Kama haupo sawa katafute msaada

Hivi mtu asiye na emotion ndio huitwa( stone ) Jiwe ee hahahaha!

Mmewahi kuwa na prezida Jiwe (emotionless) kweli kweli!

Mimi Role model wangu ni JIWE aka Emotionless.

On a serious note ni utoto kujali kila hisia ya Mtu, bora kuelewa tu anachofeel na kusonga mbele ( empathy)..

Wanawake humuona mwanaume anaeonyesha Hisia zake as Weak, So nawashauri wanaume wote wawe kama Jiwe tuu ( emotionless)

Though nakubali emotions are sweet to feel them, they are Life.
 
Aiseee,, kumbe upo kwenye mission...

Karibu, jisikie uko nyumbani....hakuna linaloshindikana chini ya Jua.
Nijikute tu.

🤣🤣🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️
 
Exactly. You made the best points on your comment. The chaos is growing now days. Relationships are flooded by sick minded individuals who pretend to be okay.

This once nilikutana na spouse ambaye alibreak up kisa sikuweza msaidia kodi kwa wakati alipohitaji. Just imagine, mtu anapata hasira na sababu ya kubreak a healthy relationship sababu ya kukosa sapoti alipohitaji.

Na ni mtu ambaye alipokuwa na shida ndogo ndogo nimekuwa nikimsapoti its just my economic state and cash flows hazikuwa on point so i was kinda broke.

Fast-forward few years baadae she had an audacity ya kuappologize baada ya mimi kumsalimia. Ananiomba msamaha kwa kutokuwa mvumilivu wakati alipokuwa na shida halafu hapo hapo anatoa ushauri kuwa next time nisifanye nilichofanya kwa my next lover. Nilishiwa pozi sikutaka kumjibu kwa wakati ule maana nilihisi nitamtukana.

Then ilichukua kama siku tatu nikareply ule upuuzi aliandika pale. Nikamwambia so, mfano ukimuomba mama yako au baba yako kitu wakashindwa kukupatia, do you break up with them na kuwa disown kama wanafamilia wako?!

Akajibu kuwa wale ni wazazi wangu sasa nawaachaje wazazi wangu.

Nikamwambia nenda katafute therapy kwasababu wazazi wako hawajakuandaa kuishi na binadamu wengine if thats what umejifunza katika malezi waliyokupa. By the way Karma is headed your way say hi for me.

Akajibu, so unaniombea mabaya? Nikawambwa no, mimi sina uwezo wa kukuletea mabaya ila wewe kwa mwenendo wako huo unavutia mabaya yakufuate.

Nikaona mpuuzi m'moja tu huyu. Nikamkaushia hadi kesho namtazama tu.
 
Kwa hiyo twende kwa ma Psychologist?
Kama unajiona kabisa swaga zako kwenye mahusiano una mawenge mengi hebu nenda kaonane na therapist akupe msaada mahusiano sio sehemu ya maumivu tabia zetu ndio hutuletea maumivu na kuwaumiza wengine.
 
Elimu ya bure kabisa hii...
Wengi wetu tunahitaji matibabu...tatizo therapy sio utamaduni wetu...[emoji6][emoji854]
Kabisa. Therapy ni muhimu. Watu wengi wameharibika tokea tokea utotoni. Wanakuwa wanavaa vizuri, wananukia vizuri, wanatabasamu ila akianza kuishi na mtu ndipo inajulikana kuwa kichwani hayupo sawa.
 
Kimsingi mimi mtoto akija kunirepotia kuwa ndugu yake kamtendea jambo lisilo la haki kama kumnyima kitu au kumdhurumu au kumnyang'anya kitu huwa nakuwa mbogo sana na nitataka haki itendeke haraka sana.

Kwasababu hivyo vitu vikiachwa chuki za utotoni huwa zinamea nakuwa kubwa utu uzimani.

Nina baba mdogo wangu haivi na dada yake hadi sasa ni watu wazima. Shida ilianza utotoni ni kuwa shangazi alikuwa anaachiwa maagizo ya kuangalia nyumba na kusimamia wadogo zake kipindi cha utotoni.

Sasa akawa anatumia authority hiyo kibabe na kuwafanyika wadogo zake majukumu kibabe na kuwapelekesha na ilitokea wakagoma wazazi wakirudi yeye atachomea utambi na wadogo watachapwa.

Sasa wamekuwa watu wazima na yule mdogo amekuwa na pesa ni meneja wa Tanesco ngazi ya mkoa,dada yake mambo si mazuri anaishi maisha ya kawaida sana. Sasa ikitokea jambo halafu dada mtu akataka kutoa sauti mdogo wake anasusa na hataki mtu amwambie lolote anakuwa mbogo.

Basi sababu ya pesa inabidi asikilizwe basi litakwenda namna anataka hataki majadiriano.

Kuna kipindi baba yao alikuja mjini kupata vipimo, dada mtu bila kumshirikisha mdogo wake alipanga safari ya mzee wao ya kuja Dar. Mdogo mtu akajua akamind sana. Alipofika akampeleka Hospital bila kuzungumza nae walipofika hospital akapewa vipimo, balaa kwenye kulipia akamtumia ndugu kumpigia simu mdogo mtu kumjulisha. Alichofanya hakwenda hospital akakaa kimya hadi walimrudisha mzee wao home kwa dada mtu. Ndugu kumuuliza mdogo mtu akatoa ya moyoni, basi wakabidi kujishusha yeye atoe maagizo.

So akaja akamchukua mzee wake na dada yake wakaenda hadi muhimbili kuendelea na matibabu. Ameenda wamekaa kufanya vipimo walipomaliza dada mtu sijui alitoka nje kutafuta nini mdogo mtu akatekenya gari huyooo kaenda na baba yake nyumbani kwake akamuacha.

Dada mtu anatoka anakuta washasepa. Kupiga simu haipokelewi. Akarudi na daladala.

Kwahiyo chuki huwa zinamea ni vema sana kuwatendea haki watoto wakiwa wadogo ili akikua anakuwa hana kinyongo na ndugu yake.
 
Ubaya ni kwamba unaweza kuwa na tatizo na hujui kama una tatizo teh

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ni rahisi sana kujua kuwa una matatizo ya kitabia yanayotokana na makuzi yako ya utotoni maana tabia hazianzii kuharibikia ukubwani.


Mfano, leo hii mabinti na vijana wengi katika mahusiano unaweza kuwatambua kuwa si wazima kutokana na tabia zao.

Mfano. Binti kuomba sana pesa na kufosi kupewa mahitaji ambayo si stahiki yake maana si mke wa mtu ni ishara ya kutoka familia au maisha ya kukosa kipato sasa anataka kupata au kufidia alichokosa.

Kijana unakuta anapenda mwanamke wake achangie gharama za maisha hata kama yeye ana uwezo wa kufinance kila kitu. Hii ni dalili katoka katika familia ambayo ili mlea kutokuwa responsible kama kiongozi wa familia.

Au ana hasira hasira za haraka, kuna uwezekano mkubwa ni kuwa alikuwa hasikilizwi alipokuwa katika familia yake sasa namna ya kujenga hoja ni kwa kutumia ukali au sauti ya kufoka ili kuweza kusikilizwa.

Au unakutana na binti anadharau sana na hawezi kutii maelekezo ya mwanaume wake. Ukichunguza ni mama yake kamjenga na hiyo tabia kutokana na mahusiano mabaya na mume wake au ni binti aliona mama yake na baba wakiishi kwa kutokuheshimiana so na yeye anacopy hivyo hivyo.

So its better kupata therapy before mtu hajafika 30 years of age sababu ikifika hapo uwezo wa akili kurepair tabia unaanza kupungua kwa kasi sana. Ndio maana hatushauri mwanamke kuingia mahusiano serious above 25 hadi 30 sababu ni umri mbaya sana kwa mtu ambaye hajitambui kitabia. Akifika huo umri itabidi akubali kuishi alivyo maana hatoweza badilika kirahisi na akijaribu itamtesa sana kuadopt tabia mpya.

Kwa wanaume tabia huwa inatengenezwa mapema zaidi. Ukikosea ndio basi hata akifika 30 tayari ni umri anasimama mwenyewe inakuwa tayari kishachagua tabia za kuishi nazo.
 
Na huu ndio mtihani mkubwa kuliko ambao mleta uzi hajazungumzia...

InFact Kujijua una tatizo huwa ni ngumu sana kuliko hata kulitatua tatizo lenyewe....

Asante
Ni rahisi. Changamoto ninayoiona ni kukosa elimu juu ya tabia zipi mbaya na zipi ni normal. Behavior disorder zipo nyingi. Labda kusaidia nitafanya kuandika uzi kuelezea kila moja ili tuweze kuzielewa kirahisi na kuweza kujua namna ya kufanya self diagnosis.
 
Kwahyo wanaosomesha wanajipendekeza tu...

Au fulfillment unayozungumzia ni emotional based only.!?
Nadhani kamaanisha upande wa vile vitu vya kihisia mfano kupendwa. Kuna mtu hayazoea upendo wewe ukimpenda na kumjali anaona sio kitu muhimu.

Utamletea zawadi anapokea na kusema asante ila moyoni ile kitu haimpi mshituko. Ila ukimpiga sasa au kumtukana matusi ya nguoni nafsi yake inapata msisimko wa kuhisi mahusiano yameanza kuwa active kama kile alichokiona kwa wazazi wake.

Oa binti wa kikurya uone atakavyokulazimisha umkung'ute ili ajihisi yupo musoma[emoji23]

Kuna wale mabinti wametoka familia za mitaala. Yaani baba alikuwa na wake wengi. Ukisema umpende pekee yake inakuwa kero. Anakuwa hajielewi. Ingawa mdomoni anakutamkia kuwa hataki umsaliti ila ndani ya nafsi yake anatamani kusikia au kuona upo na mwanamke mwingine, itamuuma ila atapokea na kuvumilia kama mama yake alivyovumilia.

Mwingine amekulia familia ya kulelewa na mama tu baba hayupo. So ataanza na wewe kimahaba sana mkishapata watoto anaanza kukuletea tabia zisizo ili akukwaze uondoke abakie na watoto aishi vile kama mama yake na yeye na nduguze kipindi cha utotoni.

So ni vema kujua watu wanadeal na takataka gani kichwani before hatujacommit nao.
 
Hakika yaan
 
Duh[emoji17]
 
Kama unajiona kabisa swaga zako kwenye mahusiano una mawenge mengi hebu nenda kaonane na therapist akupe msaada mahusiano sio sehemu ya maumivu tabia zetu ndio hutuletea maumivu na kuwaumiza wengine.
Kabisa
Yaani jmn mtu unampenda,kisa aliumizwa alikotoka nawe anakuumiza bila kosa
Duh inaboa sana

Ila kibongobongo watu huu sio utamaduni wetu ni shida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…