Kama hujui kufa chungulia...urais?

Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
32
Points
135
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 32 135
na Chesi Mpilipili

KHERI ya Mwaka Mpya. Kwenye toleo la gazeti hili nambari 113, Desemba mwaka jana niliandika kuhusu sheria zetu za nchi zinavyoelekea kupindishwa ili kukidhi imani zetu za kiroho.

Nilitoa mfano wa mganga wa kienyeji mashuhuri jijini aliyekwenda Kanisa la Mchungaji na Mheshimiwa Mbunge Getrude Rwakatare na mfupa uliosemekana kuwa ni wa paja la binadamu na kutubu madhambi yake na kutangaza kumrudia Mungu. Nilieleza jinsi waumini wa kanisa hilo na kiongozi wao walivyoelekeza nguvu zao katika kumuombea na kuchoma moto tunguli za mganga huyo aliyedai kumrejea kwa Mungu bila sehemu ya nguvu hizo kumfikisha kwenye vyombo vya usalama kueleza jinsi alivyoupata mfupa huo.

Nilitahadharisha juu ya hatari ya kuruhusu mganga huyo na wengine wa aina yake, kuachwa hivi hivi kwa vile tu walikuwa wanadai kuwa wanamrudia Mungu bila kuchukuliwa hatua za kisheria za kutakiwa kutoa maelezo wanakopata viungo vya binadamu wenzao.

Nikashauri kuwa ni vema kazi ya kusamehe akaachiwa Mungu mwenyewe lakini sisi huku duniani sheria ziachwe zichukue mkondo wake ili kuzuia uwezekano wa hali hiyo kuonekana ni kitu cha kawaida.

Mwezi uliopita tumekwenda mbele zaidi katika hili pale mnajimu mashuhuri nchini na Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein, alipoita waandishi wa habari na kutangaza utabiri wake kwa mwaka 2010.

Alitabiri mambo mengi lakini kubwa ambalo limeelekea kushitua ni lile la kutabiri kifo cha ghafla kwa mwanachama yeyote wa CCM atakayetaka kusimama na Rais Jakaya Kikwete kuwania nafasi ya kugombea Urais kutoka chama hicho. Kwamba mpaka sasa mnajimu huyo anaendelea na shughuli zake kama kawaida na hakuna taarifa yoyote kuhusu yeye kutakiwa atoe ufafanuzi kuhusiana na kauli yake kunaonyesha jinsi tusivyokuwa makini na mambo yetu kama vile tunavyoweza kumuachia mtu aliyekuja kanisani kutubu na mfupa wa binadamu mwenzake bila kumtaka atoe maelezo alikoutoa.

Sina uhakika na ujasiri wa Watanzania. Nilicho na uhakika nacho ni kwamba wapo wengi tu wanaoamini katika unajimu na ushirikina na kwa maana hiyo kauli ya mnajimu huyo ina uwezekano mkubwa wa kupunguza kwa kiasi kikubwa ujasiri wa waliokuwa na ndoto za kujaribu kusimama na Mwenyekiti wa CCM kugombea kuteuliwa kuwa wagombea urais kupitia chama hicho.

Ni kauli ambayo inaweza pia ikasababisha uvunjifu wa amani iwapo kutatokea lolote, hata kwa bahati mbaya ya kweli, kwa jasiri asiyeogopa utabiri wa kifo wa mnajimu wetu na kusimama dhidi ya mwenyekiti wake kugombea nafasi hiyo.

Pengine utabiri wa mnajimu huyo ungeweza kupita tu na upepo na ukasahauliwa kama isingekuwa ni kauli iliyotolewa na Msemaji wa Ikulu ya kutaka Watanzania kuheshimu kauli ya mnajimu huyo kwa vile ana haki ya kutoa mawazo yake kama Mtanzania mwingine.

Yaani tunatakiwa kuheshimu kauli ya kwamba mwanachama yeyote wa CCM atakayejitokeza kusimama na Rais Kikwete kugombea nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu atapatwa na kifo cha ghafla?!

Nilidhani Ikulu ilipaswa kufanya moja kati ya mambo miwili makubwa dhidi ya kauli ya mnajimu huyo. Ama kunyamaza na kuiacha ipite kama ambavyo imenyamazia mambo mengine ambayo yameishalikumba Taifa na kuachia usahaulifu wa Watanzania ufanye kazi yake ama ingetoa kauli kali ya kuikemea vikali lakini si kututaka wananchi tuiheshimu!

Kwa hakika haingii akilini kutakiwa kuheshimu kauli inayotaka kuaminisha kwamba sasa tumefika mahali uongozi wa nchi yetu unapatikana kwa kusoma viganja na kuangalia mkao wa nyota angani.

Kwa nini tusione kwamba kauli ya mnajimu wetu si utabiri bali ni aina fulani ya onyo la chini chini kwa wale wanachama wote ambao wana mawazo ya kutumia haki yao ya msingi kusimama na mwenyekiti wao ili kugombea nafasi ya kuteuliwa na chama chao kuwa wagombea urais wa chama hicho?

Kwa nini tusikubali kwamba kwa ‘utabiri’ huu wa mnajimu hatakuwapo mwanachama ambaye atathubutu kujitokeza kusimama dhidi ya Mwenyekiti wake kuomba nafasi ya kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho kutokana na ukweli kwamba ujasiri wa aina hiyo uliondoka na akina Kinjeketile, Mkwawa na ‘Kibanga ampiga Mkoloni’?

Kilichoshangaza zaidi ni jinsi utabiri huo ulivyoelezwa kwa mapana na marefu na vyombo vyetu vya habari kama ambavyo imekuwa siku zote zinapokuja tabiri za kisiasa kutoka kwa mnajimu huyo.

Tunajionyesha jinsi tulivyo Taifa linaloshabikia unajimu na ushirikina. Hivi kweli utabiri wa mnajimu ni habari ya kuwa ukurasa wa mbele wa vyombo vyetu vyote vya habari na kutolewa tamko na msemaji wa Ikulu? Ni nini kilichofanya waandishi wa habari wamiminike kwa wingi kwenye nyumba ya mnajimu huyo kusikiliza utabiri wake badala ya kumtaka aende Maelezo akatolee maelezo yake huko kama watu wengine wanavyofanya na wao wangemfuata huko?

Ni kweli kwamba mzee wetu huyu mnajimu ambaye mimi binafsi nimeanza kusoma unajimu wake kuanzia mwaka 1967 kwenye gazeti la Baraza la Kenya amekuwa miongoni mwa viongozi wetu wa kitaifa ambao wanaweza kuitisha mikutano ya waandishi wa habari majumbani mwao kuongelea masuala mbali mbali yanayohusu Taifa na ikawa habari ya ukurasa wa mbele? Inawezekana. Lakini basi yawe haya ya kusema kuwa mtu atayejitokeza kutaka kusimama na Mwenyekiti wa chama cha CCM kugombea nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kutoka chama hicho atafikwa na kifo cha ghafla? Hii ndio kauli tunatakiwa na Ikulu tuiheshimu?

Haya ya kusema kuwa kifo cha kiongozi mwingine wa kuheshimika wa chama hicho ni dalili ya ushindi wa kishindo kwa Rais Kikwete kwenye uchaguzi ujao kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi uliopita? Kweli?

Je, CCM wenyewe wana kauli gani kuhusu utabiri wa Sheikh Yahya? Tuchukulie kwamba ‘sauti kubwa’ ya ukimya wao inamaanisha kukubaliana nao?

Tujiulize. Hivi kweli maneno haya yangetoka kinywani mwa kiongozi wa chama cha siasa cha Upinzani bado tungekuwa naye uraiani saa hizi badala ya kuwa mahali akitakiwa kufafanua vizuri kauli yake? Ni kweli tungetakiwa pia kuheshimu kauli yake kama tunavyotakiwa kuiheshimu kauli ya mnajimu wetu? Hivi hapa ndipo nchi yetu ilipofikishwa pa watu kutishwa kupitia unajimu ili wasijaribu kutumia haki yao ya msingi ya kutaka kuchaguliwa ili kuwaongoza Watanzania wenzao?

Wakati tukiingia mwaka 2010 tukiwa njiani kuelekea Uchaguzi Mkuu ni vizuri kauli za aina ya unajimu wa Sheikh Yahya Hussein kudhibitiwa mapema ili kuhakikisha kuwa haziwavurugi wananchi.

Bila kufanya hivyo kuna uwezekano kuwa kadri tutakavyokuwa tunasogelea Uchaguzi Mkuu wataibuka wanajimu wengine huko mikoani ambao ‘watatabiri’ kuwa watu watakaosimama dhidi ya wabunge wa majimbo fulani ambao ni vipenzi wa wanajimu hao watafikwa na vifo vya ghafla. Hamkani itakuwa si shwari tena.

Itakuwa vyema pia tabiri za wanajimu wetu zikapunguza kuwa na muelekeo wa kisiasa na badala yake zikabaki kwenye kututabiria mshindi wa mechi ya Yanga na Simba na nguo za rangi gani tuvae ili kusafisha nyota zetu kama ilivyokuwa siku zote. Ya kuchagua viongozi waachiwe wapiga kura wenyewe. Maana kila mtu akianza kutoa utabiri wa kuwaonya Watanzania kutogombea nafasi moja ama nyingine kwa vile kufanya hivyo kutawapotezea uhai wao, hakutakuwa na mabadiliko ya viongozi na tutajikuta bila kujua tukisimika ufalme. Ujasiri wetu uliondoka na akina Kinjeketile.

Source:
Raia Mwema

My take:
Nimefurahishwa sana na hii article and especially this quote
" Nilitahadharisha juu ya hatari ya kuruhusu mganga huyo na wengine wa aina yake, kuachwa hivi hivi kwa vile tu walikuwa wanadai kuwa wanamrudia Mungu bila kuchukuliwa hatua za kisheria za kutakiwa kutoa maelezo wanakopata viungo vya binadamu wenzao."

Inanikumbusha the pic below, long time ago. Mzee wangu aliposisitiza kwamba hii picha hapa chini ingekuwa Bongo, Polisi lazima wangekubana uwapeleke ulipopigia. Where are they these dayz????????

Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
38,994
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 38,994 280
good article
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,286
Likes
65
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,286 65 145
Source: Inanikumbusha the pic below, long time ago. Mzee wangu aliposisitiza kwamba hii picha hapa chini ingekuwa Bongo, Polisi lazima wangekubana uwapeleke ulipopigia. Where are they these dayz????????

........these days are GONE MEEN!
i mean that period is OVER AND OUT
 
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
32
Points
135
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 32 135
........these days are GONE MEEN!
i mean that period is OVER AND OUT
Yea but what about a man confessing to ber holding a human bone? Don't that trouble the authorities at least to know where did the femur or pelvis originated from?????????

Same thing like the other pic, Do you remember some bongo flava artist were arrested just by appearing in a video with army uniforms?
 
BabaDesi

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Messages
2,858
Likes
106
Points
160
BabaDesi

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2007
2,858 106 160

...Kweli, Ujasiri wa waTanzania uliondoka na babu zetu akina Kinjeketile na Milambo. Nitashangaa sana kama kuna mwanaCCM atasimama na Muungwana kugombea nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea uchaguzi wa Chama hicho!
 
Forum statistics

Threads 1,250,865
Members 481,514
Posts 29,748,717