Kama hamtaki kwenda Vijijini tupeni hizo nafasi tunaotaka kwenda

Kujiriwa ni utumimejadiliana na shemeji mume wa dada nimemwambia siwezi kwenda huko ngoja nisubiri nafasi zingine mwakan

Kujiriwa ni utumwa
Anaongea hivi mtu anaishi mjini kwa kutegemea kiuno cha dada ake.
Unadhani siku Shemeji akikasirika unachako hapo?

Anaongea hivi mtu aliyemwambia Shemeji "Nita apply mjini"

Mashemeji wanakazi sanaa ya kulea.

#YNWA
 
Ushakua mtumwa sugu wewe unaamini kuajiriwa ndo kuyapatia maisha tulia utumike
 
Hivi enzi za Magu,mtu angeanza kudekadeka hivyo,eti anataka kubadili kituo huku hata kuripoti Bado,si mzee angetoa maeoekezi ya haraka kua ambao hawataki wasiende na nafasi zao zigawiwe kwa wengine haraka?
Kwanza ngoja nifanye utaratibu wa kuwasiliana na watu wa TAMISEMI,hizo nafasi zichangamkiwe haraka sana,eboo! hivi deadline ya kuripoti ni lini kwa anayejua,ili hayo ma-gepu yajazwe haraka?
Mambo yalishabadilika mkuu, sasa tunaongea kwa uhuru
 
Hoja ya kijinga Sana

Mimi Sina hiyo ajira na nikiipata Form day one tu naanza mchakato wa kuhamia DSM, ungekuwa na Hoja endapo ungesema wanaacha kazi(Hawaripoti kazini) kumbe kuhama vituo ni lengo na ndoto za 99% ya watumishi kuhama vituo.

Njaa usidumaze Reasoning
Bora ukiomba usipate ili hiyo nafasi wapate wengine wenye kiu ya kuishi popote ilia wapate riziki
 
Tanzania ni dsm na mwanza huko kwengine ni maporini na mashambani.

Acha tujazane karibu na dsm...ndio kwenye huduma zote bora za kijamii..maji safi..umeme..miundombinu bora..hospitali vyuo na starehe kama kidimbwi.

Karibu dsm toka huko uswekeni utachakaa.

#MaendeleoHayanaChama

#MaendeleoHayanaChama
Itaje Arusha mjini haraka au hatua kali za kinidhamu zitakufatia
 
Nimepata nafasi lakin ni kijijini sana nimejadiliana na shemeji mume wa dada nimemwambia siwezi kwenda huko ngoja nisubiri nafasi zingine mwakan
Mkuu nenda karipoti kituoni kwako baada ya mwaka unahama, Mimi kutuo changu Cha kazi Cha kwanza kilikuwa Lindi wilaya ya liwale Kijiji Cha Kikulyungu, ni kijijini hasa, baadae nilihamishiwa Mpigamiti huko huko liwale nako ilikuwa kijijini hasa, simu Ni kwa ajili ya kumlikia na kusikiliza miziki, ukiwasiliana na ndugu wakati wa kuja mjini kuchukua mshahara hiyo imetoka hadi mwezi ujao ndo utawasiliana nao tena .

Leo hii Niko eneo la mjini ambako Hadi muda huu na type hapa namtumia smartphone na mtandao unasoma H++
 
Duh
 
Kuna madogo wawili mmoja amepelekwa katavi mwingne kigoma
Wamekataa kwenda kabsaaa
Wapo private hapa dar tunakula maisha
Sasa wanajua Tamisemi ni mambo ya vijijini kwa asilimia kubwa halafu wanaomba hizo nafasi huku wakijua hawatoenda, wamezingua wangeachia wengine hizo nafasi kwa kutoapply
 
Back
Top Bottom