kosa tena na tena na tena.

  Je, hapo wewe utafanyajeeeee?

  Tuzungumze kuhusu hilo jamani,nadhani na wengine wanaweza wakapata shule kupitia hii mada. Karibuni!
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hii siyo "if ... or ..." question. Kwa watoto njia zote mbili zinapaswa kutumika. Wale ambao wanasema mtoto kuchapwa ni ukatili watanisamehe. Kuna kuchapa kikatili na kuchapa kwa nia ya kurekebisha. Kama mtoto bado anarudia kosa ina maana somo bado hajalipata au wewe unamchapa bila kumweleza kwa nini unafanya hivyo. Jambo la kwanza ni kumwita mtoto ukamweleza kosa (bila jazba kubwa). Halafu ukamweleza madhara ya kosa lake. Baada ya hapo unampa nafasi ya kujitetea. Kama utetezi wake ni dhaifu unamweleza hukumu/adhabu atakayopata. Kwa mfano kama ni viboko unamweleza ni viboko vingapi utamchapa au adhabu nyingine. Na siku akiwa mtoto mzuri unaweza kumpa hata zawadi kuonyesha kuwa unafurahia kujirekebisha kwake. Hii inaitwa reward/sanction system. Na siyo lazima kila kosa liambatane na adhabu. Kumbuka mtoto bado anajifunza. Kuna mahali atakosea kwa sababu ya kukosa uzoefu au kutoelewa mambo.
   
 3. m

  madiya Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aaaah mi tatumia njia zote mbili mafundisho ya maadili mema kwa watoto na viboko vingi sana ikiwezekana vilevile tajitahidi niwalee kwenye mazingira ya kumjua Mungu naamini watakua na tabia njema sana vinginevyo kama hawaelewi hakika tasubiri wakue ulimwengu uchukue jukumu la kuwaweka sawa asante bwana
   
Loading...