Kama hawa wakiwa Walimu wa Kiingereza nitaomba nifundishwe na huyu...

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Wote ni Watoto wa Wanasiasa Waandamizi kabisa nchini Tanzania na nimebahatika kwa umakini kabisa kusikia Viingereza vyao na kama ikitokea kati ya Mtoto wa Mzee Maghembe na Mtoto wa Mzee Masha wote wakafungua darasa la kufundisha Kiingereza nitaenda na Mtoto wa Mzee Masha.

Kiingereza cha Mtoto wa Maghembe ni cha mashauzi, sifa na kina chembe chembe ya dharau ILA Kiingereza cha Mtoto wa Masha ni cha nidhamu, umakini, unyenyekevu na kinachoashiria kuwa amelelewa kuwa na busara na uzalendo kwa nchi.

Kwako Lawrence Masha tafadhali fungua darasa la kutufundisha Kiingereza kwako nimekipenda, kimenyooka na ni cha Kimaendeleo zaidi tofauti cha mwenzako ( Mtoto wa Waziri Maghembe ) ambacho ni cha ' kimashauzi ' zaidi.
 
Back
Top Bottom