Kama haya ndio mawazo ya Watanzania basi adui UJINGA ataendelea kuishi Tanzania milele.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Nilikuwa nafuatilia Majibu ya swali la kipima joto ITV lililohoji "Uhalali wa Polisi kuwazuia wanafunzi kufanya sherehe za mahali kwa madai ya kukosa kibali" nafikiri ilikua ni mifano ya CHASO wa UDOM na Kilimanjaro.

Mtu amajibu kwa kusema eti polisi walikua sahihi kwa sababu wanafunzi wanapaswa kufanya sherehe kwa kutoingiza siasa, mwingine anajibu kua hayakua mahafali bali ni mikutano wa kisiasa kwa sababu palipambwa na bendera za vyama,Mwingine anasema kua hayakua mahafali kwa sababu walialikwa viongozi wa kisiasa.

MASWALI KWENI WATANZANIA

Hivi tunaelewa maana ya CHASO? Tunatofaitishaje CHASO na siasa? Haya mahali ya namna hii yameanza leo? Yaani kwenye mahafali ya kuwaaga vijana wahitimu wanachama Chadema aalikwe Ole Sendeka au Philipi Mangula?tulitaka aalikwe Cardinal Pengo au Mufti Zuberi?Wangealikwa viongozi gani hasa maana yale yalikua ni mahafali ya CHASO? Tulitaka zitumike bendera za CCM au bendera ya Taifa kupamba ukumbi kwenye mahafali ya CHASO?

Hawa ni vijana wasomi wanaolelewa katika vyama vya siasa wakiwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu na ndio maana kuna matawi ya vyama vyote vya siasa ndani ya vyuo mbali mbali. Huwezi kutofautisha mahafali haya na maneno ya kisiasa kwa sababu wale vijana ni wafuasi wa vyama. Kina Nyerere, Kikwete, Pius Msekwa, Masaburi na wengine walilelewa ndani ya mashirikisho haya ya vyama vya siasa vyuoni sasa leo watu wanakurupuka tu kuzuia sherehe kama hizi kwa kukosa uelewa wa historia au ni makusudi tuu?

Waislamu waliopo vyuoni hua na shirikisho lao la wanafunzi ambalo huliita TAMSIYA, Wakristo wana TYCS nk! Hawa inapofikia mwisho wa kuhitimu mahafali huandaliwa ili kuwakumbuka na kuwaandalia nasaha njema pindi waingiapo mtaani. Hizi itikadi za kiimani hazina tofauti za zile za kisiasa ndio maana nao huona ni vema kuwaandalia sherehe wenzao wanaomaliza.

Inawezekana kabisa kabisa Magufuli hana mkono wake juu ya haya bali ni woga wa baadhi ya viongozi ndani ya serikali ili kutafuta sifa kutoka kwa kwake Rais, hawa ndio maadui namba moja wa Rais Magufuli! Wanafanya mambo ya ajabu kabisa wakifikiri Rais labda atawasifia.Yaani muda wote kuna viongozi baadhi serikalini wako kutetemeka wamejawa na hofu hawajui Mh Rais hua anapendezwa na kitu gani au anachukizwa na kitu gani.

Ni uhakika kuhusu hili jambo la mahafali Rais atailitolea ufafanuzi kwa maneno yake mwenyewe siku moja na ukweli utajulikana tu. Anaelewa kua kuna viongozi hawajui wajibu wao ila wapo wapo tu kwa hofu hofu hawajiamini wanashindwa kuamua na kupambanua mambo.

Kuanzia RPC, RC wa Dodoma na Kilimanjaro wajiulize ni upi utofauti wao na RPC na RC wa Dar es salaam na Iringa?Vinginevyo kuna tofauti za kiutendaji za watu hawa na kuna tatizo.
 
Mh! Sina hakika na nina mashaka makubwa sana juu ya nani aliye bariki haya yatendeke katika sura hii iliyopo sasa.
 
Mkuu ukitaka kulijua hili jiulize ni kwanini RCna RPC wa Dar na Iringa waliruhusu sherehe hizo lakini RC na RPC wa Kilimanjaro na Dodoma walizuia? Upinzani uliopo Dar utaufananisha na wa Dodoma? Hapa kuna madhaifu ya viongozi na sio Rais.
 
Kaka wala usihoji, tumefika hapa kwa sababu ya umbulula wa Watanzania na ccm kamwe haitatoa Elimu bora na kwa wote ili ujinga uendelee na wao waendelee kutawala. Kama kutafanyika utafiti nadhani Tz itakuwa ndo nchi ya kwanza kuwa na watu wenye uelewa mdogo
 
Back
Top Bottom